Magreth sitta nae kaanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Magreth sitta nae kaanza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by M-bongo, Dec 29, 2008.

 1. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndg zangu kwa kadri siku zinavyopungua kuelekea uchaguzi mkuu 2010, mama Magreth Sitta juzi 27/12/2008 alifanya vituko katika uchaguzi mkuu wa UWT mkoa wa Tabora katika ukumbi wa Mirambo Sekondari, Mh huyo akiwa anatumia nguvu nyingi kuhakikisha mmoja wa wagombea anashinda nadhani ili aweze kumsaidia katika maandalizi yake ya kjugombea ubunge viti maalumu mkoa wa Tabora, vituko vya kibosile huyo viliambatana na kusimamisha mabasi yaliyokuwa yamebeba wajumbe na kugawa fedha bila woga kati ya 5000 na 10,000 kwa wajumbe na kumwombea kura mtu aliyekuwa amemuandaa Bi Sekasua ambaye hata hivyo alishindwa vibaya, tatizo langu hapa hivi hawa viongozi wanapokaa majukwaani na kuhubiri haki, utawala bora, kupiga vita rushwa huwa wanamaanisha nini hasa? Pole sana mama Sita tunakusubiri kwa hamu sana Tabora 2010, ili tuweze angalau kumalizia vibanda vyetu japo najua matokeo ya UWT mkoa yatakuwa yameweka kitu fulani akilini mwako
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Uongozi sasa unatafutwa kwa njia yoyote, hakuna muda wa kuhudumia wananchi. Uchaguzi ukiisha, wanaangalia uchaguzi unaofuata watashinda tena vipi kwa nafasi zinazofaa. Lakini mwisho wa yote, ni sisi WANANCHI tutakapoamua kusema basi, hawatakuwa na jinsi manake wataiba kura na hazitaibika. Lakni M-Bongo, mbona nawe unasema unasubiri aje 2010 ili muweze angalau kumalizia vibanda vyenu,huoni huko ni kujidhalilisha na kurudia yale yale wafanyayo kununua kura?.
   
 3. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Certain conditions should exist for ufisadi to be exercised, one of them is to be closer to the opportunities. In principle hawa viongozi huwa ni wawakilishi wa wananchi / waliotumwa na wananchi kufanya kazi fulani kwa niaba ya wananchi. Inapokuja mtu ananunua kutumwa ujue iko namna. kama ni kutumwa tu, mtu hawezi kutumia mamilioni yake just for the saske of kutumwa- kufacilitate kazi ya kufisadi.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi bado mnayashangaa mambo haya! Asingefanya hivyo labda ndio ningeshangaa
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Siku zote viongozi hujivika ngozi ya kondoo wanapo omba huruma ya wananchi waingie madarakani wakiingia wanajivua ngozi ya kondoo wanavaa ngozi ya chui au fisi hapo wanakuwa wangine tena na wanasahau tabasamu la huruma walilo kuwa wakilitoa.
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM wote wameoza kuanzia Kikwete hadi kwa balozi wa nyumba kumikumi. Hii nguvu na kibri ya kutoa rushwa waziwazi wanaipata kwa Kikwete mwenyewe na si kwingine kokote kule.
   
 7. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Ohh kwa kutumia mfano wa wote waliopo CCM, si bora tu ungesema wananchi wote wote wameoza..!!!
   
 8. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #8
  Dec 29, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280

  Hiyo principle uliyoweka hapo ina walakini; premise yake is sahihi lakini conclusion yake siyo sahihi kabisa. Kuwepo kwa opportunities siyo condition ya ufisadi kuexist, kwa vile rais Clintoni alikuwa opportunities sawa ama zaidi ya Rais Mkapa lakini Clintoni hakuwa fisadi.

  Ufisadi unaexist kwa sababu jumuia yetu unauruhusu. Kama mama huyu amegawa hela hadharani na wala hakuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya rushwa basi, anaweza kufanya hivyo tena na tena, na jumuia imeruhusu.
   
 9. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  neah,

  kabla sijafika kwa wananchi wote, ninaanzia pale ambapo tatizo limekubuhu na kuelekea kwenye udonda ndugu (kansa?) ambako ni ccm ya Kikwete, Makamba, Rostam Azizi, Manji, Chenge (tume ya maadili ya ccm?) nk
   
 10. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2008
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Hapana. Si kweli kwamba wananchi wote wameoza. Ila kuna wajanja (ndio waliooza) wachache katika jamii wamewalaghai walio wengi. Uongozi Tanzania umejaa ulaghai mwingi. Bahati mbaya: inakosekana namna ya kuwatia disiplini hao walaghai.
   
 11. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #11
  Dec 30, 2008
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani mtoa hoja ue na evidence angalaau hata tu picha. sio mnaandika tu , ama kuchafulia tu watu majina huu ni upuuuzi tu.
   
 12. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #12
  Dec 30, 2008
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuchafuliana majina tu , huna evidence yoyote ndugu M-bongo,lete topic nyingine .wewe hujashitukia watu hawataki kuchangia lolote wanaona huna facts , eti waziri mzima akasimamishe basi na kuanzaa kugawa pesa mhhhh yani unamuona mjinga kiasi gani afanye hivyo katika kipindi hichi cha siasa hapo nchini karibu kila kiongozi yuko muoga na rushwa halafu eti agawe pesa weeeee wee hebu acha utani wako humu jamvini.lete topic mpya
   
 13. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2008
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ndugu mleata hoja,
  Hii ni ishue ya kuchekesha sana kwani pale Tabora kuna vyombo vya habari na waandishi wa habari, kwa kitu kama hiki ni lazima ingeandikwa ama kulipotiwa na moja kati ya vyombo vyetu vya habari. Sasa wewe mwenzetu umeipata wapi issue hii?
   
 14. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Vyombo vya habari hivi hivi vya kila siku au vingine?Hebu nikupe mfano mwepesi.Mamlaka ya Usafiri wa anga ilipotoa taarifa kwamba imeizuia ATC kufanya safari zake,Mattaka aliruka kimanga kuhusu habari hiyo akidai ni ya uongo.Siku mbili tatu baadaye,Mattaka huyohuyo akaeleza kuwa habari hiyo ni kweli,na hakuna mwandishi mmoja aliyemuuliza kwanini aling'aka in the first place.Kuna mambo mengi tu yanayotokea lakini vyombo vyetu vya habari viko makini zaidi katika kuripoti wanacholishwa kuliko kutafiti habari.

  Sintoshangaa iwapo habari hiyo haikuripotiwa na gazeti lolote kwani hata matokeo yenyewe ya uchaguzi hayajapewa coverage kubwa.By the way,hata Dr Slaa alipotangaza list of shame pale mwembeyangtu magazeti yote (except Mwanahalisi) aidha hawakuitoa kabisa habari hiyo au walipoitoa hawakutaja majina.

  Kumbuka pia kwamba JF inajitahidi sana kuziba vacuum inayosababishwa na vyombo vyetu vya habari vinavyoogopa kuweka baadhi ya habari kwa hofu ya kuwa sued....na vinavyokalia habari kwa maslahi yao binafsi....unachokiona kama uzushi hapa JF kinaweza kuwa ndio habari yenyewe kamili kama zilivyoanza ishu mbalimbali eg EPA,Richmond,etc
   
 15. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2008
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Naomba kutofautiana na wewe ndugu yangu.Kumbuka system yetu ya utawala tangu tupate uhuru imekuwa ni top-bottom model.Maelekezo,sera,visheni,nk zinatoka juu kuja chini.
   
 16. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Jana nilikutana na mama mmoja kichaa alikuwa akilalamika na kuzungumza kwa jazba kama vile yuko jukwaani .. nilibahatika kuyasikia badhi ya maneno yake alisema hivi "ccm wezi kweli kweli hawafai kabisa , washenzi ... " maneno mengine ni makubwa zaidi .. kwani ni matusi ya nguoni kwa viongozi wa chama hicho

  Niliwaza sana na kushangaa kwanini ccm inalalamikiwa mpaka na vichaa .. ndugu zangu hapa kunani??????

