Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 186
Hii sentensi si sahihi...labda ungesema.....''sisi baadhi'' ungeeleweka zaidi kwa sababu hapo chini kuna baadhi yao mnawatuhumu tayari so definately hao wakoexcluded!Sisi ni wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya......
Isije kuwa mna mpango wa kuchoma moto kujustify madai yenu......!Tunaomba watanzania waelewe kuwa kuanzia sasa ofisi hizo zitaungua moto wakati wowote. .
Mmejificha hivi tena bado mnaogopa? taja majina.....pamoja na ufisadi wao bana....acha umbea vinginevyo!.....imekuwa ikikaliwa na mafisadi wanaojificha katika jina la vinara wa mapambano dhidi ya ufisadi, na kiongozi wao wa Mkuu ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta.
Kupatiwa fedha kivipi? Kama masurufu au kama malipo yake halali au kama advances/loan au kama any other benefits.....elezeni vizuri hapo, kama hamjui taratibu za pesa tulia!Analazimisha kupatiwa fedha kutoka katika ofisi ya bunge anapokuwa katika ziara zake binafsi katika Jimbo lake la Urambo Mashariki. Ushahidi wa haya upo katika vocha za malipo haya. Tunaomba wakaguzi waje wakague watakuta haya
Huu ni umbea kabisa.....wabunge wote niliowasikia ''wakiisulubu serikali''walifanya hivyo kwa sababu za wazi kabisa....kama Richmond, Radar, Twin tower, Buzwagi etc....na ni ukweli kuwa serikali yetu ni hovyo kwa sababu imeshindwa kupambana na ufisadi na kuwainulia kipata na maisha bora wananchi wake!*Spika Sitta amekula akilazimisha kukiukwa kwa kanuni za bunge ili tu kuwapa nafasi wabunge wenzaki walio katika kambi moja kuisulubu serikali ili kuwaaminisha wananchi serikali ni ya hovyo bali yeye na wabunge hao ndiyo wana uchungu wa kweli na taifa hili.
...Haya maneno yenu yamekosa mfupa kabisa......totally umbea!*Spika Sitta hafuati taratibu za uchukuaji fedha za ofisi. Huwa anaamrisha apewe hata fedha za kununua vifaa muhimu vya ofisi akiwa hana fedha na anapokuwa akizihitaji. Fedha zilizopotea kwa njia ni mabilioni, lakini hakuna anayemuhoji.
Rejea hapo juu...hakuna kitu kama hiki....kweli tangia aingie madarakani....HAFUATI kabisa sheria za manunuzi? kuna weza kuwa na kasoro...lakini si kwa kiasi hiki!*Spika Sitta hata siku moja tangu aliposhika wadhfa huo, amekuwa hafuati taratibu za kawaida za sheria ya manunuzi umma katika mambo mengi hapa bungeni. Yota haya ushahidi wake upo ofisi ya uhasibu lakini analindwa na kundi la wabunge wanaodai kuwa wanapoambana na ufisadi kwa* sababua anakula nao.
Hili limeshajadiliwa sana hapa JF .....rejea michango ya members kny thread husika!*Spika Sitta ameshinikiza kukodishiwa nyumba ya gharama kubwa. Dola za Marekani 8,000 kwa mwezi wakati alikuwa amepewa nyumba nzuri tu ya serikali huko Oysterbay. Baada ya kukodishiwa Nyumba hii, alilazimisha pia Ofisi ya Bunge itoe sh milioni 250 kwa ajili ya kununua samani za ndani alizodai kuwa ndizo zinazolingana na hadhi yake ya Spika.
