Ni nani aliyewahi kuuelewa mziki wa Michael Jackson?

Wewe umezaliwa 2009 unataka kumuelewa msanii ambaye alikuwa anatumbuiza enzi baba yako na mama yako wako vidudu. Huna adabu kabisa wewe mtoto. Tena ukome kama ulivyokoma ziwa la mama yako.

Mwaka 1988 pale Drive in ( kwasasa ni ubalozi wa Marekani) kulikuwa na bonge la screen. Nyimbo ya Michael Jackson, Thriller ilikuwa ndio inawekwa mida ya saa sita usiku. Aiseeee acha wewe mbwa. Yaani sikulala nyumbani siku hiyo nilikojoa kupitia dirishani aisee acha kabisa.

Wewe dogo naomba kwanza ukatubu hii dhambi umetutukania historia yetu kwamba msanii ambaye alikuwa anatusisimua na kututoa machozi leo hii unasema hakuna alilofanya. Wewe mtoto shika adabu yako aiseeee.
 
Mtu anatumia masaa 8 kupigia mazoezi step moja tu unajua diet aliyokua anafanya kumaintain mwili wake wa kimuziki? kafatilie documentary ya ile video ya thriller uone uandaaji wake watu wanapiga kazi usiku kwenye baridi kali alafu we unasema anatajirika bila jasho seriously.!
NImetamani kuandika mambo mengi lkn nilipoona joined 2022 nikaona nitaua mende kwa nyundo huku mimi nikipoteza nguvu nyingi zaidi.
 
Za jioni ndugu zangu, kwema?

Michael Jackson enzi za uhai wake alikuwa msanii maarufu na tajiri kuliko msanii yeyote hapa duniani.

Lakini pamoja na hizo sifa mbili kubwa nilizozitaja, kwangu mimi naona kuwa jamaa alibebwa na nyota tu kama ilivyo kwa Diamond, ila kiuimbaji au utungaji jamaa hakuwa anatunga au kuimba nyimbo zozote za maana.

Em fikiria Michael Jackson alikuwa na uwezo gani wa kutunga nyimbo nzuri na za maana kushinda wasanii kama Lionel Richie, Steven Wonder, Phil Collins, au mademu kama vile Whitney Houston, Celine Dion, Shania Twain nk.

Labda aliwashinda kwenye kucheza kama vile kusimamia kucha, kuteleza sakafuni, mabreka nk. Lakini kwenye tungo iwe za mapenzi, kijamii nk Michael alikuwa mweupe tu kama ilivyo kwa Diamond kuonekana anajua na kupata umaarufu wa ndani na nje zaidi ya wakongwe wa mziki kama vile kina Nature, Afande Sele, Kiba, Barnaba na wakongwe wengine mbali mbali.

Sijajua hili linatokana na nyota kweli au kuna namna tu media zinaamua kukubeba kwa lengo fulani.

Kwa kweli mpaka sasa sijauelewa mziki au wimbo uliomfanya Michael Jackson apendwe na kuitwa mfalme. Mwenye uelewa zaidi wa nyimbo zake aje atuambie.

Michael Jackson atabaki kuwa extraordinary human being.. Na ni ngumu sana kupata Tena binadamu kama yeye kwa kizazi chetu

Ingawa kama binadamu alikuwa na mapungufu yake n.k lakini kimziki jamaa ni kama Einstein au Tesla kwenye umeme
 
Acha kusikiliza singeli, ukiacha rudi tena kasikilize wimbo wowote wa hayati Michael Jackson, baadhi ya nyimbo hizo ni Human Nature, Liberian Girl, Slave To Rythm, Black or White, Bad, Stranger in Moscow, Billie Jean, Don't stop till you get enough, thriller, You are not alone, Will you be there e.t.c

Jitahidi unavyoanzisha thread hata kama haulipii utumie akili kuwasilisha unachotaka na sio kuja bila mpangilio. Yangu ni hayo
Umesahau ngoma mbili

1. Heal the word
2. Earth Song.

Sauti za humu ndani ni balaa tupu.
 
Umefanya niingie YouTube nisikilize liberian girl kuclear huu upupu wako uliouandika apo juu
 
Dah we nguruwe huu uzi wako umenichefua sana. Maana umekosa adabu kupita maelezo na umetukosea adabu wakubwa.

Ngoja nikuandikie nyimbo hizi kama una bundle nenda YouTube kazitafute utazame video na uhakikishe una music system nzuri au spika nzuri za masikioni.

