Ni ukweli wanawake tegemezi wanaume tunawachukia

Ni ukweli wanawake tegemezi wanaume tunawachukia

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Ni wazi kabisa kwa asilimia kubwa ya wanaume sikuhizi hatutaki kutegemewa kwa kila kitu kwani maisha yamekuwa magumu wakati mwingine unakuta hata sisi wenyewe tunashindwa kujitosheleza kimahitaji.

Hivyo kuwa na mpenzi tegemezi tunaona ni hasara kubwa na kutokana na hilo wanaume tukiona mwanamke pale mwanzo tu baada ya kumtokea mara anaomba vocha, msaada wa kifedha yaani shida zake zote anataka mwanamume amsaidie.

Kiukweli si kitu kizuri ndiyo maana baadhi ya wanaume wakiona tabia kama hizi basi anaanza kukata mawasiliano taratibu mwishowe ukimpigia simu hapokei kabisa.

Na mzigo alishatafuna tena sana tu ni muhimu wanawake muwe na tabia ya kujituma ili msiwe ombaomba kila wakati kwani inawezekana mnachokwa mapema kutokana na nyie kuzidisha virungu vya kijinga jinga.

Acheni ubwegge wa kutengemea wanaume jitumeni na msichague kazi endesheni hata daladala tutawaunga mkono utegemezi wenu umezidi ni janga la kitaifa sasa hivi.

Nakaribisha mjadala.

Cc deejaywillzz lara 1 Munkari kabanga utafiti ICHANA miss neddy miss chagga Mr Rocky na wengine wote
 
Mungu alivosema wanaume tutakula kwa jasho unadhani alikua ana-wink...teh tehh
Basi zaa kwa uchungu mkuu as way of consolation...
Mi naweza kusema ni ulimbuken tu mkuu wamezaliwa wanatakiwa kujituma na siyo kutegemea tu kile anachokuja kukikuta kwa mwanaume ndio maana wengine mahusiano yakiyumba kidogo tu wanaanza kuuza mzigo
Kwa sababu unakuta wengi washalemaa hawawezi kujitafutia wenyewe.
 
Mi naweza kusema ni ulimbuken tu mkuu wamezaliwa wanatakiwa kujituma na siyo kutegemea tu kile anachokuja kukikuta kwa mwanaume ndio maana wengine mahusiano yakiyumba kidogo tu wanaanza kuuza mzigo
Kwa sababu unakuta wengi washalemaa hawawezi kujitafutia wenyewe.
hatukuzaliwa ili kujituma bali tuangalie familia huku nyie mkileta ha ha ha
kutafuta ni kiherehere chetu tu
 
Kuna mmoja humu alisema wao wanataka haki sawa ila sio wajibu sawa. Hao ndio female
 
mwanamke parasite mi simtaki kabisa...kuna wenzangu na mie hadi kwa bedi ni wategemezi hadi umsukume ndio anafanya kazi lasivyo anasoma Mwananchi..
 
.....kiasili mwanaume hujisikia fahari anapomgharamia mkewe kwa kila kitu.....
Kuoa mke anayefanya kazi kunaondoa maana mzima ya kuoa kwa maana mke atakuwa anapokea amri nyingi na mara nyingi mkeo humpati kwa wakati unaomuhitaji....
unaweza ukarudi nyumbani mapema unakuta mkeo bado hajarudi kazini...
unawekewa maji na housegirl unaenda kuoga...unaketi mezani unapata msosi...unaenda kupumzisha mwili kidogo huku! ukimngoja mkeo kipenzi...mpaka usingizi unakupitia...kuja kushtuka saa nne na bado mkeo hajarudi..unampigia simu anakuambia wamepata kikao cha dharura ofisini...unakomaa mpaka saa tano ndio anarudi...anaenda kuoga anapata msosi...huku unamngoje kwa hamu
....anakuja anakuambia mimi leo nimechoka si unajua ofisini kazi zilikuwa nyingi....Mzee unakuwa umeshaikosa papuchi ya mkeo kwa mtindo huo....
 
Kibo10 Mungu si alishagawanyisha majukumu tangu mwanzo ingawa sikatai kusaidiana kupo hii iwe kwa wanandoa ila kwa wanaoibana acha mwanaume awajibike
 
mkuu katika siku ulizoongea point leo yaani leo umeongea bonge la point na utawaona wapo watakaopinga huu uzi.......i!!!
kwa sababu wao hata wakilala wanaota mizinga tu!!!
na mizinga mingine ni indirect yaani unaambiwa nisindikize sehemu ujue kuna kupanda gari, baby twende lunch hapo lazima ujipange, baby tubadilishane simu ujue yako nzuri na harudishi ng'ooo!!! baby yaani huwa sipendi kwenda dukani kununua vocha kuna waavlana wananisumbua kweli hapo anataka ummunge na bando la mwezi.....!!!
 
"nature"....nature ya mwanaume si tu kuwa na wanawake wengi na kula beki tatu na kuhudumia pia ni nature....

mwanaume akishakuhudumia kila kitu lazima atakudharau na haitachukua hata mwezi lazima atafute mchepuko....
mwanamke umekaa tu ndani siku nzima huingizi hata mia alafu utegemee kupendwa!!!!
 
Mmmmhhhh

Sidhani ka kuna mjadala hapo umeshaitimisha mwenyewe.

Nadhani unachotaka ni kuamsha ama kuona reaction ya wadada humu .

But kumbuka kuna wafanyakazi na wanafunzi

BTW mwanamke anayejitambua hawezi kutegemea pesa ya mwanaume labda ka mwanandoa..istoshe kuna wanaume wenye roho zao wanaopenda kuwahudumia wapenzi wao kwa hiari yao wenyewe..

Mwisho Tunashukuru kwa ushauri wako japo umeuleta kiuchokozi zaidi.
 
Mungu alivosema wanaume tutakula kwa jasho unadhani alikua ana-wink...teh tehh
Basi zaa kwa uchungu mkuu as way of consolation...

kula kwa jasho haimaanishi kila kitu uprovide wewe, basi mashuleni na ofisini wasingekuepo wanawake... mbona wengine wanajituma na maisha yanasonga!!!
 
mwanamke mfanyakazi z ofisini ni pasua kichwa sihitaji tabu hiyo atakaa nyumbani sio kuhangaika kila siku
 
Kibo10 Mungu si alishagawanyisha majukumu tangu mwanzo ingawa sikatai kusaidiana kupo hii iwe kwa wanandoa ila kwa wanaoibana acha mwanaume awajibike

Kwa mwanamke anayesema ni wajibu wa mwanaume kuhudumia kila kitu sioi hata unipeleke kwa alshabab..mwanamke anayeweza kujitegemea safi sana, iwe wa kuibana au wa ndoa bado akiwa mtafutaji kuna faida kubwa miss neddy hata siku lolote likikutokea ka unamiradi ataweza kuimanage isife na kukulindia watoto, ni vema kujichukulia wanawake wenye elimu kichwani, na wenye kujitambua hawa wadada wanaofelifeli ovyo walikua wanasumbuliwa na nini?kama sio wanaume wakati wanasoma waliendekeza utegemezi wa kijinga
 
Back
Top Bottom