Naibu Katibu Mkuu wa ASP Youth League ya Mapinduzi ya 1964 atema nyongo

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
Mzee Baraka - CCM IMESALITI, NIA NA SABABU ZA MAPINDUZI MATUKUFU YA 1964


View: https://m.youtube.com/watch?v=habiWXzPxFM
Mzee Baraka Shamte mwenye umri wa miaka 94 aliye na afya njema, katika mahojiano exclusive na Jambo TV akikumbuka mapinduzi matukufu na uongozi wa Mzee Abeid Amani Karume wa kuanzia 1964 hadi 1972 Mzee Karume alipouawa na wapinga mapinduzi ya makabwela, Mzee Baraka analia kwa uchungu na kutema nyongo kuhusu waliochukua madaraka ndani ya CCM sasa hawajali wanyonge kama serikali ya Mzee Abeid Karume

Mzee Baraka Shamte akiangalia nyuma mbali, anajiuliza vipi hakuna Kumbukizi ya Mzee Abeid Karume kama ilivyo Kumbukizi ya Mwl. Julius Nyerere kupitia Taasisi ya Mwalimu Nyerere kila mwaka kuendeshwa kwa makongamano yenye kuufanyia tathmini utawala wa Nyerere lakini kwa Zanzibar wamemtupa kiongozi wa mapinduzi ya 1964...

Mwanamapinduzi Mzee Baraka anasema kukosekana kwa kumbukizi ya Abeid Karume ni mwendelezo wa wapinga mapinduzi kwani wamefikia hadi kuuvunja uwanja wa Amani Karume ambao ni moja ya kumbukumbu nyingi wazee wanamapinduzi walio hai walikuwa wanavienzi kwa wivu mkubwa mzuri sasa kiwanja kimebomolewa, wakati wangeweza kujenga kiwanja cha kisasa chengine huku wakibakiza kumbukumbu mojawapo kubwa ya muasisi wa Zanzibar huru.

Mzee Baraka anakazia kuwa badala ya kuwakaribisha wanamapinduzi waliokuwepo wakati wa mapinduzi ya 1964 kuzungumzia hali ya siasa Zanzibar kabla na baada ya mapinduzi, sasa wanaalika watoto wadogo kusoma historia kutokana na mabuku yaliyochakachuliwa badala ya kualika watu kama yeye walioishi katika kipindi halisi.

Mzee Baraka Shamte anaendelea kuelezea hujuma kibao dhidi ya wananchi wa Zanzibar zinazofanywa na viongozi walafi wa CCM wanaoshirikiana na wapinga mapinduzi ndani ya Tanzania na nje ....

Mzee Baraka anaongeza tuliungoa utawala wa kisultani uliokuwa unarithishana uongozi kifalme na sasa utawala wa CCM nao umetumbukia ktk kurithishana uongozi kindugu pia kifamilia na mbaya hawataki mtu achukue fomu kugombea nafasi hadi mtu amalize miaka 10 ikulu wakati katiba inasema kila miaka 5 uchaguzi ufanyike ...

Mzee Baraka azidi kuanika hulka za kibwanyenye zinazozidi kukita ndani ya chama kongwe dola cha CCM ....
 
Akiguswa tu analia. Mzee huyu anatakiwa akeshe misikitini kufanya toba maana muda wake mwingi anitumia kutukana watu.
 
Huyo mzee laana ya baba yake ndiyo inayomuandama aliiunga mkono ASP kuipindua serikali iliyoshinda uchaguzi 1963 na baba yake akawa waziri mkuu sasa anaweweseka,akatubu.
 
Mzee Baraka anasema CCM imetekwa wa mkoloni weusi wasomi, kitu alichokitolea tahadhari Mzee Abeid Amani Karume mara baada ya mapinduzi kuwa wasaliti watakuwa watu weusi wasomi ambao wataongoza kujitajirisha kwa wizi wa mali ya umma, kuandika historia potofu ya ukweli wa kilichotokea mara baada ya mapinduzi, kuwagawa watu katika makundi huyu mpemba yule mzazibari na wale wabara ....
 
Mzee Baraka Shamte akipokea nishani kutoka kwa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi mh. Dr. Shein

1704479081342.png
 

Dhahama alizokumbana nazo Mzee Baraka Muhammed Shamte ktk kukikosoa chama chake, ingawa cha hicho kongwe dola kinadai kupitia kiapo cha mwanzo kuwa mwana CCM lazima awe tayari " Kusema Kweli Daima"


Toka maktaba :​

CCM Zanzibar Yakosa Uvumilivu wa Kisiasa, Yamfukuza Baraka Shamte Kumnusuru Rais Mwinyi​

CCM Zanzibar Yamfukuza Baraka Shamte Kumnusuru Rais Mwinyi
ni hatua ya kujibu mapigo na kumkomoa kada wake wa muda mrefu, Baraka Shamte, ambaye amependekeza kuwa rais Mwinyi aliyekuwa katibu mwenezi wa ccm wilaya ya mjini Baraka Shamte ameikosoa serikali ya rais Mwinyi na uongozi wake akisema Shamte, mwanachama wa CCM Zanzibar akizungumza na vyombo vya habari. CCM yamfukuza rasmi uwanachama Baraka Shamte , aliyekuwa mwanachama na kada wa CCM Zanzibar amepigwa na watu wasiojulikana siku chache baada ya mwanasiasa mkongwe zanzibar Baraka Muhamed Shamte kuukosoa utawala uliopo madarakani.
Source: intaneti
 
Kama uwanja uliitwa amani kwa heshima ya rais wa kwanza wa zanzibar huru, sheikh abeid amani karume kulikuwa na sababu gani kubadilisha jina na kuuita jina jipya la new amani complex hata kama waliukarabati? Wangejenga uwanja mwingine na kuuita complex
 
Back
Top Bottom