  Kwa hali hii .. najitoa kote kote .. sina chama mie
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Bado namwomba mungu ili watz wakatae kununuliwa kwa kutumia ela simu etc.
  Bse 5000tsh ya ela ilaruin maisha yako for the comming 5 years.
  Qiet unproportional
   
 18. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yote heri , ujumbe wangu mkuu hapa kwa mama Six ni kuwa ,taratibu watu wameanza kutanbua mtu anayefaa na si vinginevyona nadhani muda si mrefu tutafika kule ambako fedha si kigezo cha kupata viongozi, hebu fikiria Waziri anayeongoza wizara ya serikali anapopambana na watu wadogo kabisa wasio na uwezo wa kutapanya fedha lakini mwisho wa yote waziri huyo na kibarakawake wanaambulia patupu, hii kwa kifupi inatupa matumaini sisi tunaoitwa wa daraja la tatu. ile hoja yangu pale juu ya kumalizia kibanda ni lugha ya kejeli niliyoitumia kufikisha ujumbe sikuwana maanaya kujidhalilisha kama ambavyo mmoja wetu hapo juu amefikiria!
   
 19. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Endeleeni kusubiri vyanzo vya habari vya uhakika, nilichosema ndicho hicho kama una maslahi na mama Six its none of my bussness! kifupi mama Sixalisimamisha basi la wajumbe toka Urambo eneo la makokola relini!akatoa fedha,alisimamisha basi la wajumbe wa NZega eneo la Ipuli akatoa fedha, aliwafuata wajumbe wa Sikonge Nice Hotel akatoa fedha,aliwafuata wajumbe wa Igunga ,Isamilo Inn akamaliza mchezo zaidi ya hapo wahitaji ushahidi gani, hatahivyo swala la kuamini au kutokuamini si langu ni wewe unayesoma habari hizi!cha msingi habari halisi ndio hizi
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wee Urambotabora,
  Je unayokataa una uhakika nayo? Kama kweli watoka Urambo si ungelifanya ka-utafiti kidogo ujue kulikoni? Au wazuka tu kukataa? Sasa jamaa kakuambia hadi sehemu ambayo mama alitoa pesa. Pia huyu M-bongo humfahamu wewe. Unaweza kukuta ni Mwandishi wa habari, kaiandika hii habari ila huko juu Maboss wameipiga chini. Inabaki sasa swala moja tu yaani kuitoa JF ili watu wajue.
  Naomba kama kuna mtu ana mawasiliano na Rage basi amuulizie hili swala maana yule atakuwa na habari nyingi sana za pale Tabora. Nilipomuona Tabora mwezi wa tatu, alikuwa kazungukwa na wapambe wengi sana kila anakopita. Bahati mbaya mie hapa sina mtu wa UHAKIKA anayeweza kunipa hizi habari kutoka Tabora. Ila maadamu haya walifanya akina Lowasa uchaguzi uliopita, sintashangaa leo hii haya mambo ndiyo kwanza yanaingia Tabora.
  Tabora ile wala siwezi kushangaa. Mtu kama Nkumba (Baba ya Mbunge wa Sikonge) alikuwa anasema kabisa "sisi Wanyamwezi tuacheni tu hatufai kuendelea". Kiongozi kama huyu na watu wote waliomzunguka unategemea nini kutoka kwake? Mkoa ule uko palepale utafikiri mkoa uko mwaka 1972 wakati Tabira Jazz inaimba " ..... Muumba, dua tunakuomba pokea........." Naona Muumba aligoma kupokea dua na leo hii tumesimama palepale. Kilichobadilika Tabora ni kituo cha mabasi tu. Sanasana hata zile barabara za lami za mjini zimeshachoka kabisa. Ahhh, badala ya Taxi, nilishangaa naambiwa eti nipandishwe kwenye PIKIPIKI, mie na sanduku langu.
  Kama Wanyamwezi wangu wameanza kuamka it's well and good. Wachukue tu pesa na wampigie kra yule ambaye hakutoa pesa. Hii iwe adhabu kwa wale wote wanaofikiria watanunua kura. Wakichaguliwa hawatafanya kitu na uchaguzi ukifika wanarudi tena na Mahela yao waliyofisadi na kuanza kugawia watu. Mzee wa Visenti yeye anauwa ng'ombe. Kweli sasa naamini kuwa Viongozi wetu na sisi wenyewe ni DUGU MOJA.
   
Loading...