Ni nani makomredi walioshiriki Mapinduzi ya Zanzibar 1964

Hamid Rubawa

Member
May 23, 2018
72
202
Ni nani makomredi walioshiriki Mapinduzi ya Zanzibar 1964

Picha: Baraza la Kwanza la Mapinduzi Zanzibar

WIKI iliyopita mwandishi Salma Said alichangia katika mazungumzo ya humu mtandaoni yaliyoanzishwa na makala ya @ahmedrajab katika Gazeti la Dunia yakimzungumzia Badawi Qullatein.

Salma aliandika kuwa yeye aliwahi kukutana na kuzungumza na Badawi. Akawataja pia makomredi wakuu wengine wa Umma Party aliowahi kukutana nao, kwa mfano Ali Sultan Issa, Salim Rashid na Khamis Abdulla Ameir, ambaye Mei Mosi atatimia miaka 93.

Salma alituhimiza tukisome kitabu cha Khamis alichokizindua mwaka jana kiitwacho “Maisha yangu: Miaka minane ndani ya Baraza la Mapinduzi. Khaini au Mhanga wa Mapinduzi?”

Kitabu hicho kinauzwa ALIFU Bookshop, Mkunazini, Unguja. Bei ni TSh65,000. Pia kinapatikana kwenye ofisi ya Zanzibar Institute for Research and Public Policy (ZIRRP) nyuma ya ukumbi wa sinema wa Majestic, Vuga, Unguja.
Walio nje ya Unguja wanaweza kupiga simu +255 714 197 810 na kuagiza.

Gazeti la Dunia lina furaha kuchapisha hapa chini Dibaji ya kitabu hicho iliyoandikwa na @ahmedrajab.

Na Ahmed Rajab

NI nani makomredi walioshiriki, kwa kiwango fulani, katika Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964? Walikuwa mazimwi walioifisidi nchi yao au walikuwa wanamapinduzi wa kweli waliokuwa na dhamira njema za kuleta usawa na maendeleo nchini mwao? Khamis Abdalla Ameir, mmoja wa waasisi wa Umma Party, chama cha makomredi, anayajibu maswali hayo kwa umahiri mkubwa katika kurasa za kitabu hichi.

Komredi Khamis, aliyezaliwa tarehe Mosi, Mei, 1930, anayajibu maswali hayo anapoyasimulia maisha yake na kujiuliza swali kuu linalomsugua roho anapoutathmini mchango wake katika mapinduzi ya Zanzibar: ameibuka kuwa nani katika kadhia nzima ya mapinduzi hayo? Ni khaini au ni mhanga wa hayo mapinduzi? Anaiacha jawabu yake ikining’inia, kama utandabui, akiwa na hakika kwamba kwa jinsi jawabu hiyo ilivyoiva msomaji hatokuwa na mushkili wowote wa kuung’amua ukweli wa mambo ulivyokuwa.

Kwa hakika, Khamis hatoi jawabu ya mkato. Anaanza mbali kwa kuutaja uzawa wake, wazazi wake, nasaba zake (makabila mawili ya Kiarabu, al Hinai na Mazrui, na moja la Kiafrika la Kinyasa), maisha yake ya utotoni na ya ubarobaro uliojaa utundu na ujasiri. Halafu anayachupia maisha yake ya ujanani akiwa ughaibuni, kwanza Arabuni na hatimaye Uingereza, alikoishi kwa miaka minane na ambako ndiko alikoanza kuzinusa siasa za mrengo wa kushoto na, hatimaye, akazikumbatia kwa mahaba ya dhati.

Alipokuwa akiishi London, Mzanzibari huyo alisaidia harakati za wapigania uhuru wa Kenya. Ilisadifu kwamba nyumba aliyokuwa akiishi ikikabiliana na ile ya Mbiyu Koinange, mmoja wa wafuasi wakuu wa Jomo Kenyatta. Khamis pamoja na Wazanzibari wengine walikuwa hawatoki nyumbani kwa Koinange. Wakimsaidia katika kampeni zake za kutetea uhuru wa Kenya kwa kuuza barabarani magazeti aliyokuwa akiyaandika Koinange kupinga ukoloni wa Uingereza.

