Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Mh.Spika Sita naomba sana uwatafute hawa wafanyakazi wanaotumiwa na mafisadi uwaondoe maana wanachafua Ofisi ya Bunge.Sitta ni shujaa na amelipa hadhi Bunge.Nyie mnaojiita Wafanyakazi wa Bunge ni wahuni mshindwe na mlegee.
 
Unaendelea kusambazwa kwenye internet kama njugu.Kama ni kweli,kitu ambacho sina wasiwasi nacho,hali inatisha!

Waraka wa wazi kwa Watanzania kutoka kwa watumishi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ufisadi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania

Ndugu zetu Watanzania. Sisi ni wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tunapenda kutumia nafasi hii kuwafikishia ujumbe huu muhimu kupitia waraka wetu huu wazi kwenu.

Tunaomba ifahamike kuwa, haikuwa nia yetu hata kidogo kutumia njia hii kueleza mambo ya siri sana yanayofanyika ndani ya Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Tumelazimika kuchukua hatua hii baada ya jitihada zetu za kufikisha taarifa hizi pamoja na malalamiko yetu ngazi husika kutokufanikiwa. Aidha, mbali na hayo hata juhudi za ziada tulizochukua kuwasiliana na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kueleza uvundo ulio katika taasisi hii hazikufanikiwa kutokana na nguvu ya pesa iliyotumika na ofisi ya bunge kuwafunga midomo waandishi wa habari na wahariri wao.

Lakini kikubwa zaidi kilichotusukuma kuandika waraka huu kwa Watanzania wote ni baada ya kubaini kuwepo kwa njama za kuchoma moto ofisi ya uhasibu ya bunge ili kupoteza kumbukumbu muhimu kabisa za matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi ya ofisi ya bunge yaliyofanywa Spika pamoja na marafiki zake. Tunaomba watanzania waelewe kuwa kuanzia sasa ofisi hizo zitaungua moto wakati wowote. Na kama jambo hili litatokea watanzania wote hasa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndivyo vinavyopaswa kulaumiwa zaidi kwa kushindwa kubaini ufisadi wa kutisha katika ofisi hii hadi njama za kuchoma moto ofisi.

Ndugu zetu Watanzania, tunapenda kuwafahamisha kuwa Ofisi ya Bunge, katika kipindi cha miaka mitatu na ushee, imekuwa ikikaliwa na mafisadi wanaojificha katika jina la vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi, na kiongozi wao wa Mkuu ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Tunajua kuwa wapo baadhi ya Watanzania wenzetu wanaoweza kuona kuwa tunasema mambo ya uongo au tusiyo kuwa na uhakika nayo. Kwa kuthibitisha haya tunayoyasema, tunaomba tueleze mambo machache machafu ya kifisadi yanayofanywa na Spika Sitta pamoja na wabunge kadhaa walio karibuni naye, wakisaidiwa na badhii ya watendaji wenye nyadhifa kubwa katika Ofisi ya Bunge.

  • Tangu Spika alipoingia madarakani amekuwa akiiongoza ofisi ya bunge kidikteta. Analazimisha kupatiwa fedha kutoka katika ofisi ya bunge anapokuwa katika ziara zake binafsi katika Jimbo lake la Urambo Mashariki. Ushahidi wa haya upo katika vocha za malipo haya. Tunaomba wakaguzi waje wakague watakuta haya.

  • Spika Sitta amekula akilazimisha kukiukwa kwa kanuni za bunge ili tu kuwapa nafasi wabunge wenzaki walio katika kambi moja kuisulubu serikali ili kuwaaminisha wananchi serikali ni ya hovyo bali yeye na wabunge hao ndiyo wana uchungu wa kweli na taifa hili.

  • Spika Sitta hafuati taratibu za uchukuaji fedha za ofisi. Huwa anaamrisha apewe hata fedha za kununua vifaa muhimu vya ofisi akiwa hana fedha na anapokuwa akizihitaji. Fedha zilizopotea kwa njia ni mabilioni, lakini hakuna anayemuhoji.

  • Spika Sitta hata siku moja tangu aliposhika wadhfa huo, amekuwa hafuati taratibu za kawaida za sheria ya manunuzi umma katika mambo mengi hapa bungeni. Yota haya ushahidi wake upo ofisi ya uhasibu lakini analindwa na kundi la wabunge wanaodai kuwa wanapoambana na ufisadi kwa* sababua anakula nao.

  • *Spika Sitta ameshinikiza kukodishiwa nyumba ya gharama kubwa. Dola za Marekani 8,000 kwa mwezi wakati alikuwa amepewa nyumba nzuri tu ya serikali huko Oysterbay. Baada ya kukodishiwa Nyumba hii, alilazimisha pia Ofisi ya Bunge itoe sh milioni 250 kwa ajili ya kununua samani za ndani alizodai kuwa ndizo zinazolingana na hadhi yake ya Spika.