Tafuta hizi video:

1. Thriller
2. Earth Song
3. Bad (long version)
4. Smooth Criminal
5. Beat it (lomg version)
6. Black or White ( tafuta long version ya huu wimbo pale yule chui mweusi/Black Panther anatoka nakushuka kule chini utamu wa ile video ndio upo kule)
7.You rock my world (Long version)
8. Ghosts (long version)
9. Blood on the dance floor

Tafuta video za live concert za Michael Jackson uone Matusi ya uwezo wake hakuna mtu anamfikia hadi leo hii kwa rekodi shenzi wewe.

Nenda katazame hizo kazi halafu ndio uje kuandika utumbo wako hapa.

Umenikera sana dogo, ungekuwa mbele yangu kwanza ningekuchapa kofi tatu za haraka halafu ningekufukuza.
 
We jamaa umeniharibia siku kwa kumponda mfalme wa pop. MJ toka akiwa mtoto alikuwa anatisha. Sikiliza I'll be there alioimba na kaka zake (Jacksons5) akiwa mtoto kabisa. Huo wimbo ulikuja kurudiwa (remix) na Mariah Carey.

Endelea kusikiliza Singeli. Haya mambo yanayohusisha kiingereza achana nayo.
Amenikera sana huyu dogo hadi nimeshindwa kula. Hawa watoto wa miaka 2000 wanadharau sana hawa.
 
Ili upate toba ya kweli, sikiliza huku unasoma lyrics za hizi nyimbo;

Earth song- Uharibifu wa Mazingira, Madhara ya vita, Ubaguzi wa rangi/utumwa.

Gone too soon- Waliotengwa kwa kuugua UKIMWI.

Black or white - Anakemea ubaguzi wa rangi

Another Part of Me - Umoja

Man in the Mirror - Kujitambua (Self-awareness)

The Lost Children- Anaongelea watoto wa mitaani

Alafu ule hizi ngoma:-

This Girl is Mine
Jam
Leave me alone,
Off the Wall,
Pretty Young Thing(PYT)
Rock With You
Speechless
You Rock My World
Who Is It
Butterfly

NB: Ukimaliza uje uombe radhi hapa
 
Plus:

Dirty Diana... Hasahasa album nzima "Thriller" na "Bad".

Hizo album mauzo yake hayajawahi kufikiwa hadi leo.. hasa Thriller ngoma zote kwenye album ni nyundo... enzi hizo unasikiliza side A unaenda side B unarudi side A mwendo kugeuza kanda... Masaa mawili ya hits.
 
Alafu kama watu walikuhadithia kuhusu yeye na kwanini yuko kama alivyokuwa sikiliza huu wimbo wake 'Childhood'

Na malizia kwa kuangalia documentary yakuitwa 'The Killing of Michael Jackson'
 
Za jioni ndugu zangu, kwema?

Michael Jackson enzi za uhai wake alikuwa msanii maarufu na tajiri kuliko msanii yeyote hapa duniani.

Lakini pamoja na hizo sifa mbili kubwa nilizozitaja, kwangu mimi naona kuwa jamaa alibebwa na nyota tu kama ilivyo kwa Diamond, ila kiuimbaji au utungaji jamaa hakuwa anatunga au kuimba nyimbo zozote za maana.

Em fikiria Michael Jackson alikuwa na uwezo gani wa kutunga nyimbo nzuri na za maana kushinda wasanii kama Lionel Richie, Steven Wonder, Phil Collins, au mademu kama vile Whitney Houston, Celine Dion, Shania Twain nk.

Labda aliwashinda kwenye kucheza kama vile kusimamia kucha, kuteleza sakafuni, mabreka nk. Lakini kwenye tungo iwe za mapenzi, kijamii nk Michael alikuwa mweupe tu kama ilivyo kwa Diamond kuonekana anajua na kupata umaarufu wa ndani na nje zaidi ya wakongwe wa mziki kama vile kina Nature, Afande Sele, Kiba, Barnaba na wakongwe wengine mbali mbali.

Sijajua hili linatokana na nyota kweli au kuna namna tu media zinaamua kukubeba kwa lengo fulani.

Kwa kweli mpaka sasa sijauelewa mziki au wimbo uliomfanya Michael Jackson apendwe na kuitwa mfalme. Mwenye uelewa zaidi wa nyimbo zake aje atuambie.

Una miaka mingapi?
 
Plus:

Dirty Diana... Hasahasa album nzima "Thriller" na "Bad".

Hizo album mauzo yake hayajawahi kufikiwa hadi leo.. hasa Thriller ngoma zote kwenye album ni nyundo... enzi hizo unasikiliza side A unaenda side B unarudi side A mwendo kugeuza kanda... Masaa mawili ya hits.
Mzee, acha kabisa! Sasa kijana wetu huyu..
 
Back
Top Bottom