Ni nani yuko nyuma ya Polepole?

Ni nani yuko nyuma ya Polepole?

1. Alikuwa katibu mwenezi awamu ya 5 2- Yakatokea yaliyotokea akaishi maisha ya awamu ya 5 akiwa awamu ya 6 3. wakamuondosha njiani yeye mwenyewe akijua anajua anaondoshwa /Awe na watu nyuma yake au mbele yake wote ni walewale wasitufanye watanzania makhanithi wa fikra Sababu anazotoa slowslow zinaweza zikawa za kweli lakini jee ni ukweli amewahi kuuishi ndani ya ccm, especially k/mwenezi ? Jee uvunjifu wa haki umeanza lini, na cku zote alikuwa wapi ?

"Mijadala ndio huwa chemchem ya maendeleo ya Taifa lolote. Tutakuwa na Taifa mfu iwapo tutakosa mijadala ihusuyo mambo mbalimbali yanayolihusu Taifa letu"
Mhe DR. BASHIRU ALI KAKURWA, KM- CCM Juni 19, 2019



Maswali Mawili Chechefu :

1. Je, ukiwa Kiongozi na ukawa hukubaliani na yanayofanyika au kuna mambo yanayokuudhi, unatakiwa ufanyeje ?

1.1 Kwenye Muhimili wa Bunge, wabunge, mara kadhaa, hulazimika kupiga kura. Kuna wapigao kura za Ndio na wengine Hapana. Kwavile uamuzi ni "Wengi wape", Azimio la Bunge hutokana na walioshinda. Hata kama mbunge alipiga kura ya hapana, kwavile hilo sasa limekuwa ni Azimio la Bunge, inabidi akubaliane nalo. Vinginevyo, ateme bungo.

1.2 Kwenye Muhimili wa Serikali, Waziri akitoa mawazo yake ambayo yanapingana na Mawaziri wenzie kwenye Baraza la Mawaziri, inabidi akubaliane na uamuzi "Ministerial responsibility" vinginevyo ateme bungo.

1.3 Kwenye Muhimili wa Mahakama, Majaji Watatu (Panel) wakimaliza kusikiliza kesi, wawili wakiwa upande mmoja na mwingine yuko peke yake, hukumu huwa ni mawazo ya wale wawili. Yule mmoja aweza kuandika maoni yake (dissenting opinion) lakini hukumu ya Mahakama itakayosimama huwa ni ile ya wengi.

1.4 Novemba 11, 1979, Mhe Edwin Mtei, aliyekuwa Waziri wa Fedha, alitema bungo baada ya kutofautiana misimamo na Rais Julius Nyerere. Mhe Mtei alitaka nchi ikubaliane na masharti ya IMF na kushusha thamani ya shilingi yetu, kitu ambacho Rais Nyerere hakukitaka hata kidogo.

Mhe Mtei aliwapeleka Msasani maafisa 3 wa IMF waliotoka USA kumpiga shule Mwalimu. Mwalimu akaona wanaongea pumba tu! Akabishana nao sana. Akachukia mno. Bila kuaga, akatoka nje na kwenda nyuma ya nyumba "beach". Mhe Mtei alidhani Mwalimu kaenda "Washroom". Ilipopita saa nzima, ikabidi aulize, akaambiwa Mwalimu yuko "beach". Hakuamini! Akaenda "beach". Akamkuta Mwalimu na mlinzi wake wanapunga upepo ufukweni kwa raha zao! Mhe Mtei alijitahidi kumbembeleza Mwalimu japo aende kuwaaga wale wageni lakini Mwalimu alikataa katakata. Mhe Mtei, kwa shingo upande, akasepa na kwenda kuwapitia wageni na kuondoka nao.

Zahir Ali Zorro & Kimulimuli Jazz Band wakatunga wimbo kuyazodoa Mataifa Makubwa yaliyotutaka tuishushe shilingi yetu. Tukajiona wajanja.

Hata hivyo, miaka michache tu baadaye, Tanzania ilitii Sheria bila shuruti" kwa kushusha thamani ya shilingi yetu.

1.5. Rafiki yangu mmoja kiongozi aliwahi kunisimulia jinsi baadhi ya "Bongolanderz" walivyokataa kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mawaziri mwaka 2015. Aliwataja 2 ; mmoja alisema kuwa asingeiweza kasi ya Mhe Magufuli kwani aliuona utendaji wake usio mfanowe akiwa Waziri wa Ujenzi. Mwingine akasema kuwa Mhe Magufuli sio mtu wa kufuata Katiba & Sheria hivyo wasingewezana.

Prof. Benno Ndulu, alipokuwa Gavana wa Benki Kuu, alitupa ubuyu mwaka 2017 tukiwa 3 nchini Fiji tulikokuwa tukihudhuria mkutano. Siku hiyo ya Ijumaa usiku iliyokuwa ya sherehe "beach" ambapo washiriki wote tulivaa nguo nyeupe, Prof. Ndulu "alijiachia" sana kwa michapo lukuki kuhusu Rais Magufuli. Alitunyetishia kuwa Rais Magufuli alitaka kumfanya awe Waziri wa Fedha lakini akakataa. Ubuyu mwingine aliotupa ni pale aliposimulia : "Rais Magufuli hajui kama binadamu anahitaji usingizi. Yeye hata saa 8,9, 10 usiku atakupigia simu akupige maswali. Sijui alikuwa analala saa ngapi!. Pia ni kama Rais Magufuli alikuwa ananivizia. Maana kila baada ya dinner na nikienda kuoga tu, nikimaliza nakuta amenipigia simu na swali la kwanza "kwanini wewe ni mzito wa kupokea simu?".

1.6. Mhe Samia Suluhu Hassan alipokuwa Makamu wa Rais, nae siku moja alitupa ubuyu. Hii ilikuwa Novemba 16, 2020.

Siku hiyo, Rais Magufuli alikuwa akimwapisha PM Majaliwa Kassim Majaliwa, Prof. Kabudi (Waziri wa Mambo ya Nje) na Dr. Isdory Mpango (Waziri wa Fedha). Hao ndio walikuwa Mawaziri wa kwanza kuteuliwa na kuapishwa 2020. Mhe VP Samia, alipoongea kwenye sherehe hizo za kuapishwa viongozi hao, akatuacha wote midomo wazi luningani! Alieleza, kwa hisia kali, kuwa ile miaka miwili ya mwanzo chini ya utawala wa Rais Magufuli ilikuwa migumu sana kwake. Alisema hakuwa amezoea aina ile ya utawala ya "Nginjanginja"! Akaiona ofisi chungu na akawa akijifungia ofisini akilia! Je, alipaswa kujiuzulu? Je, kila mtu anayekwazika akijiuzulu itakuwaje?

2. Je, Kiongozi akitaka kujiuzulu, Rais hawezi kukataa ?

2.1 Mhe Joseph Sinde Warioba alieleza kuwa mwaka 1984 akiwa kwenye Baraza la Mawaziri alipingana na Rais na Mawaziri ambao walitaka kupitisha Sheria ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa na vipengele vingi tata mf vikakatazavyo dhamana, kuwa na Mahakama maalum ya kesi za uhujumu uchumi na kesi kusikilizwa faragha. Mhe Warioba alikuwa Waziri wa Sheria & AG. Alipoona yuko pekee na hawamuelewi, akatangaza kujiuzulu.

PM Sokoine akamwita na kumwambia "Kitu kidogo tu kama hiki wewe unaamua kujiuzulu?".

Keshoye, PM Sokoine akampeleka Mhe Warioba Msasani kwa Rais Nyerere. Wakaondoa baadhi ya vipengele lakini vingine mf dhamana vikabaki. Sheria ikapita Aprili 1983.

Muda mfupi baadaye, Wazee wa CCM mkoa wa Mwanza wakasafiri hadi Msasani na kumwambia hawakubaliani na kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CCM Kanda ya Ziwa. Rais Nyerere akamuagiza PM Sokoine amuachie. PM Sokoine akamwandikia Mhe Warioba amuachie lakini Mhe Warioba akadinda! Ikabidi PM Sokoine amwite Mhe Warioba na akamwambia "We ni mtu wa aina gani unagoma kutekeleza agizo la Rais?". Mhe Warioba akasema Rais Nyerere alisema Sheria yoyote isivunjwe hata ikiwa mbaya kiasi gani, ila yaweza kurekebishwa. PM Sokoine alimwelewa ila akasema anaogopa kwenda Msasani kumwambia Mwalimu kuwa Agizo lake halitekelezeki hivyo wakakubaliana na Mhe Warioba Sheria irekebishwe.

Juni 1983, Sheria hiyo ikarekebishwa!

Wewe unaonaje ?. WAMANG'ATI husema:

The ball is in your court
 
Ukisoma barua yake kaongea ukweli na hali iliyopo .

Ila kosa lake kubwa ni kukubali kuwa sehemu hicho anachokilalamikia.

Kwakuwa mfumo wa kiuchaguzi na yeye amehusika kuuharibu .

Anastahili kupewa lawama na pongezi pia kwa wakati mmoja.


Pia kwa Age yake , Exposure n.k anaweza akawa ameona umuhimu wa kumtukuna Mamba kwakuwa ameshavuka mto.


Means wapo walio nyuma yake na ikiwa hawapo lazima amepata green pastures n.k


Faida za kukaa Cuba hazikuwa kwa polepole Ila zilikuwa kwa Serikali , kumzima kwa kummezesha tonge la ugali mdomoni.


Tutaona .
 
Polepole tatizo lake hana adabu.
Polepole dhamira yake imemsuta. Mtu binadamu wa kweli, mtu mwema, mkweli unayeheshimu utu na uhai wa wanadamu wenzako huwezi kukubali kuwa kwenye mfumo unaoteka na kuua binadamu wenzako.

Nina hakika wengi mpaka kufika October watakuwa wamejitenga na waovu na Chama Cha Mashetani. Asili ya mwanadamu siyo uovu, japo anaweza kuwepo kwenye uovu. Huko watabakia tu wale wa uzao wa ibilisi wanaoishi na roho ya ibilisi.
 
Hili swali lingekuwa halina maana kama yasingetokea leo ya kujiuzulu nafasi nyeti ya ubalozi nchini Cuba na uwakilishi wa mataifa jirani na Cuba

Tatizo sio kujiudhulu bali ni sababu za kujiuzulu.. Kawa muwazi sana sana na kanyoosha maelezo bila kutumia lugha laini ya kidiplomasia

Kuna wanaojaribu kupooza fukuto kwa kusema ile barua ya kujiuzulu ni bandia, huku wengine wakidai hajaandika yeye bali imeandikwa na "wanaharakati" kina huyu Lucas yeye kaenda mbali zaidi kwa kusema eti ataijibu barua ya Polepole.. Sasa sijui kwa mamlaka yapi na kwa vigezo gani.. Kwakuwa ile sio barua ya posa kwamba inahitaji majibu

Mfahamu Pole pole yule wa bunge la katiba... Si sehemu ya mfumo.. Alivutwa kwa nguvu na mwendazake.. Na mambo yalipobadilika, akionekana ni team JPM akawa ni kati ya waliotolewa kwenye mfumo wa sasa! But a short time to live!

Safari ya kutolewa chamani mpaka Malawi halafu baadae Cuba ina simulizi yake ambayo hitimisho lake ni hili tukio la leo

Sababu alizotoa zimenyooka sana. Kaongea lugha ya CHADEMA kwa kwa tune nyingine.. Nafasi aliyokuwa nayo kipindi cha mwendazake ni wazi alikutana na wakubwa wenye mitazamo inayofanana na kwa vyovyote walitengeneza bond!

Kitendo cha kujiuzulu akiwa kazini na barua yake kusambaa mitandaoni.. Kina tafsiri yake pia.. Na ukizingatiq kafanya hivyo siku ya weekend tena mchana kuelekea adhuhuri

Cuba ni nchi rafiki na Tanganyika. Kuna hatari na nusu kufanya alichofanya akiwa ndani ya Cuba hata Kama ni weekend
Kwa maneno ya moja kwa moja ni kwamba kaasi.. Na hayuko ofisini kwake Cuba

Kwa barua ile na kwa hali ilivyo ni wazi hawezi kamwe kurejea nchini kwa sasa.. Je yuko wapi? Kwa hadhi gani? Ya ukimbizi?

Ni wazi kuna jambo ana hakika nalo, na lina backup ya vivuli visivyojulikana kwasasa.. Huku ndio nyumbani kwake hivyo hawezi kukaa ukimbizini ama mafichoni kwa muda mrefu

Nice wazi hii ni project ya kikundi cha watu ndani ya mfumo.. Lakini je mfumo haukuwa na hizi taarifa? Au kitakachotokea?

Hata kama haitatamkwa hadharani.. Lakini kayatimua maji vibaya sana! Chekeche litaanza maramoja kutafuta walio nyuma yake na mipango yao...

Kwasasa zinapimwa athari za uamuzi wake kishapo itakuwa ni zamu ya kujibu mapigo...!
Banda ya barua yake ya kujiuzulu je atakaa kimya.. Ama ndio itakuwa mwanzo wa kutapika nyongo kwa uhuru?
Yajayo ni Mengi
Good night TanganyikaView attachment 3404860
Binafsi naona katumia haki yake ya kikatiba ya kueleza mawazo yake, kama ilivyo katika Ibara ya 18. Labda akirejea nchini watu mbalimbali watamuuliza na atafafanua zaidi kilichomsukuma afanye huo uamuzi, na kuweka katika lugha aliyoitumia. Kwa sasa, kwa vile hatujui chochote tungempa 'the benefit of the doubt'. Ndivyo ninavyoona mimi.
 
Mm nahisi mtu mwenye hakili huwa hakurupuki.anyway nilianza kumjua yule bro mwaka 2018.kipindi nahitimu elimu yangu ya form four...ni mtu niliyekuwa natamani siku moja nimjue zaidi...anyway endeleeni kupiga porojo.lakini vipi wakuu hivi ile barabara ya kuelekea bunju imekamilika?....au tusubiri mwakani
Msumi kuna ntu amekimbia na fuko la pesa za barabara
 
Binafsi naona katumia haki yake ya kikatika ya kueleza mawazo yake, kama ilivyo katika Ibara ya 18. Labda akirejea nchini watu mbalimbali watamuuliza na atafafanua zaidi kilichomsukuma afanye huo uamuzi, na kuweka katika lugha aliyoitumia. Kwa sasa, kwa vile hatujui chochote tungempa 'the benefit of the doubt'. Ndivyo ninavyoona mimi.
Kwa aliyoyasema na kwa hali ilivyo unadhani atarudi nchini kweli?
 
Back
Top Bottom