Ni tabia gani umepanga/ulipanga kuiacha kufanya punde tu ukiuanza mwaka mpya? Vipi matokeo yake.

Half american

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
26,091
68,375
Habari wakuu, herini wote kwa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Tukiwa kwenye siku ya mwisho ya mwaka 2023 ni jambo jema sana kumshukuru Mungu na kumuomba atuvushe salama wote tuuone na kuuanza mwaka mpya wa 2024.

Kama ilivyo kawaida kwa miaka mingine iliyopita, baadhi yetu huweka maazimio ya kufanya kitu fulani kwa mara ya mwisho na kuahidi kubadilika kabisa mwaka mpya ukishaanza. Wengi ni ishu ya tabia na mazoea ya kufanya jambo fulani kwa mfano kuvuta sigara, kunywa pombe, kujichukulia sheria mkononi na tabia nyinginezo.

Hii ya kufanya kwa mara ya mwisho inawagharimu wengi sana na kushindwa kuacha tabia husika.

Binafsi mwisho wa mwaka jana niliweka azimio la kuachana na unywaji wa soda kabisa ila nimeshindwa kulifanikisha hilo, kwa kiasi fulani nimepunguza ila sijaweza kuacha jumla. Nipeni mbinu wakuu.

Ni tabia gani unapambana kuiacha kila mwaka na imeshindikana? Tupeane mbinu za kuacha/kuondokana kwa waliofanikiwa kuachana na mazoea/tabia hizo.

Wale wa kushindana na pombe na wanawake slow down ni hatari kwa afya.

Tuumalize mwaka 2023 salama wakuu.

NB: Pambana na yale mambo yaliyokukwamisha mwaka uliopita ufanye mwaka mpya kuwa wa kipekee kwako na wanaokuzunguka.
 

Attachments

  • images (10).jpeg
    images (10).jpeg
    34.8 KB · Views: 5
Back
Top Bottom