Ni nyoka gani mkubwa kuliko wote duniani

Mkuu ni vyema ukarudi na anti-venom za hawa nyoka. Itatusaidia sana sisi watu wa pori. Nasikia sikonge ni balaa kwa koboko!
Tabora region yote ni balaa kwa nyoka. Kuanzia wadogo. Vifutu.swila. sawaka. Cobra mpka huyo black mamba au koboko.
Pia vipo vinyoka flani hivi vidogo vyembamba vya kijani vinaruka pia. Hivo navyo balaa.
Vijijini kule usiku inabidi utembee na chungu cha moto au uji wa moto. Vinginevyo unashangaa mbele yako kuna nyoka kasimama unalingana nae.
 
Kwa hatari huyo koboko msikie tu ila usiombe uingie kwenye 18 zake na wakati huo umkute katoka kwenye mashamba ya bangi kujiria majani.
hahahaa! ni shida sio kwa script hio aisee.. sasa mkuu naomba kujua, hivi joka la kibisa ni lipi hilo? natamani sana nilijue kwa kizungu au picha!

maana wanaume wasio na madhara wanafananishwa sana na huyo kiumbe
 
81d0ffe7c9e9c2cfd696b7e06915d165.jpg
hmm jamani aganza, profile picture yako inaita balaa!
 
Tabora region yote ni balaa kwa nyoka. Kuanzia wadogo. Vifutu.swila. sawaka. Cobra mpka huyo black mamba au koboko.
Pia vipo vinyoka flani hivi vidogo vyembamba vya kijani vinaruka pia. Hivo navyo balaa.
Vijijini kule usiku inabidi utembee na chungu cha moto au uji wa moto. Vinginevyo unashangaa mbele yako kuna nyoka kasimama unalingana nae.
Huko nako ni shida, poleni
 
Anaconda akifutiwa na chatu wa Asia ya Kusini(ukubwa) (hawana sumu, wanaua kwa constriction)
Nyoka mkubwa mwenye sumu ni King Cobra
Nyoka hatari sana kama taipan(ana sumu yenye uwezo wa kuua mpaka watu 400)na Tiger snake wote toka Australia... Australia pekee ina top 10 ya nyoka wenye sumu kali zaidi duniani
Nyoka mwenye sumu kali Afrika ni Black Mamba(koboko) sumu yake inaitwa neurotoxin pamoja na cardiotoxin(inaathiri mfumo wa neva pamoja na moyo
ndo nyoka mwenye kasi zaidi pengine dunia anakwenda km 19 kwa saa(12mph)... Lakini kwa Afrika Boomslang na vine au twig wanaweza kuwa na sumu kali zaidi japo watu wengi wanachukuliwa poa kwa sababu sio wakorofi sana kama Mamba (silent killers (hawa wana sumu inayoitwa haemotoxin ambayo huathiri damu... ina chemical component ambayo huzuia damu kuganda (clotting) na chemical component nyingine husababisha kupasuka kwa mishipa ya damu hii husababisha damu kuvuja ndani na nje kupitia matundu ya mwili )
Puff adder (kifutu) ndo nyoka mwenye kuuwa watu wengi Afrika kuliko nyoka mwingine(sumu yake inaitwa cytotoxin hii huathiri tishu... Inasababisha kuungua au kuoza sehemu ilioumwa
Mozambican spitting Cobra ndo nyoka anaedhuru watu wengi Kusini mwa Afrika
NB:Angali nyoka wote kwa umakini japo asilimia 70 ya nyoka tz hawana sumu ya kudhuru binadamu... Nyoka mdogo ni hatari zaidi (concentration ya sumu kwa nyoka wadogo ni kubwa... Wanatumia kujilinda kutokana na udogo wao)
Nyoka wakubwa umbo lao laweza kuwasaidia kuogofya
Umejibu kitaalamu sana mkuu. Hongera.
 
Kwa muda mrefu nasikia majina tofauti tofauti ya nyoka na sifa zake,hatari zake...lakini je ni yupi ndio kiboko ya yote...yaani funga kazi.anapatikana wapi

Wanasifika sana ni kama vile
Koboko,chatu,cobra,anakonda,futu, n.k

Tujuzane kidogo wakuu


Nyoka mkubwa/mrefu zaidi na asiye na sumu duniani ni Anaconda. Yeye hana sumu ila ana meno madogo madogo na hupatikana baadhi ya nchi za Marekani Kusini. Nyoka mkubwa/mrefu duniani mwenye sumu ni King Cobra, yeye hupatikana India na South East Asia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom