Ni muda muafaka sasa kwa shule za serikali kuwa "english medium"kwa sababu...

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
681
825
1. Tayari sasa ni mwaka wa saba tangu serikali ilipo anza kuanzisha shule za majaribio ili kuona ufanisi wa tija juu ya mabadiliko hayo ambapo hadi sasa mafanikio yameonekana kuwa makubwa zaidi kwa shule zilizo katika majaribio ikilinganishwa na shule za kawaida (zinazo tumia kiswahili)

2. Hadi sasa ni ukweli usiopingika kuwa Wananchi zaidi ya 90% hata wale waliobatizwa jina la "mnyonge" wanapenda wanapenda na kutamani Sana watoto wao wasome shule za "English medium" hasa wakiamini kuwa ushindani wa soko la ajira ni mdogo Sana kwa wale wasioelewa lugha ya kiingereza.

Lakini pia hao "wanyonge" wanajiuliza maswali kwamba kwa nini hao viongozi wao wa serikali hawawapeleki watoto wao katika shule za lugha ya kiswahili?

3. Pamoja na juhudi za serikali kutaka kiswahili kishamiri Afrika na duniani hakuna madhara yoyote ya kufifisha jitihada hizo kwa kurasimisha lugha ya kiingereza kutumika kufundishia/kujifunzia.

4. Ni kweli kuwa changamoto kubwa ni uzoefu kwa walimu katika lugha yenyewe. Hata hivyo siyo kweli kwamba walimu hawajui kuongea kiingereza la hasha bali tu ni kasoro ndogo za mazoea ambazo zinaweza kupatiwa ufumbuzi kwa kuwapeleka walimu katika kozi fupi fupi za miezi sita kwa awamu katika kila shule.

5. Hadi sasa ni wazi kuwa tayari tumekwisha ruhusu matabaka katika elimu huku wengi wa waitwao "wanyonge' wakiamini kuwa elimu wapatayo watoto wao si lolote si chochote kutokana na hoja zao ambazo kiasi fulani zaweza kuwa na uhalisia.
 
Back
Top Bottom