  • Spika Sitta ambaye baada tu ya kuingia katika wadhfa wake alinunuliwa gari jipya aina ya benz. Sasa amelichoka likiwa hata halijamaliza miaka mitatu, anataka kununuliwa jingine na amekwishamuarua Katibu wa Bunge, Thomas Kahililah ambaye ni swahiba wake mkubwa kwa sababu wanakula pamoja kutoa kiasi cha sh milioni 367 kwa ajili ya kununulia gari hilo . Tayari zimekwishalipwa sh milioni 270. wakati haya yakifanywa na Spika, anajua fika kuwa taifa liko katika hali mbaya kifedha na bunge liko katika hali mbaya zaidi kiasi kwamba vikao vyake vinakatishwa.

  • Spika Sitta ana sifa mbaya ya ukware. Tangu ameshika wadhfa huo amekwishatembea na wabunge wanawake wa bunge la Jamhuri ya Muunagni ambao ni wake za watu zaidi 12 na ushahidi wa hili upo kwao wenyewe wabunge. Akikanusha hili tunaomba watumwe maofisa usalama waje wafanye uchunguzi kwa siri, watabaini jinsi anavyofanya ufirauni na wake za watu ambao ni wabunge. Anatembea mpaka na wabunge wa upinzani halafu anajitapa kuwa ni Spika wa wote hivyo lazima awalee. Ni aibu lakini huo ndio ukweli.

  • Ni mtu anayevidhalilisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa sababu amekuwa akisema wazi kuwa hakuna chombo chenye nguvu za kumchunguza yeye na bunge kwa sababu bunge ni dola. Na ukweli sasa umeanza kubainika kwa sababu ni dhahili kuwa serikali inamuogopa Spika na timu ya wabunge wake. Ndiyo maana licha ma malalamiko na ushahidi mwingi tuliokwishatoa toa kuhusu ufisadi wake, si TAKUKURU, polisi waka usalama wa taifa waliothubutu hata kumuhoji.

  • Spika amewagawa wafanyakazi wa Bunge wa Idara ya Uhasibu. Wapo ambao amewateua kuwa watu wake ambao wanashughulika na malipo yake yeye, makamishina wa tume ya huduma ya bunge ambao wanakula naye pamoja, pamoja na wabunge kadhaa ambao uchunguzi wa kina ukifanyika watafahamika.

  • Wahasibu hawa pamoja na Kashililah ndiyo wanaolipwa mishahara mikubwa, wanalipwa posho hata kama hawakufanya kazi za ziada na wanasafiri na Spika kila anapokwenda nchi za nje. Watumishi hao ni kama ifuatavyo hapa chini.

  1. Evance Nkanta - Huyu ni muhudumu wa idara ya uhasibu. Ni mtu wa karibu sana na* Spika Sitta pamoja na Mhasibu Mkuu wa Bunge, Bwana Kombe. Cha kushangaza hakifanyi kazi za bunge kama inavyotakiwa, kazi kubwa ni kupeleka fedha katika akaunti ya Spika na Kombe au kupeleka fedha katika miradi yao .

    Nkata ana miradi mingi na utajiri mkubwa wa kutisha. Anamiliki taksi nyingi mjini Dodoma na Dar es Salaam , ana nyumba za kifahali Dar na* Dodoma na anamilioni ya fedha katika benki kadhaa hapa nchini. Ana sauti kubwa kuliko hata baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa bunge. Akataka ufukuzwe kazi anamwambia tu Spika au Kashilalah kuwa kuna matu anafuatilia nyendo zao, kesho mtu huyo anafukuzwa kazi.

    Hii ndio maana Spika na tume yake ya huduma za bunge imepipitisha sheria mpya tofauti na ile iliyosainiwa ya rais inayompa Spika Sitta na tume hiyo madaraka makubwa ya kuajiri au kufukuza mtumishi yoyote, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.

  2. Rose Mlalase - Huyu ameajiliwa hivi karibuni bila kufanyiwa usaili. Ana uhusiano wa kingoni na* Spika Siita. Ndiye mshika mikoba yenye nyaraka za siri za Spika Sitta. Huwa hatumwi na mtu mwingine zaidi ya Spika mwenyewe katika masuala ya kihasibu. Katika muda mfupi usiozidi mwaka mmoja kazini amekwishapa mali nyingi zikiwemo nyumba kadhaa na magari.

    Huwa analipwa posho za vikao na safari za nje bila kufanya kazi yoyote au kusafiri kwa maelekezo ya Spika mwenyewe.

    Mhasibu Mkuu, Bwana Kombe. Ana mabilioni ya shulindi katika benki za CRDB, NMB na NBC. Amejenga hotel ya kisasa inafahamika kwa jina la African Dream, mjini Dodoma kwa kutumia fedha za bunge. Hana sifa za kuwa mhasibu mkuu wa bunge kwa sababu ana cheti cha chini kabisa cha uhasibu badala ya NAD. Amefanya mitihani kadhaa ya uhasibu lakini anashindwa.

    Bwana Kombe, akitaka pesa kwa ajili ya kupeleka kwenye miradi yake huwa anajiidhinishia hadi milioni 100. ndiye anatoa fedha za bunge kwa ajili ya shughuli binafsi za Spika. Anahusika kulipa yeye mwenyewe malipo yoyote kwa mbunge ambaye Spika ataamuru alipwe bila maelezo yoyote kuhusu kutolewa kwa fedha hizo.

