Ni nyoka gani mkubwa kuliko wote duniani

Kwa muda mrefu nasikia majina tofauti tofauti ya nyoka na sifa zake,hatari zake...lakini je ni yupi ndio kiboko ya yote...yaani funga kazi.anapatikana wapi

Wanasifika sana ni kama vile
Koboko,chatu,cobra,anakonda,futu, n.k

Tujuzane kidogo wakuu
Kuna nyoka/ chatu anaeshikilia record ya dunia kwa sasa..

Huyo nyoka anaitwa MEDUSA na anamilikiwa na Kampuni ya Full moon production Inc. Kutoka jimbo la Misouri , nchini marekani.

Nyoka huyo ana urefu wa 7.67M sawa na futi 25 na inchi 2. Vikiwa ni vipimo vilivyochukuliwa mwaka 2011 mwezi october.

Nyoka huyo mwenye umri unaokadiriwa kufikia miaka 10 , alihiyaji watu 15 ili aweze kushikwa kwa unyoofu ili apimwe urefu wake..

a5da48344abf9d9131f71bacdfb0012b.jpg


e0a1eb1b9086df117ea470d128958128.jpg


e77fff018254df4298a7a53383ad92d7.jpg

a3f00709edafcc94851b5c780a457765.jpg
 
Kwa muda mrefu nasikia majina tofauti tofauti ya nyoka na sifa zake,hatari zake...lakini je ni yupi ndio kiboko ya yote...yaani funga kazi.anapatikana wapi

Wanasifika sana ni kama vile
Koboko,chatu,cobra,anakonda,futu, n.k

Tujuzane kidogo wakuu
Anaconda akifutiwa na chatu wa Asia ya Kusini(ukubwa) (hawana sumu, wanaua kwa constriction)
Nyoka mkubwa mwenye sumu ni King Cobra
Nyoka hatari sana kama taipan(ana sumu yenye uwezo wa kuua mpaka watu 400)na Tiger snake wote toka Australia... Australia pekee ina top 10 ya nyoka wenye sumu kali zaidi duniani
Nyoka mwenye sumu kali Afrika ni Black Mamba(koboko) sumu yake inaitwa neurotoxin pamoja na cardiotoxin(inaathiri mfumo wa neva pamoja na moyo
ndo nyoka mwenye kasi zaidi pengine dunia anakwenda km 19 kwa saa(12mph)... Lakini kwa Afrika Boomslang na vine au twig wanaweza kuwa na sumu kali zaidi japo watu wengi wanachukuliwa poa kwa sababu sio wakorofi sana kama Mamba (silent killers (hawa wana sumu inayoitwa haemotoxin ambayo huathiri damu... ina chemical component ambayo huzuia damu kuganda (clotting) na chemical component nyingine husababisha kupasuka kwa mishipa ya damu hii husababisha damu kuvuja ndani na nje kupitia matundu ya mwili )
Puff adder (kifutu) ndo nyoka mwenye kuuwa watu wengi Afrika kuliko nyoka mwingine(sumu yake inaitwa cytotoxin hii huathiri tishu... Inasababisha kuungua au kuoza sehemu ilioumwa
Mozambican spitting Cobra ndo nyoka anaedhuru watu wengi Kusini mwa Afrika
NB:Angali nyoka wote kwa umakini japo asilimia 70 ya nyoka tz hawana sumu ya kudhuru binadamu... Nyoka mdogo ni hatari zaidi (concentration ya sumu kwa nyoka wadogo ni kubwa... Wanatumia kujilinda kutokana na udogo wao)
Nyoka wakubwa umbo lao laweza kuwasaidia kuogofya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom