Ni siku 21 leo, endelea kulala salama kipenzi chetu Rais John Pombe Joseph Magufuli

Mi natamani siku aliyokufa Magufuli itangazwe kua ni siku ya demokrasia kitaifa.Yaani siku ambayo demokrasia ilizaliwa upya.
 
Too early to judge! Miradi aliyokuwa ameanzisha inaweza kukamilika kwa sababu za kisheria, lakini je kutakuwa na miradi mipya ya viwango hivyo tena?
Kwani alikuwa anatoa hela kutoka kwa mama yake kujenga hyo miradi ?
Huyo alikuwa rais kituko kuliko wote Tuache Ujinga hizo pesa ni kodi zetu hakuna hta shilingi alitoa mfukoni kwa baba yake. Ameikuta Tanzania ina maendeleo mengi kuliko upuuzi alio wekeza wa Chuki na mauaji.
 
Ni wewe tu mwenye chuki, hata jibu lako hili linaonyesha kujawa na chuki tu. Hakuna aliyesema kuwa Magufuli alitumia hela zake au za mama yake kama kwa lugha yako ya kijinga, lakini alitumia hela za walipa kodi kwenye miradi yenye impact kubwa ya mda mrefu kwa nchi, siyo kutumia hela hizo hovyo hovyo kwa mambo ya muda mfupi tu eti kufurahisha watu kama wewe. Miradi ya bwawa la umeme na SGR itanufaisha vizazi na vizazi vikavyo kwa zaidi ya miaka 100 ijayo. Huduma za afya, mashule na umememe vijijini ni miradi ya kujenga nguvu kazi ya ambayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa siku za mbele.

Wewe ulitaka kuwe na warsha za kila leo kusudi watu wapate sitting allowance na safari za kila mara kusudi watu wa;lipwe night allowances wanazoingiza kwenye mzunguko kama ilivyokuwa zamani harafu bila kujua kuwa hiyo ni short term impact tu. Kwa miaka 10 ya Kikwete hizi semina elekezi, warsha, na safari zilikuwa kibao tu, hivyo watu walikuwa wanapata allowances nyingi kusababisha hela kujaa sana mitaani ambapo inflation ilipanda. Ni kwa vile hiyo ilikuwa ni short term impact ndiyo maana mabadiliko ya Magufuli yakawafanya watu kama wewe wachukie.
 
Too early to judge! Miradi aliyokuwa ameanzisha inaweza kukamilika kwa sababu za kisheria, lakini je kutakuwa na miradi mipya ya viwango hivyo tena?
Tuombe Mungu, unaweza shangaa hii miradi ikikamilika wakajibinafsishia watu kwa kisingizio cha serikali kutofanya biashara. Unakumbuka wahindi walivyopewa shirika letu la reli?!
 
Serrikali kuhaimia Dodoma, kununua ndege kujenga Ikulu na misikiti imemsaidia nini "mnyonge"? Unafahamu kweli anachohitaji mnyonge? Nachelea kusema jiwe alikuwa amezungukwa na watu wenye akili fupi ya aina yako!
Hayupo tena baada ya kufanya na kuanzisha kile alichoamini na alichotamani kwa nchi yake

John Pombe Joseph Magufuli aliipenda nchi yake

Makao makuu imehamia Dodoma kama ilivyopangwa
Ikulu imejengwa na watanzania
Ndege zimenunuliwa
Reli zimejengwa
Barabara na madaraja vimejengwa
Shule na mahospitali vimejengwa na kuboreshwa
Makanisa na misikiti vimejengwa na kuboreshwa
Ametengeneza viongozi imara na wazalendo
Kawajengea watanzania walio wengi imani kwa serikali yao na upendo kwa nchi yao
Na mengine mengiiiiiii

Tuseme nini kwa Mungu zaidi ya kushukuru kwa zawadi ya uhai wake John Pombe Joseph Magufuli

Rest well our hero
 
Bora zimeisha mama afanye kazi kwa amani... Maana zilikua kero tupu for nonsense
 
Kuna ndege yoyote iliyotua Chato tangu aondoke?
Ni wewe tu usiyejuwa kuwa kuna ndege zinakwenda huko mara mbili kwa wiki. Business class imeshakribia kujaa imabaki seat moja tu. Unasumbuliwa na chuki dhidi ya jina Chato bila kujua kuwa uwanja ule unaitwa Geita Regional Airport.
1617757155316.png
 
Nikiondoka Mimi hizi ndege zitanunuliwa?

Je, nikiondoka Mimi hizi flyover zitajengwa?

Nikiondoka Mimi,hizi barabara zitajengwa?Mbona hapo kabla mambo haya yalikuwa hayafanyiki?

Leo, hayupo Tena lakini mbona Tanzania ipo na itazid kuwepo?

Dunia tunapita, nothing is permanent even the world itself.

Mungu,kaingilia Kati.
Wote tutakufa Ila heri katangulia huyu aliyebadilisha nchi kuwa ya kabila moja.
 
Too early to judge! Miradi aliyokuwa ameanzisha inaweza kukamilika kwa sababu za kisheria, lakini je kutakuwa na miradi mipya ya viwango hivyo tena?
Itakuwepo Miradi ambayo itatayalishwa kwa weledi na sio kwa kukurupuka kama alivyofanya JIWE na team yake kununua hayo madège bila kufuata utaalam!!
 
Kipenzi chenu na nani!!!?hakuna mtu aliyeharibu umoja na mshikamano wa taifa hili kama huyo Jiwe,apumzike alipojiandalia.mm simkumbuki Cha zuri lolote zaidi utekaji uliokithiri kipindi chake
 
Apumzike Kwa Amani
Tutamkumbuka!!

Unampa Mtoto Wako Yai Na Bado Unamwambia Kula
Unamzaba Kofi Moja Atalibugia Vizuri
Unampa Uji Anatupa Kikombe Ujue Mtoto Ana Kiburi
😆😅😄😃😃😂😂😁😁😀😄😅😆😆😃😂😁
 
Serrikali kuhaimia Dodoma, kununua ndege kujenga Ikulu na misikiti imemsaidia nini "mnyonge"? Unafahamu kweli anachohitaji mnyonge? Nachelea kusema jiwe alikuwa amezungukwa na watu wenye akili fupi ya aina yako!
Shughuli za maendeleo ni kwa Watanzania wote, wanyonge wakiwa kati yao
Ujiongezage basi na wewe

IMG-20210406-WA0092.jpg
 
Back
Top Bottom