Mchango wa Wazanzibari hao kuwasaidia wazalendo wa Kenya ulikuwa mfano wa mafungamano ya umajumui wa Afrika na ushirikiano wa Wazanzibari na Wakenya dhidi ya ukoloni. Harakati zao za ukombozi hazikuijali mipaka ya nchi zao. Adui yao alikuwa mmoja: Ukoloni wa Uingereza. Na waliazimia kuupiga vita kwa pamoja.

Wakati huo, hukohuko London, Khamis alikuwa amekwishakutana na Abdulrahman Babu na Ali Sultan Issa, Wazanzibari wenzake waliokuwa na mwamko mkubwa wa kisiasa na waliokuwa wamekwishajipatia umaarufu katika duru za kisiasa za wakombozi wa Afrika. Babu alikuwa mfuasi wa falsafa ya kisiasa iitwayo kwa Kiingereza “anarchism”. Falsafa hiyo, na vuguvugu lake, haiamini kuwepo kwa serikali. Inauona mfumo wa kuwa na serikali kuwa ni mfumo usiohitajika kwa kuwa una madhara makubwa kwa jamii. Badala yake wafuasi wa falsafa hiyo wanaamini kuwa bora jamii iwe inaendeshwa kwa ushirika, tena wa khiyari, bila ya wananchi kushurutishwa. Wanataka pawepo utawala huria usiotegemea serikali wala sheria.

Siku hizo Babu alikuwa bado hajawa muumini wa siasa za Kimarx. Lakini Ali Sultan tayari alikuwa mkomunisti na haikuchukuwa muda Khamis naye alijiunga na Chama cha Kikomunisti cha Uingereza (Communist Party of Great Britain, CPGB). Tukisoma simulizi za Khamis kukhusu maisha yao walipokuwa London, haishangazi kuona kwamba baadaye watatu hao waliibuka kuwa vinara wa siasa za Kimarx visiwani Zanzibar.

Khamis alijikita zaidi katika vyama vya wafanyakazi, akijitolea kupigania haki zao. Kinyume na walivyofanya Babu na Ali Sultan, Khamis, aliporudi Zanzibar, alikataa katukatu kuwa mwanachama wa chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP, maarufu Hizbu) au kile cha ASP.

Lakini Babu na wenzake walipokiacha mkono chama cha Hizbu, Khamis aliungana nao kukiasisi cha Umma Party. Hicho ndicho chama cha Zanzibar alichoingia kwa khiyari yake. Baada ya mapinduzi, hakuwa na hila ila kuwa mwanachama wa chama pekee kilichokuwa halali, yaani Afro-Shirazi Party (ASP).

Khamis alikuwa miongoni mwa wajumbe wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi la mwanzo la Zanzibar chini ya uwenyekiti wa Sheikh Abeid Amani Karume. Alikuwa mjumbe wa Baraza hilo kwa miaka minane mpaka alipokamatwa baada ya kuuliwa Karume na akafungwa akihusishwa na mauaji hayo. Kurasa zinazozungumzia kadhia hii, na aliyoyashuhudia jela, zinasisimua.

Sifa kubwa ya kitabu hiki ni kwamba si kikavu, si chapwa hata kidogo. Kimekolea viungo vingi vilivyonyuyizwa hapa na pale, kwa mtiririko kama wa kazi za kubuni, kama riwaya au filamu. Siku moja alishtuka kumuona mwanawe aliyekuwa na umri mdogo katumbukizwa jela kwa utundu wake.

Kwenye kurasa hizi Khamis pia anatutajia mafunzo ya ki-intelijentsia aliyofunzwa Czechoslovakia zama za ukoloni na namna alivyozihaulisha hadi Zanzibar bastola alizokuwa ameachiwa katika Ubalozi wa Czechoslovakia, mjini Mogadishu, Somalia. Ametueleza kukhusu ndoa zake mbili: ya kwanza aliyoifunga London na chuo chake cha pili alichokipiga Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Chuo chake cha kwanza kilikuwa na mwanamke wa Kihabeshi wa familia ya kimwinyi iliyokuwa karibu sana na Mfalme Haile Selassie. Walijaaliwa binti mmoja, ambaye alipokuwa mchanga Khamis alimlea peke yake, kwa muda wa miezi sita, huku akifanya kazi jijini London. Mida hiyo mama mtoto alikuwa akimhudumia Mfalme Haile Selassie akiwa muuguzi wake rasmi. Kwa bahati mbaya ndoa hiyo haikuweza kuhimili mivutano ya kitabaka baina ya Komredi Khamis na familia ya mkewe. Mivutano hiyo pia ilimfanya ashindwe kuanza maisha mapya Ethiopia. Ndipo aliporudi Zanzibar na kujimwaga katika medani za kisiasa.

Mwaka 2013 Komredi Khamis na mimi tulialikwa Addis Ababa, Ethiopia, na Muungano wa Afrika (African Union), tukiwa wajumbe wa Vuguvugu la Umajumui wa Afrika (Pan-African Movement) kushiriki katika kongamano juu ya mustakbali wa Afrika. Katika ziara yetu nilizidi kuushuhudia utu wa Khamis kwani alifanya jitihada ya kuwatafuta na kwenda kuonana na jamaa zake mkewe wa kwanza, miaka zaidi ya 50 tangu waachane.

Katika kurasa za kitabu hiki, Khamis anaeleza mengi kukhusu siasa za Zanzibar na khasa matukio ya baada ya Mapinduzi. Anatufungulia pazia tuone jinsi Rais Abeid Karume alivyokuwa akiiendesha mikutano ya Baraza la Mapinduzi na maisha ya “waheshimiwa wanamapinduzi”. Kwa mfano, wajumbe wa Baraza la Mapinduzi walikuwa wakilipwa mishahara miwili, mmoja wa kuwa katika Baraza na mwingine wa ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na huko kwenye Bunge la Muungano waliamrishwa wawe mabubu, wasithubutu kuchangia chochote katika mijadala.

Khamis ametudokolea jinsi Sheikh Karume alivyowaamrisha waheshimiwa hao wachukuwe mikopo ya serikali kujijengea nyumba. Mjumbe pekee wa Baraza la Mapinduzi aliyekataa mkopo huo, licha ya kubembelezwa akubali, alikuwa Abdulrahman Babu. Yeye akitaka fedha hizo za mikopo zitumiwe kuwajengea nyumba walio masikini.

Chama cha makomredi cha Umma Party kilikuwa chama pekee katika ukanda mzima wa Afrika ya Mashariki kilichokuwa kikifuata falsafa iliyotungwa na Karl Marx, Friedrich Engels pamoja na Vladimir Lenin na iliyoendelezwa na Mwenyekiti Mao Zedong wa China. Falsafa hiyo imejikita juu ya nadharia za kimaendeleo, zinazoichambua jamii kitabaka.

Khamis Abdalla Ameir, aliyebobea katika falsafa hiyo, ni mtu muhimu sana katika taarikhi ya harakati za ukombozi wa Zanzibar na khasa za vuguvugu la wafanyakazi wa visiwa hivyo. Utaipunja na kuionea historia lau ukijaribu kuandika kukhusu harakati hizo bila ya kumtaja na kueleza namna alivyojitolea kuwapigania wafanyakazi na kusaidia katika jitihada za kuutokomeza ukoloni. Tushukuru kwamba amewapunguzia kazi wanahistoria kwa kuandika kitabu hiki chenye kuelezea maisha yake na fikra zake.

Amezianika fikra hizo kadamnasi, parwanja, tena kwa ufasaha, bila ya kuzigubika na chochote. Kwa kufanya hivyo amewawezesha wasomaji wake wazisome kwa uwazi kabisa na waone jinsi zinavyowachambua, na kuwachamba, baadhi ya viongozi wakuu wa siasa za Zanzibar. Hakujaribu kukistiri chama chochote cha siasa. Hata chama chake cha Umma Party na baadhi ya viongozi wake hawakusalimika.

