Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Baada ya kuchoshwa na tuhuma nyingi zinazoelekezwa kwake kupitia magazetini, muda mfupi uliopita spika samwel sitta amesema tuhuma hizo zinapikwa na watu wasiompenda wakiyatumia magazeti ya tanzania daima na tazama. Huko nyuma tuliwahi kusikia kuwa wahariri wa gazeti la tanzania daima (absalom kibanda na charles mulinda) wamenunuliwa na mafisadi wakiongozwa na r.a. Ili kuwashambulia maadui zao, akiwemo spika sitta. Hawa wamekuwa pia wakilitumia pia jamvi hili la jf kupenyezaa upuuzi wao. Akizungumza kwa kujiamini spika ameonyesha kukerwa zaidi na tuhuma kwamba anapanga njama za kuchoma ofisi za bunge ili kuharibu ushahidi wa baadhi ya tuhuma. Sasa amemuomba waziri mkuu amuongezee ulinzi kwani anadhani watu hao ni hatari.
 
lakini wahenga walisema lisemwalo lipo kama halipo linakuja.

Jamani wana JF ,nadhani dereva wa spika atakuwa anajua mengi zaidi, ni nani huyo dereva, nipe data zake tafadhali
 
tatizo kubwa ni kuogopa kivuli na inapofikia mtu mzima kama yeye kuanza kulia lia hadharani ujue mambo hayamuendei vizuri. japo siamini sana katika yale aliyosema leo bungeni kuwa anaha kika ya kurudi tena bungeni na kuwa spika
 
Baada ya kuchoshwa na tuhuma nyingi zinazoelekezwa kwake kupitia magazetini, muda mfupi uliopita spika samwel sitta amesema tuhuma hizo zinapikwa na watu wasiompenda wakiyatumia magazeti ya tanzania daima na tazama. Huko nyuma tuliwahi kusikia kuwa wahariri wa gazeti la tanzania daima (absalom kibanda na charles mulinda) wamenunuliwa na mafisadi wakiongozwa na r.a. Ili kuwashambulia maadui zao, akiwemo spika sitta. Hawa wamekuwa pia wakilitumia pia jamvi hili la jf kupenyezaa upuuzi wao. Akizungumza kwa kujiamini spika ameonyesha kukerwa zaidi na tuhuma kwamba anapanga njama za kuchoma ofisi za bunge ili kuharibu ushahidi wa baadhi ya tuhuma. Sasa amemuomba waziri mkuu amuongezee ulinzi kwani anadhani watu hao ni hatari.

Hivi hayo ni maneno ya Sitta hau ni yako mzee. Naona umeleta hii halafu tayari ushachagua upande. Naona mwenzetu umetumwa!!!!!!
 
bado mazoea yatatusumbua sana! sikuamini macho yangu pale nilipomuona na kumsikia SS bungeni, akitamba ,aking'aka kuwa lazima atakuwa tena mbunge wa urambo, na lazima atakuwa tena Spika katika bunge lijalo hivi hayo ni maneno ya kuongea mtu mzima kama yeye tena mwenye dhamana kubwa katika chombo cha maamuzi yaani bunge? Sita its your time to quit! we are fed up
 
katika kile nilichokiona kuwa ni dalili za kukata tamaa kwa SS leo asubuhi Mh huyo alitoa kauli zenye utata huku akijua kabisa anavunja taratibu za katiba ya CCM hasa pale alipo sisitiza kuwa lazima yeye atakuwa ni mbunge wa Urambo katika uchaguzi mkuu ujao lakini lazima pia atakuwa Spika wa bunge lijalo, hivi mh SS hafahamu kuwa ili kuwa mbunge na hasa kupitia CCM lazima kwanza jina lako liteuliwe na kamati yako ya siasa ya wilaya husika ili tu uwe mgombea kwenye kura za maoni na baada ya hapo vikao vya wilaya na mkoa vikae kujadili matokeo ya kura za maoni na mwisho vikao kamati kuu na NEC navyo vikae na kufanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea? hiyo haitoshi bado mteuliwa husika atahitaji kuingia katika uchaguzi mkuu wa serikali utakaoshirikisha vyama vyote vyenye usajiri, hiyo haitoshi, ukishinda kuwa mbunge utahitaji kuomba kuteuliwa kuwa mgombea U-spika kwa nafasi hiyo ya Ubunge au vinginevyo na ukiteuliwa kuwa mgombea itakulazimu kuingia kwenye uchaguzi ambao wawezashinda au shindwa. kwa hatua hizo zote mh SS anataka tumueleweje kwa kuiambia jamii kuwa yeye lazima atakuwa Mb, na lazima atakuwa Spika? Je Spika anaitisha CCM kuwa lazima imteue kwa nafasi zote atakazo omba?
 
Last edited:
Kusema kweli spika 6 anapendwa na wengi wa watumishi wa bunge, kwani wakati akitamka hayo, nikiwa humu mjengoni, watumishi walishangilia aliposema na nitakuwa mimi spika tena wa bunge lijalo.
 
No different from any other CCM leaders who believe they were anointed to be in certain positions for life. Kama kweli kasema hivyo basi ana reflect watu wengi na siyo viongozi wa CCM au wana siasa tu. He just said out loud what many have in their hearts and that is to lead for as lond as they can thinking they are irreplaceable.
 
