Ndoa za wasanii wa Mziki wa Injili

MLIMAWANYOKA

JF-Expert Member
Oct 25, 2019
488
1,637
𝑡𝒂. 𝑱𝒐𝒉𝒏-π‘©π’‚π’‘π’•π’Šπ’”π’• 𝑴. π‘΅π’ˆπ’‚π’•π’–π’π’ˆπ’‚
____________________________
Nimekuwa mfuatiliaji sana wa maneno yaliyokuwa yakisemwa na baadhi ya Waimbaji wa Kike wa Nyimbo za Injili hasa baada yaWanawake hao kuachana na Waume zao, kutoka kwenye Ndoa zao baada ya Ndoa zao kuvunjika.

Nilifuatilia zilipovunjika Ndoa za akina Sarah Mvungi, Neema Mushi/Mwaipopo, Bahati Bukuku, Flora Mbasha, Janeth Mrema, Upendo Kilahiro/Wisdom, Angel Bernard, Martha Mwaipaja na sasa Christina Shusho.

Kitu nilichokigundua kwa Wasanii hawa ni kwamba, Wanawake wote hao wameonesha kwamba kulikuwa na shida kwa upande wa Waume zao. Lakini kikubwa kuliko vyote ni kwamba Ndoa za Wasanii hawa zilivunjika baada ya kuwa Maarufu.

Kibaya zaidi ni kwamba hakuna Msanii hata mmoja aliyesema labda kilichosababisha Ndoa kuvunjika ni shetani kuwa na nguvu kubwa katika kuivunja Ndoa yao kiasi cha kuizidi Nguvu za Roho wa Mungu aliyekuwa amepotea ndani yao. Wote wamewasemea 'vibaya' Waume zao.

Sina lengo la kukipinga wanachokisema kuwa sio kweli wala sikusudii kuwahukumu kuwa walikosea maana hilo sio jukumu langu na sina haki ya kumhukumu binadamu mwenzangu, Mungu pekee ndiye Hakimu Mwenye Haki maana Hukumu yake ni ya Haki na huwa haikatwi rufaa.

Lakini kama watu tulioumbwa na Mwenyezi Mungu tukapewa Zawadi ya Akili, Utashi na Uhuru, basi tunao Uhuru wa kuzifanya Akili zetu zifanye kazi zake sawa sawa. Tunapaswa kuhoji na kujihoji, kudadisi na kujidadisi juu mambo kadhaa kutoka kwenye kauli zao na matukio yaliyoambatana na kuvunjika kwa Ndoa zao.

Kwani, kukaa kimya tu baada ya Ndoa hizo kuvunjika sio busara? Au kwa vile ni Wanawake Maarufu basi wakishapewa tu kipaza sauti ni lazima wayaongelee Madhaifu yaliyokuwa kwenye Ndoa zao? Ni kweli kwamba Wanawake hao akina Shusho walikuwa Malaika hivi kwenye Ndoa hizo?

Akina Shusho wanataka kutuaminisha kwamba Ndoa zao zilikuwa kati ya Shetani (Waume zao) na Malaika (Wao)? Kama huo ndio ukweli, waliwezaje kudumu kwenye hizo Ndoa kwa muda huo wote waliodumu hadi kuzaa watoto waliowazaa? Kama waliweza kuyavumilia yote waliyoyavumilia, walishindwa vipi kuendelea kuyavumilia?

Kwani kwa muda wote wa Uhai wa Ndoa zao, walikuwa hawajui kama Ndoa inahitaji kuisha Maisha katika Shida na Raha, taabu na Magonjwa mpaka kifo kitakapowatenganisha? Kwani kitendo cha wao kuwa Waimbaji wa Nyimbo za Injili kinakuwa ni Kinga ya kuzifanya Ndoa zao zisikumbwe na Changamoto kama zilivyo Ndoa za watu wengine?