  3. Hassan Mohamed - alifeli diploma ya uhasibu mwaka 2005 katika chuo cha uhasibu Arusha. Hivi sasa anasoma IFM. Yuko chuoni lakini ndiyo msimamizi mkuu wa masuala ya fedha katika ofisi ndogo ya bunge mjini Dar es Salaam. Naye ana utajiri wa kutisha ambao haulingana hata kidogo na kipato chake na umri wake kazini.

  4. John Joel - Ni mhasibu lakini kwa sasa amehamishiwa katika ofisi ya utawala. Mdiyo msiri mkuu wa Kashililah kiasi kwamba akisafiri ofisi huwa anaiacha mikononi mwake. Ameteuliwa hajamaliza kata miezi minne lakini sasa anawazifdi hata walio na miaka 10 kazini.

  5. Bwana Mtenda - Huyu alichukuliwa na Spika mwenyewe na kuwekwa uhasibu pasipo kwa sababu ambazo mpaka sasa haziko wazi. Lakini ndi miongoni mwa watu wanaohusika kushughulikia vocha za malipo ya* Spika, makamishina na Tume ya huduma za bunge na kundi la wabunge marafiki wa Spika Sitta.

    Mtenda ana historia mbaya katika utumishi wa umma lakini inashangaza kuona Spika Sitta akiwa amemng’ang’ani katika kufanya kazi ofisi ya bunge. Alikuwa mtumishi wa idara ya ustawishaji makao makuu Dodoma (CDA) ambako aliondolewa kutokana na kuandamwa na kesi lukuki ambazo almanusura zimpeleke gerezani.

    Kila mara huwa anachukua fedha kwa ajili ya kwenda semina nje ya nchi lakini huwa anaishia Dar es Salaam kuponda na baadaye kurudi Dodoma . Haifahamiki ni kwanini anafanyiwa hivi na wakubwa.

  6. Bwana Ndalo - huyu ndiye anayechukua masurufu yote ya Spika Sitta. Anahusika kuwalipa wote walio katika orodha ya kulipwa na* Spika, iwe wanasiasa au watu binafsi. Ni kama kichwa cha* Spika.* Huwa anavchukua masurufu mengi hadi anashindwa kurudisha.
Kwa ufupi sana hii ndiyo timu ya Spika Sitta hapa bungeni. Timu ambayo inashirikiana nayo kujitajilisha kupitia bunge.

Tunawaomba* Watanzania mfahamu kuwa Serikali inamuogopa Spika Sitta kwa sababu amefanikiwa kuwa na nguvu kubwa ya wabunge wenye uwezo mkubwa wa kuongea na kujenga hoja zao. Inafahamu fika ufisadi unaofanyika hapa kuwa ni mkubwa kuliko hata ule wa Richmond lakini kamwe haiwezi kuthubutu kumgusa Spika Sitta kwa vile anaweza kuiangusha. Hivyo kwenu Watanzania wote kama tunaamua kukaa kimya huku haya yakiendelea sawa au tuchukue hatua ya kushinikiza uchunguzi huru kufanyika.

Kama wafanyakazi wa kawaida, kwa kizingatia baadhi ya wabunge akiwemo Spika wanavyohuburi vita dhidi ya ufisadi na mambo yanayofanyika hapa tumeona bi bora kuyaweka wazi ili watanzania waamke na kushinikiza kuundwa tume huru ya kuchunguza ufisadi ndani ya ofisi ya Spika.

Waraka huu tunaomba ukikufikia upeleke kwa mtanzania mwenzako ili sote tujue jinsi wakubwa wetu tuliowachagua kwa kura zetu wanavyoishi maisha ya utukufu huku wakituhadaa kuwa wanapambana na wanatumia jasho letu kihiana kuishi maisha ya utukufu. Tuwezalo tumefanya kwa faida ya taifa letu. Mungu ni shahidi yetu.

Huu ndio ujumbe wetu.

Asanteni sana .

Mungu Ibariki Tanzania ...

*
**
 
watu wajungu utajua tu jamaani mue na ma documento sio mna weka tu vitu ama tuseme muache Tabia ya ku copy na ku paste vihadisi mnavyo okota kama alivyo andika HOFSTEDE ,mimi naona hapa watu wanapakana matope tu kwa ajili ya uchaguzi mwakani 2010 hakuna la ziada. eti wafanyakazi wa bunge lol, moderator funga upuuzi huu

Gray Mgonja afikishwa mahakamani

ngoja wampe mdhamana mtaona !! atakimbia nchi hata kama watashika passport yake.mke wake na watoto wote wanaishi California Marekani.

hana lakumuweka bongo.passport ziko nje nje hapo bongo

Homeboy,

Naona kaka Sita akikamatwa pabaya, unawaka moto vibaya sana.