Kama hayo madai ya kununua gari la zaidi TZS 360 ni kweli....hapa kuna concern kubwa sana ya viongozi wetu kuhusu suala la kupambana na umasikini.*Spika Sitta ambaye baada tu ya kuingia katika wadhfa wake alinunuliwa gari jipya aina ya benz. Sasa amelichoka likiwa hata halijamaliza miaka mitatu, anataka kununuliwa jingine na amekwishamuarua Katibu wa Bunge, Thomas Kahililah ambaye ni swahiba wake mkubwa kwa sababu wanakula pamoja kutoa kiasi cha sh milioni 367 kwa ajili ya kununulia gari hilo . Tayari zimekwishalipwa sh milioni 270. wakati haya yakifanywa na Spika, anajua fika kuwa taifa liko katika hali mbaya kifedha na bunge liko katika hali mbaya zaidi kiasi kwamba vikao vyake vinakatishwa.
Hata na hivyo hii imekuwa ndo trend ya viongozi wetu wote wa ngazi ya juu. Ebu niambie, kiongozi gani wa ngazi ya juu TZ unayemfahamu ambaye hajabadili gari lake tangia aingie madarakani 2005?....so nothing new here!
Nyie mlikuwa mnashikilia miguu ya hao wanawake eeeh? au nyie ni washenga? Hata kama ni kweli, je, hao wanawake wanabakwa au wanakubaliana? acha kutuletea Ze utamu hapa bana!*Spika Sitta ana sifa mbaya ya ukware. Tangu ameshika wadhfa huo amekwishatembea na wabunge wanawake wa bunge la Jamhuri ya Muunagni ambao ni wake za watu zaidi 12 na ushahidi wa hili upo kwao wenyewe wabunge. Akikanusha hili tunaomba watumwe maofisa usalama waje wafanye uchunguzi kwa siri, watabaini jinsi anavyofanya ufirauni na wake za watu ambao ni wabunge. Anatembea mpaka na wabunge wa upinzani halafu anajitapa kuwa ni Spika wa wote hivyo lazima awalee. Ni aibu lakini huo ndio ukweli.
Kama vyombo hivyo havijui kazi zao.....vinajidhalilisha na kudhalilishwa kwa kufindishwa what they are supposed to be doing!*Ni mtu anayevidhalilisha vyombo vya ulinzi na usalama kwa sababu amekuwa akisema wazi kuwa hakuna chombo chenye nguvu za kumchunguza yeye na bunge kwa sababu bunge ni dola.
Safi sana kama this is true aisee!Na ukweli sasa umeanza kubainika kwa sababu ni dhahili kuwa serikali inamuogopa Spika na timu ya wabunge wake.
Ushahidi upi waungwana? .....hayo maneno yenu ya umbea ndo mnayaita ushahidi eeh?Ndiyo maana licha ma malalamiko na ushahidi mwingi tuliokwishatoa toa kuhusu ufisadi wake, si TAKUKURU, polisi waka usalama wa taifa waliothubutu hata kumuhoji.
...nyie kama mpo utawala, au mipango au huduma za bunge...acheni kuwaonea wivu wenzenu wa uhasibu...! Kama kuna mhasibu anamhudumia spika wholly & exclusively hii ndo nzuri zaidi....inaonyesha kuna umakini kwa upande wa spika kuhakikisha pesa zinakuwa properly accounted for!*Spika amewagawa wafanyakazi wa Bunge wa Idara ya Uhasibu. Wapo ambao amewateua kuwa watu wake ambao wanashughulika na malipo yake yeye, makamishina wa tume ya huduma ya bunge ambao wanakula naye pamoja, pamoja na wabunge kadhaa ambao uchunguzi wa kina ukifanyika watafahamika.
Kama wamekuzidi cheo na uzoefu kazini ni dhahiri watalipwa zaidi yako mkubwa!*Wahasibu hawa pamoja na Kashililah ndiyo wanaolipwa mishahara mikubwa,
hili halina ushahidi kabisa!wanalipwa posho hata kama hawakufanya kazi za ziada
Hili si kweli....yaani kila spika akienda nje anaenda na delegation yote hiyo ya wahasibu for what?na wanasafiri na Spika kila anapokwenda nchi za nje.