Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 44,384
- 105,226
Hii haiwezi kuwa habari mpya sana kwa wengi wetu humu.
Makala nyingi zimeandika habari hiyo kuwa ni kweli. Lakini mimi naijumuisha katika moja ya conspiracy theories. Ni kawaida sana kwa mtu mashuhuri kuwekewa habari nyingi za uongo kwa media ili ku catch attention ya watu.
Kumbuka 27 Januari 1984 Michael Jackson akiwa jukwaani akifanya show kwa ajili ya tangazo la Pepsi, aki-perfom nyimbo yake maarufu ya Billie Jean
Kulikuwa kuna zile pipe za kutolea moto kwa ajili ya manjonjo ya show (pyro effects) zilikuwa jirani na usawa wa kichwa chake wakati anacheza.
Moto ulidaka nywele zake, nayeye aliendelea kucheza akiwa hatambui kuwa nywele zimeshika moto. Washirika aliokuwa nao kwenye kikosi cha kuchukua hiyo filamu ya hilo tangazo ndio waliomvuta kumtoa kwenye moto. Lakini wakati huo tayari madhara ya moto yalikwisha fanyika.
Aliugulia majeraha ya moto kwa kiwango kilichohatarisha kupoteza hadi uhai wake. Kufuatia ajali hiyo, Pepsi ilimlipa mamilioni ya dola za kimarekani kama fidia, ambapo kwenye hizo pesa alijitolea kujenga clinic kwa ajili ya kusaidia kutibu wahanga wa moto.
Katika kujenga hiyo clinic Michael Jackson alinunua vifaa vya kisasa kwa ajili ya kurudisha hali ya ngozi iliyoharibiwa na majeraha ya moto. Moja ya kifaa hicho ilikuwa ni hyperbaric oxygen chamber.
Tazama picha hapa chini.
Hicho ni kifaa ambacho kinamuwezesha muhanga wa moto kuweza kupokea hewa nzuri ya oxygen iliyochujwa pamoja na kumuongeza mtiririko mzuri wa damu. Hutumika kurejesha ngozi ambayo imehathiriwa na majeraha ya moto.
Sasa Michael Jackson alipoinunua kwa ajili ya Clinic yake, wakati wa uzinduzi aliamua kujaribu mwenyewe kisha kuruhusu watu wapige picha akiwa ndani ya hiyo chemba.
Baada ya hapo ndio wale haters wa "Wape picha stori watatunga wao," wakaanza kuzusha propaganda kuwa analala humo ili kufanya aishi miaka mingi. Mara Michael Jackson anaogopa uzee hivyo analala kwenye chemba ili kuepuka asizeeke.
Wakati hiyo chemba yenyewe hutakiwi kulala zaidi ya masaa mawili kwasababu inaweza kusababisha upoteze maisha.
********************†***************
Nawasalimu kwa jina la Hip Hop.