Siyo siri kuwa kaka Sita nilikuwa nategemea awe ametemwa siku nyingi hasa walivyokomba zile hela za CDA. Sijui iliisha ishaje? Anyway, jamaa na yeye ni Jisamake siku hizi kwenye bwawa la Tanzania.

Mkuu, wee uliandika maneno kibao hapo juu kuwa Mgonja atakimbilia Marekani
Re: Magreth sitta nae kaanza!
kuchafuliana majina tu , huna evidence yoyote ndugu M-bongo,lete topic nyingine .wewe hujashitukia watu hawataki kuchangia lolote wanaona huna facts , eti waziri mzima akasimamishe basi na kuanzaa kugawa pesa mhhhh yani unamuona mjinga kiasi gani afanye hivyo katika kipindi hichi cha siasa hapo nchini karibu kila kiongozi yuko muoga na rushwa halafu eti agawe pesa weeeee wee hebu acha utani wako humu jamvini.lete topic mpya

Na chini ukawa umeahidi kutuletea DATAS kama wee unavyodai kila siku na UKAUCHUNA. Magreth Sitta anabaki na yeye kuwa kafisadi kalikotoa pesa ili kapigiwe kura Tabora...

Re: Magreth sitta nae kaanza!

bw, m-bongo
baada ya kufuatilia hii hoja yako nataka nikufamishe kuwa mwandishi wetu alieko isevya ttabora ambae alikuwepo anasema kwamba mama six alifika ukumbini akitokea uwanja wa ndege moja kwa mmoja kuelekea ukumbini maana ndege ndogo iliowaleta na watu wengine ilifika ikiwa imechelewa, sasa swali langu kwako ni muda gani mtu atapata wa kugawa hizo fuedha ? Na habari zaidi zinasema waligeuza siku hiyo hiyo. Na nimeomba nipatiwe mpaka gari alilopanda na namba zake ili tuwakilishe hapa na pia muandishi wetu anajaribu kumsaka dereva alie muendesha ili atueleze zaidi kaa mkao wa kula....more to come

Hii Isevya Ttabora una maana ya Tabora? Kama ni hiyo basi lazima ufahamu kuwa Isevya na ilipo Airport ni mbalimbali. Airport iko kama unaenda Kipalapala kwa njia ya barabara (Itetemya) na Dar es Salaam kama waenda kwa reli. Wakati huo, Isevya iko njia ya kwenda Nzega.
 
Msitubabaishe kwani na nyinyi ni mafisadi kama hao mliowataja ,kila siku tunasema kama kuna machafu kwanini mnang'ang'ania tu ,hivi kwa kwanini hamuachii hivyo vyeo na kujiunga na upande wa upinzani ,ndio maana yake kijeshi tunasemAGA KULYAAAA CHAWANYIKA ,sasa mnasubiri nini ,aondoke spika na watu wake mpishwe nyinyi ?

WaTanzania hatutaki kusikia mnatoa waraka ,hii ni sampuli ya watu wa dini iliyoingia siku hizi achaneni nayo ,kila mmoja kwa upande wake ahame na kuhamia kwengine ,ita vyombo vya wadaku ubwage manyanga mbele yao huku unatapika kila kitu na hapo kila mTz atasikia harufi na kunusa na kuona kumbe wapo wanaoweza kufanya kweli ,mbona WaPemba wameikataa na wanaikataa CCM hadharani tena mchana kweupe ,maana kufika UN si jambo dogo na mpaka leo wapo hivyo hivyo walivyo na kuteswa kote lakini wameapa kwamba hawataichagua tena CCM ,liwalo na liwe.

Sasa huu mnaoonyesha nyinyi ni undumila kuwili ugoigoi ,kama haitoshi WaZanzibari Mawaziri kiasi ya kumi na moja walitimuliwa hapo bungeni na katika serikali za CCM kutokana na kutokubaliana na baadhi ya mambo ya kiutawala ,na mpaka leo wapo wengine wamekuwa wabunge mashuhuri sana . Sasa nyinyi mnaleta mambo ya kike kabisa ,maana hii ni fitna na si vinginevyo ,ni umbea ni udaku.

yaani manshindwa kuelewa kuwa ni juzi tu ndio tumepata fibre Optoc cable ya simu ambayo haijulikani ni lini waTanzania walio wengi wataweza kufaidika ,na itachukua miaka mingapi kuweza nao kujumuika hapa JF.

Maana hata huu ambao mumeuita waraka au utambi naona utafulia tu haufiki mbali kwani mwanamme wa kweli hawezi akauchukua na kuupeleka anakokujua yeye ili iwe ni uthibitisho wa utapeli na wizi wa moja kati ya magenge yenu hapo Dodoma Bungeni ,kwani hata hivyo vielelezo havipo ni anaetaka afunge safari aingie bungeni ,sasa hata akifika hapo akikuuliza wewe basi si ajabu ukamjibu hujawahi kusikia na unaona mambo ni kawaida tu.

Wacheni undumila kuwili ili wananchi wajue kama ni kusuka au kunyoa.
 
hii habari inaonekana kupikwa na kuungwa vizuri sana, jamaa aliyeitayarisha ni mpishi mzuri sana. Hakika amefuzu kuajiriwa na kundi la mafisadi na kulipwa fedha nyingi sana.
 
Lisemwalo lipo!

Ushahidi wa nini zaidi hapa JF?? kwani mengine huletwa ushahidi wa namna gani??

Watu bwana!!!
 
Mh.Spika Sita naomba sana uwatafute hawa wafanyakazi wanaotumiwa na mafisadi uwaondoe maana wanachafua Ofisi ya Bunge.Sitta ni shujaa na amelipa hadhi Bunge.Nyie mnaojiita Wafanyakazi wa Bunge ni wahuni mshindwe na mlegee.

Na wewe upo kwenye payroll?
 
Kumjadili mtu kwa maovu bila kuwa na vithibitisho ni kumwonea na kumchafulia jina. Wale wafanyakazi kama wanataka tumtendee haki mzee Sitta hapa jamvini watuletee hizo documents zinazo-support madai yao. Maneno matupu si msingi imara wa kuanza kumjadili mtu. Watoe walau vithibitisho vichache. Hatuwezi kuwaamini tu kwa kuwa wameandika kwa maneno ya uchungu mkubwa. Please evidences!

Tukianza kujadili watu bila ushahidi tutaingizwa mkenge na wengi sana humu. Watu wataletana humu ili kumalizana. Kwa mwndo huo hatutafika mbali.
 
"Waraka wa wazi wa Ufisadi ndani ya Bunge"
Wewe ni muongo acha majungu.umesahau unaongea na watanzania ambao kwa sasa wanafahaamu mafisadi ni akina nani tena kwa msaada mkubwa wa hao wabunge unao wakosoa. mafisadi wanatajwa kwa majina, nyaraka, na tena mbugeni mchana kweupe. sio unavyokuja gizani bila hata nyaraka. Bajeti ya matumizi ya bunge haya hayasaidii maendeleo ya wananchi.kama matatitizo yenu kazini ungeleta hapa majibu ya barua zako za malalamiko.rudi kwa Rostam AZIZ akufunde vizuri
 
Hivi hawa wanaodai ushahidi wanapinga nini hasa :-
1. Kwamba wafanyakazi waliotajwa si waajiriwa wa bunge ?
2. Kuwa Bwana Kombe si mhasibu mkuu wa bunge na hana sifa ?
3. Kwamba Mh. Sitta hakuwahi kuwa mkuu wa CDA ?
4. Kwamba Bwana Mtenda hakuwahi kufanya kazi CDA ?
5. Kwamba Mh. Sitta hakununuliwa benz mpya na sasa anasubiri gari jipya la dola zaidi ya 300,000. ?
6. Kwamba Mh. Sitta amehamia nyumba ambayo pango lake ni dola 8,000 kwa mwezi ?
7. Kwamba Spika Sitta hakuzuia mjadala wa Richmond hadi awepo - kama huu si ubabe ni nini ?
8. Kwamba, kwamba ...... duh, I could go on and on !!

Nina ujumbe kwa wote wanaoogopa kumkoma nyani kwa kumwangalia uso kuwa hiyo hairuhusiwi hapa JF. Hapa hatuangalii jinsia, itikadi, cheo, rangi, umri, dini wala nini - kama kuna kaharufu ya kifisadi, basi ni halali yetu kumkoma nyani giledi awe JK, EL, Chakaar, Patel, Vijisenti, Idris, Mkapa, Mwinyi, Hosea bila kumsahau Spika Sitta.

Tatizo wengine ama ni wageni au wana umri mdogo - haka ka-nchi kametafunwa sana na kwa siku nyingi. Hivi sasa imefikia wakati wa kutooneana aibu tena, wakati wa kuita koleo kwa jina lake na wakati wa kuufungulia milango mwanga tuwamulike hawa wanga wanaoitafuna nchi kama vile haina wenyewe - hapana, wenyewe tupo.
 
WanaJF, nimesukumiwa hii barua pepe na mdau fulani nami nikaonelea ni bora niianike jamvini ili kupata ukweli wa haya mambo, kweli politiki its a dirty game ...........

Ndugu zetu Watanzania. Sisi ni wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , tunapenda kutumia nafasi hii kuwafikishia ujumbe huu muhimu kupitia waraka wetu huu wazi kwenu.

Tunaomba ifahamike kuwa, haikuwa nia yetu hata kidogo kutumia njia hii kueleza mambo ya siri sana yanayofanyika ndani ya Ofisi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Tumelazimika kuchukua hatua hii baada ya jitihada zetu za kufikisha taarifa hizi pamoja na malalamiko yetu ngazi husika kutokufanikiwa. Aidha, mbali na hayo hata juhudi za ziada tulizochukua kuwasiliana na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini kueleza uvundo ulio katika taasisi hii hazikufanikiwa kutokana na nguvu ya pesa iliyotumika na ofisi ya bunge kuwafunga midomo waandishi wa habari na wahariri wao.