Taratibu na katiba kifungu kipi cha katiba ya CCM?. Je wanaosema JK ataendelea kuwa president wakati wakijua mwakani kuna uchaguzi wanavunja katiba,? hakika mmejipanga
 
Pasco si ajabu kumuona katekista akifurahia padri wake kuteuliwa kuwa paroko au askofu kwa maana inamhakikishia maisha yake ya kesho hao waliofurahia walionekana kwako tu maana kumbuka bunge linaonekana dunia nzima labda kitu kimoja wabunge wengi walipiga meza nadhani wengi kwa kushangaa spika anavyonyesha ubabe wake kuwa lazima alitakalo liwe
 
afadhali leo kawatolea uvivu tanznia daima full aibu laziama tuseme ukweli spika sitta ameboresha Bunge kwa kiasi kikubwa kiasi cha mawaziri kuongeza uwajibikaji hata kama anakula pesa poaa tu ilimradi Bunge linakuwa imara . Msekwa amekula wee na Bunge likwa muhuri wa serikali tu so hawa nafisadi , kibanda absolom, charles mullinda ni sawa tu na wanyma wakufugwa wasiojitafutia namuomba mbowe awatimue mara moja huko kwani huko mbeleni watamwaribia hadi CHADEMA.
 
LAZIMA AWE SPIKA COZ NI MTU MAKINI NYIE VIBARAKA WA ra , el NA MAFISADI WENZENU NDO HAMLALI MNAHOFU KWA TUNAO LIFAHAMU BUNGE NI SITA NDO ANAFAA KUWA SPIKA HUYO WA IGUNGA KWAHERI KUWENI WAZALENDO NYIE VIBARAKA TUU.
 
Pasco,
Kupendwa au kutopendwa kwa Sitta hakumsaidii mwananchi. Muhimu aje na majibu ya tuhuma za ufisadi wake. Hatujali kama tuhuma zinatoka kwa wabaya wake au kwa nani. Hata madai yake kuwa kuna fedha na pikipiki zimemwagwa jimboni kwake ili asirejee hatuyapi uzito kwani hata yeye juzi tu kaja na timu kubwa ya wana-Uramabo bungeni na kudai kuwa hiyo ndiyo kamati ya maandalizi kwa 2010.

Nimecheka sana pale aliposema wabaya wake kamera za TBC zikageuziwa kwa Lowasa utadhani ndiye mbaya wake. Mwaka huu watachinjana.
 
LAZIMA AWE SPIKA COZ NI MTU MAKINI NYIE VIBARAKA WA ra , el NA MAFISADI WENZENU NDO HAMLALI MNAHOFU KWA TUNAO LIFAHAMU BUNGE NI SITA NDO ANAFAA KUWA SPIKA HUYO WA IGUNGA KWAHERI KUWENI WAZALENDO NYIE VIBARAKA TUU.

Wrong! Siyo lazima awe spika. Akiondoka yeye mambo yataenda tu kama yalivyo kuwa yanaenda kabla ya yeye kushika hicho kiti. Ni halali yake kugombea lakini si halali yake kupewa. Kusema ni lazima ashike yeye ni kumpa umungu mtu na kukashfu Watanzania kwa kusema nchi yenye watu milioni 40 ni mtu mmoja tu mwenye uwezo na upeo wa kuwa spika wa bunge. Kumbuka kuna watu wali kuwa wanadhani Tanzania bila Nyerere haita weza kuwepo lakini Tanzania inaendelea na itaendelea kuwepo.
 
Mwanafalsafa,
Ni kweli, Tanzania bila Nyerere imeendelea kuwepo, lakini it's quite a different Tanzania!
 
bado mazoea yatatusumbua sana! sikuamini macho yangu pale nilipomuona na kumsikia SS bungeni, akitamba ,aking'aka kuwa lazima atakuwa tena mbunge wa urambo, na lazima atakuwa tena Spika katika bunge lijalo hivi hayo ni maneno ya kuongea mtu mzima kama yeye tena mwenye dhamana kubwa katika chombo cha maamuzi yaani bunge? Sita its your time to quit! we are fed up
Usigeneralize mkuu,naamini watanzania walio-wengi bado tuna imani na Spika, big up SS!!
 
Pasco si ajabu kumuona katekista akifurahia padri wake kuteuliwa kuwa paroko au askofu kwa maana inamhakikishia maisha yake ya kesho hao waliofurahia walionekana kwako tu maana kumbuka bunge linaonekana dunia nzima labda kitu kimoja wabunge wengi walipiga meza nadhani wengi kwa kushangaa spika anavyonyesha ubabe wake kuwa lazima alitakalo liwe
Ila duh....Lowasa alinuna kishenzi.....
 
Nimecheka sana pale aliposema wabaya wake kamera za TBC zikageuziwa kwa Lowasa utadhani ndiye mbaya wake. Mwaka huu watachinjana.

Wote sasa mawazo yao ni jinsi gani watarudi Bungeni tena, hivyo tutasikia na kuona mengi. Na sasa ndio wakatitutaanza kuwaona katika majimbo yetu wakija kutulaghai kwa mara nyingine, miaka yote walikuwa wakiishi Dar, kama sio Dar miji kama mijini (Arusha, Mwanza nk).
 
Mwanafalsafa,
Ni kweli, Tanzania bila Nyerere imeendelea kuwepo, lakini it's quite a different Tanzania!

It is a different Tanzania but Tanzania non the less. Nyerere's Tanzania wasn't without it's faults na kuna mambo mengi tu ya wakati ya utawala wa Nyerere watu hawa kukubaliana nayo. Tatizo la Tanzania siyo kuto kuwepo kwa Nyerere bali kuto kuwepo madarakani watu makini na sababu moja wapo ndiyo hiyo ya kuona bila watu fulani basi mambo haya endi na badala yake tunaendelea kuchagua uozo huo huo.My point is that tuache kutegemea mtu mmoja kuwa "Yesu" wetu na kuokoa taifa zima. Hakuna anaye katazwa kugombea nafasi yoyote but I refuse to believe that only one person can be in one position na bila huyo mtu basi mambo yata yumba.
 
Back
Top Bottom