Nafasi zao kama Watumishi wa Mungu zilikuwa wapi katika Kuziombea Ndoa zao zisizidiwe na Nguvu ya Shetani Mwovu? Au wao wana karama tu za kutunga Nyimbo zinazowabariki Wapendwa ila hawakuwa na uwezo wa kujibidisha katika Maombi ya kuzinusuru Ndoa zao?

Ndoa ni taasisi ambayo Mungu Mwenyewe anaianzisha ndani ya mioyo ya Upendo ya watu ili waishi katika shida na raha. Shetani hapendi kuiona Ndoa ikistawi kwa sababu Ndoa ni jambo la heri. Anaweza akamtumia Mwanamke kuivunja Ndoa yake Mwenyewe kama ambavyo yule Nyoka alivyopitia kwa Eva kuivunja Amri ya Mungu.

Shetani haiogopi Ndoa ya Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Askofu, Mchungaji, Shemasi, Katekista, Mwinjilisti, Shehe, Imamu wala Muazini. Ndoa yoyote ikilegalega katika Maombi, inaweza ikakumbwa na Wimbi la Misukosuko ya Hila za Shetani na ikavunjika.

Mwanzoni Christina Shusha amenukuliwa akisema kuwa aliachana na Mume wake ili aweze kulitimiza kusudio la Mungu lililoko ndani yake. Maana yake Mungu alimtoa Shusho kwenye Ndoa ili akalitimize kusudio lake. Kwa tafsiri nyepesi ni kwamba Ndoa ilikuwa ni pingamizi la yeye kumtumikia Mungu.

Na hivi karibuni amesema kuwa aliolewa akiwa na umri mdogo sana (miaka 19), hivo alilazimishwa kuingia kwenye Ndoa akiwa Mdogo tena bila ridhaa yake. Hivi, inawezekana kweli Mtu wa miaka 19 ashindwe kufanya maamuzi kwa miaka yote aliyoishi kwenye Ndoa hadi kuzaa watoto halafu sasa ndio agundue alilazimishwa na kutumikoshwa Ndoani? Au kuna kilichojificha nyuma ya pazia?

Wasanii hawa na Jamii kwa ujumla ikae ikijua kuwa siku Wanaume zao hao nao watakapoamua kuvunja ukimya na kutoka hadharani kuyasema 'madudu' ya Wasanii hao, nina uhakika tutazificha nyuso zetu uvunguni. Tumuombe sana Mungu aendelee kuwapa busara za unyamavu Waume zao wasiseme lolote ili kuwalindia heshima zao Wanawake hao.

Niwaombe sana Enyi Wanawake; mkiachana na Waume zenu, punguzeni maneno, msiwe kama akina Shusho, mtakuja kuaibika kwa kuwafanya wenye akili waanze kufikiri kuwa huenda kwa kipindi chote mlichokuwa mmedumu kwenye Ndoa zenu sio kwamba mlikuwa tu mnayavumilia mateso bali mlikuwa mmezoea kunywa uji wa nyumbani ila mlipoanza 'kulamba asali ya nyuki wa kubwa wa Mzinga mliokuwa hamuujui', mmeishia kuuona uji wa kazi gani.

Wasanii wote hao wamepata umaarufu wao wakiwa kwenye Ndoa. Baada ya kuwa Maarufu, wanaidharau Ndoa pamoja na Waume zao na kutoa sababu za kashfa. Wanawake, jifunzeni kwa unyenyekevu kabisa kuwa, "Kitanda ulicholalia usikinyee uondokapo". Na mkiachana na Waume zenu, msiwe na maneno mengi kama akina Shusho.

Aleluyaaaaaaaaaaa.........!!!
 
Mwandishi umenena vema,,,,umeandika kwa logic,na ikaeleweka........,inavyoonekana hapa hatuna watu wa rohoni kweli bali tuna wasanii wahuni waliokua na kiu ya kutoka na kujulikana,,,,kupitia migongo ya watu fulani.....Asilimia kubwa ya wanawake wanaamini kua wanapambana kufanikiwa ili wajikomboe toka kwa mwanaume,huku mwanaume yeye anapambana akiifikiria familia yake.....
 
Back
Top Bottom