Lakini kikubwa zaidi kilichotusukuma kuandika waraka huu kwa Watanzania wote ni baada ya kubaini kuwepo kwa njama za kuchoma moto ofisi ya uhasibu ya bunge ili kupoteza kumbukumbu muhimu kabisa za matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi ya ofisi ya bunge yaliyofanywa Spika pamoja na marafiki zake. Tunaomba watanzania waelewe kuwa kuanzia sasa ofisi hizo zitaungua moto wakati wowote. Na kama jambo hili litatokea watanzania wote hasa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndivyo vinavyopaswa kulaumiwa zaidi kwa kushindwa kubaini ufisadi wa kutisha katika ofisi hii hadi njama za kuchoma moto ofisi.

Ndugu zetu Watanzania, tunapenda kuwafahamisha kuwa Ofisi ya Bunge, katika kipindi cha miaka mitatu na ushee, imekuwa ikikaliwa na mafisadi wanaojificha katika jina la vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi, na kiongozi wao wa Mkuu ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta. Tunajua kuwa wapo baadhi ya Watanzania wenzetu wanaoweza kuona kuwa tunasema mambo ya uongo au tusiyo kuwa na uhakika nayo. Kwa kuthibitisha haya tunayoyasema, tunaomba tueleze mambo machache machafu ya kifisadi yanayofanywa na Spika Sitta pamoja na wabunge kadhaa walio karibuni naye, wakisaidiwa na badhii ya watendaji wenye nyadhifa kubwa katika Ofisi ya Bunge.

*Tangu Spika alipoingia madarakani amekuwa akiiongoza ofisi ya bunge kidikteta. Analazimisha kupatiwa fedha kutoka katika ofisi ya bunge anapokuwa katika ziara zake binafsi katika Jimbo lake la Urambo Mashariki. Ushahidi wa haya upo katika vocha za malipo haya. Tunaomba wakaguzi waje wakague watakuta haya.

*Spika Sitta amekula akilazimisha kukiukwa kwa kanuni za bunge ili tu kuwapa nafasi wabunge wenzaki walio katika kambi moja kuisulubu serikali ili kuwaaminisha wananchi serikali ni ya hovyo bali yeye na wabunge hao ndiyo wana uchungu wa kweli na taifa hili.

*Spika Sitta hafuati taratibu za uchukuaji fedha za ofisi. Huwa anaamrisha apewe hata fedha za kununua vifaa muhimu vya ofisi akiwa hana fedha na anapokuwa akizihitaji. Fedha zilizopotea kwa njia ni mabilioni, lakini hakuna anayemuhoji.

*Spika Sitta hata siku moja tangu aliposhika wadhfa huo, amekuwa hafuati taratibu za kawaida za sheria ya manunuzi umma katika mambo mengi hapa bungeni. Yota haya ushahidi wake upo ofisi ya uhasibu lakini analindwa na kundi la wabunge wanaodai kuwa wanapoambana na ufisadi kwa sababua anakula nao.

*Spika Sitta ameshinikiza kukodishiwa nyumba ya gharama kubwa. Dola za Marekani 8,000 kwa mwezi wakati alikuwa amepewa nyumba nzuri tu ya serikali huko Oysterbay. Baada ya kukodishiwa Nyumba hii, alilazimisha pia Ofisi ya Bunge itoe sh milioni 250 kwa ajili ya kununua samani za ndani alizodai kuwa ndizo zinazolingana na hadhi yake ya Spika.

*Spika Sitta ambaye baada tu ya kuingia katika wadhfa wake alinunuliwa gari jipya aina ya benz. Sasa amelichoka likiwa hata halijamaliza miaka mitatu, anataka kununuliwa jingine na amekwishamuarua Katibu wa Bunge, Thomas Kahililah ambaye ni swahiba wake mkubwa kwa sababu wanakula pamoja kutoa kiasi cha sh milioni 367 kwa ajili ya kununulia gari hilo . Tayari zimekwishalipwa sh milioni 270. wakati haya yakifanywa na Spika, anajua fika kuwa taifa liko katika hali mbaya kifedha na bunge liko katika hali mbaya zaidi kiasi kwamba vikao vyake vinakatishwa.

*Spika Sitta ana sifa mbaya ya ukware. Tangu ameshika wadhfa huo amekwishatembea na wabunge wanawake wa bunge la Jamhuri ya Muunagni ambao ni wake za watu zaidi 12 na ushahidi wa hili upo kwao wenyewe wabunge. Akikanusha hili tunaomba watumwe maofisa usalama waje wafanye uchunguzi kwa siri, watabaini jinsi anavyofanya ufirauni na wake za watu ambao ni wabunge. Anatembea mpaka na wabunge wa upinzani halafu anajitapa kuwa ni Spika wa wote hivyo lazima awalee. Ni aibu lakini huo ndio ukweli.

*Ni mtu anayevidhalilisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa sababu amekuwa akisema wazi kuwa hakuna chombo chenye nguvu za kumchunguza yeye na bunge kwa sababu bunge ni dola. Na ukweli sasa umeanza kubainika kwa sababu ni dhahili kuwa serikali inamuogopa Spika na timu ya wabunge wake. Ndiyo maana licha ma malalamiko na ushahidi mwingi tuliokwishatoa toa kuhusu ufisadi wake, si TAKUKURU, polisi waka usalama wa taifa waliothubutu hata kumuhoji.

