Evelyn Salt Wanawake wengi hukata tamaa ya maisha na hasa walio katika ndoa, huku baadhi yao wakiridhika na kipato cha waume wao, wanacholetewa kila kukicha.
Hali hii inachangia kuwepo kwa migogoro ya hapa na pale kwa baadhi ya wanandoa, inayosababishwa na waume zao kuelemewa na mzigo wa familia. Migogoro hiyo ikikua, husababisha kusambaratika kwa baadhi ya ndoa na kuchangia kutoa watoto wa mitaani na
wengine hutupwa jalalani sasa hapo nature inafaida gani?
Lakini haya yanaweza kuepukika kwa nyie wanawake kujichanganya na wenzenu ili kupata mawazo jinsi ya kuanzisha biashara ndogondogo au kwa jina lingine ujasiriamali, kwa ajili ya kujipatia kipato katika familia, kwa stail hii hata ndoa au mahusiano huimarika zaidi.