*Spika amewagawa wafanyakazi wa Bunge wa Idara ya Uhasibu. Wapo ambao amewateua kuwa watu wake ambao wanashughulika na malipo yake yeye, makamishina wa tume ya huduma ya bunge ambao wanakula naye pamoja, pamoja na wabunge kadhaa ambao uchunguzi wa kina ukifanyika watafahamika.

*Wahasibu hawa pamoja na Kashililah ndiyo wanaolipwa mishahara mikubwa, wanalipwa posho hata kama hawakufanya kazi za ziada na wanasafiri na Spika kila anapokwenda nchi za nje. Watumishi hao ni kama ifuatavyo hapa chini.

1-Evance Nkanta- Huyu ni muhudumu wa idara ya uhasibu. Ni mtu wa karibu sana na Spika Sitta pamoja na Mhasibu Mkuu wa Bunge, Bwana Kombe. Cha kushangaza hakifanyi kazi za bunge kama inavyotakiwa, kazi kubwa ni kupeleka fedha katika akaunti ya Spika na Kombe au kupeleka fedha katika miradi yao .

Nkata ana miradi mingi na utajiri mkubwa wa kutisha. Anamiliki taksi nyingi mjini Dodoma na Dar es Salaam , ana nyumba za kifahali Dar na Dodoma na anamilioni ya fedha katika benki kadhaa hapa nchini. Ana sauti kubwa kuliko hata baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa bunge. Akataka ufukuzwe kazi anamwambia tu Spika au Kashilalah kuwa kuna matu anafuatilia nyendo zao, kesho mtu huyo anafukuzwa kazi. Hii ndio maana Spika na tume yake ya huduma za bunge imepipitisha sheria mpya tofauti na ile iliyosainiwa ya rais inayompa Spika Sitta na tume hiyo madaraka makubwa ya kuajiri au kufukuza mtumishi yoyote, jambo ambalo ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.

2-Rose Mlalase- Huyu ameajiliwa hivi karibuni bila kufanyiwa usaili. Ana uhusiano wa kingoni na Spika Siita. Ndiye mshika mikoba yenye nyaraka za siri za Spika Sitta. Huwa hatumwi na mtu mwingine zaidi ya Spika mwenyewe katika masuala ya kihasibu. Katika muda mfupi usiozidi mwaka mmoja kazini amekwishapa mali nyingi zikiwemo nyumba kadhaa na magari.

Huwa analipwa posho za vikao na safari za nje bila kufanya kazi yoyote au kusafiri kwa maelekezo ya Spika mwenyewe.

Mhasibu Mkuu, Bwana Kombe. Ana mabilioni ya shulindi katika benki za CRDB, NMB na NBC. Amejenga hotel ya kisasa inafahamika kwa jina la African Dream, mjini Dodoma kwa kutumia fedha za bunge. Hana sifa za kuwa mhasibu mkuu wa bunge kwa sababu ana cheti cha chini kabisa cha uhasibu badala ya NAD. Amefanya mitihani kadhaa ya uhasibu lakini anashindwa.

Bwana Kombe, akitaka pesa kwa ajili ya kupeleka kwenye miradi yake huwa anajiidhinishia hadi milioni 100. ndiye anatoa fedha za bunge kwa ajili ya shughuli binafsi za Spika. Anahusika kulipa yeye mwenyewe malipo yoyote kwa mbunge ambaye Spika ataamuru alipwe bila maelezo yoyote kuhusu kutolewa kwa fedha hizo.

3-Hassan Mohamed-alifeli diploma ya uhasibu mwaka 2005 katika chuo cha uhasibu Arusha. Hivi sasa anasoma IFM. Yuko chuoni lakini ndiyo msimamizi mkuu wa masuala ya fedha katika ofisi ndogo ya bunge mjini Dar es Salaam. Naye ana utajiri wa kutisha ambao haulingana hata kidogo na kipato chake na umri wake kazini.

4- John Joel- Ni mhasibu lakini kwa sasa amehamishiwa katika ofisi ya utawala. Mdiyo msiri mkuu wa Kashililah kiasi kwamba akisafiri ofisi huwa anaiacha mikononi mwake. Ameteuliwa hajamaliza kata miezi minne lakini sasa anawazifdi hata walio na miaka 10 kazini.

5-Bwana Mtenda- Huyu alichukuliwa na Spika mwenyewe na kuwekwa uhasibu pasipo kwa sababu ambazo mpaka sasa haziko wazi. Lakini ndi miongoni mwa watu wanaohusika kushughulikia vocha za malipo ya Spika, makamishina na Tume ya huduma za bunge na kundi la wabunge marafiki wa Spika Sitta.

Mtenda ana historia mbaya katika utumishi wa umma lakini inashangaza kuona Spika Sitta akiwa amemng’ang’ani katika kufanya kazi ofisi ya bunge. Alikuwa mtumishi wa idara ya ustawishaji makao makuu Dodoma (CDA) ambako aliondolewa kutokana na kuandamwa na kesi lukuki ambazo almanusura zimpeleke gerezani.

Kila mara huwa anachukua fedha kwa ajili ya kwenda semina nje ya nchi lakini huwa anaishia Dar es Salaam kuponda na baadaye kurudi Dodoma . Haifahamiki ni kwanini anafanyiwa hivi na wakubwa.

6- Bwana Ndalo- huyu ndiye anayechukua masurufu yote ya Spika Sitta. Anahusika kuwalipa wote walio katika orodha ya kulipwa na Spika, iwe wanasiasa au watu binafsi. Ni kama kichwa cha Spika. Huwa anavchukua masurufu mengi hadi anashindwa kurudisha.

Kwa ufupi sana hii ndiyo timu ya Spika Sitta hapa bungeni. Timu ambayo inashirikiana nayo kujitajilisha kupitia bunge.

Tunawaomba Watanzania mfahamu kuwa Serikali inamuogopa Spika Sitta kwa sababu amefanikiwa kuwa na nguvu kubwa ya wabunge wenye uwezo mkubwa wa kuongea na kujenga hoja zao. Inafahamu fika ufisadi unaofanyika hapa kuwa ni mkubwa kuliko hata ule wa Richmond lakini kamwe haiwezi kuthubutu kumgusa Spika Sitta kwa vile anaweza kuiangusha. Hivyo kwenu Watanzania wote kama tunaamua kukaa kimya huku haya yakiendelea sawa au tuchukue hatua ya kushinikiza uchunguzi huru kufanyika.

Kama wafanyakazi wa kawaida, kwa kizingatia baadhi ya wabunge akiwemo Spika wanavyohuburi vita dhidi ya ufisadi na mambo yanayofanyika hapa tumeona bi bora kuyaweka wazi ili watanzania waamke na kushinikiza kuundwa tume huru ya kuchunguza ufisadi ndani ya ofisi ya Spika.

Waraka huu tunaomba ukikufikia upeleke kwa mtanzania mwenzako ili sote tujue jinsi wakubwa wetu tuliowachagua kwa kura zetu wanavyoishi maisha ya utukufu huku wakituhadaa kuwa wanapambana na wanatumia jasho letu kihiana kuishi maisha ya utukufu. Tuwezalo tumefanya kwa faida ya taifa letu. Mungu ni shahidi yetu.

Huu ndio ujumbe wetu.
Asanteni sana .
Mungu Ibariki Tanzania
 
Watu walioandika waraka huu hawasemi ukweli. Serikali haimuogopi spika hata kidogo. Taarifa yenyewe ina makosa mengi ya kiuandishi, ambayo inaonyesha hawa walikuwa wanaandika halafu wanafutafuta kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa yale waliyokuwa wanaandika. Ni ya kubuni. Hawa waandishi wa huu waraka ni wakosaji. Wangependa na wenyewe wale au wawe mafisadi ila wamedhibitiwa, hivyo wanaleta hizi chokochoko zisizo na miguu. Inaonekana hawa si waadilifu au waaminifu kazini na wataendelea kulalamika na kutumiwa na maadui wa spika Sitta.

Spika Sitta ameleta demokrasia kubwa bungeni kuliko ilivyokuwa wakati wa Msekwa. Ana ujasiri wa kukataa mambo anayoona yanadhoofisha demokrasia bungeni. Mfano ni alivyoshughulikia swala la Zitto Kabwe inaonyesha huyu spika alivyo imara, na mengine mengi yafananayo na hilo.

Hivyo mimi nayakataa yote yaliyoelezwa kwenye waraka na hawa watumishi wa Bunge ambao wanatumiwa au wamezibiwa mianya ya kuiba hela ya Bunge. Bravo Sitta!!!
 
Kabisa ni majungu ya kutaka kumchafua na kwa vile ni karibu na uchaguzi basi imekuwa ni hadithi za alfulelaulela tu. Waje na proof hapo tutaona ni kweli lakini siyo kuleta za kuleta hapa. Ila wenye kazi zao na wanuse huko kama wanaweza kupata chochote. Kwangu mimi haiingii akilini asilani.

Wamekwisha ona kuwa yule mzee ni kisiki sasa watampita vipi basi bora wamchafue na kama ni kweli kwa nini wasianze huko huko bungeni badala yake wanaleta kwenye mitandao na tena wanahakikisha imepita kwenye jamii kubwa? Mungu mwenyewe atawaumbua kila mtu baada ya kufika kwenye 18 ya mwenye sura ya upole!!!!
 
Bravo Mkuu wangu, hawa wanataka kutulengesha hapa sasa iwe kila mtu akitaka kumwanika na kumchafulia mtu alete ishu yake hapa nooo hapa si pake ziko sehemu za kupeleka production kama hiyo na wenyewe wenye kazi yao watafurahi sana.
 
duuh nimechoka kabisa kama haya madai ni kweli tumekwisha watanzania
 
Back
Top Bottom