Wanapostahili kuumbuliwa, Komredi Khamis amewaumbua akionesha udhaifu na taksiri zao. Amesimulia jinsi makomredi walivyofanya makosa ya kimkakati na hatimaye wakajikuta wamepigwa chenga na wahafidhina wa ASP wakisaidiwa na ghiliba na ujanja wa Rais Julius Nyerere, wasiweze kuyadhibiti na kuyaongoza mapinduzi.

Kwa wasiomjuwa, jambo la mwanzo wanaloliona kwa Khamis ni upole na uungwana wake. Si mtu wa maneno mengi, wa kupayukapayuka na kujitwaza kwa hili au lile. Si mtu wa kutakabari au kujigamba kwa lolote. Kwa tumjuwaye, tumeyaona kwake zaidi ya hayo: haiba yake ya kisiasa, ukunjufu wa moyo wake na insafu yake.

Hadi leo nakumbuka jamala aliyotuonesha mimi na mwenzangu, Abdulla Salim Mzee, tarehe Mosi, Mei, 1964 katika hafla iliyofanywa Ubalozi wa China, Zanzibar. Abdulla na mimi na vijana wengine waliokuwa wafuasi wa Umma Party pamoja na wa Afro-Shirazi Party tulikabidhiwa wajumbe kadhaa kutoka serikali za Kiafrika na nchi za kikomunisti za Ulaya ya Mashariki tuwe nao na kuwaonesha Zanzibar ilivyokuwa. Naitoshe kusema kwamba usiku ule Khamis alitufunza mengi mimi na Abdulla.

Kuna jambo jengine linalowafanya watu wahamasishwe na Khamis: mvuto wa hoja zake. Namna anavyozitoa hoja hizo anapochambua mambo ndiko kulikowavutia wengi wa makomredi wenzake kufika hadi ya kumuelezea kuwa ni “mwananadharia wa Umma Party”. Sio kwamba ametunga nadharia mpya ya Umarx lakini Khamis Abdalla Ameir huzitumia nadharia hizohizo zilizopo anapokuwa anachambua hali halisi zilivyo Zanzibar, Tanzania na kwenye mataifa mengine katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Na hufanya hivyo bila ya kukwambia kwamba nyenzo anazozitumia katika chambuzi zake ni za Kimarx. Huyaangalia mazingira ya nchi fulani na halafu hutumia misingi ya nadharia ya Kimarx kuyachambua mazingira hayo na kuifanya hiyo nadharia iwe inayasibu hayo mazingira. Ndio maana chambuzi na tathmini zake za kisiasa huwa yakinifu.

Hiyo ni mojawapo ya sababu zinazomfanya awe anaitwa “Mhishimiwa” ndani ya duru za makomredi. Hatumwiti hivyo kwa matani. Tunamshimu khasa. Mimi binafsi nimenufaika laisa kiasi na tathmini zake. Kuna kipindi ambapo kila nirudipo Zanzibar nilikuwa na kawaida ya kwanza kufululiza kwetu kumwamkua mama yangu, na halafu nikivikata vichochoro vya Mjini, Unguja, nikielekea mtaa wa Kibokoni ambako Khamis akiishi na mama yake.

Nikifanya hivyo ili nizichote hizo tathmini yakinifu kutoka kwa Mhishimiwa. Tumshukuru kwa wema aliotufanyia sisi na vizazi vijavyo vya wananchi wa Zanzibar, na wa Afrika ya Mashariki kwa jumla, kwa kutuhifadhia baadhi ya tathmini hizo katika simulizi zilizo kitabuni humu.

Ahmed Rajab
London
18 Septemba, 2021

Screenshot_20230502-203459_Chrome.jpg
 
View attachment 2607665
Mbona Mastermind Oscar Kambona usalama mwingereza humtaji? Bila yeye hamna liwalo
 
MWAMBA JOHN OKELLO BABA LAO.
 
MWAMBA JOHN OKELLO BABA LAO.

Revolutionary Okello.jpg

Huyu wa kati ndiye Field Marshal John Okelo (the forgotten hero} aliyeyaongoza mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyomtimua Sultani Jamshid bin Abdullah!

Si hivyo tu Field Marshal John Okelo ndiye aliongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar kama Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Pamoja na hayo Field Marshal John OKelo kama mwenyekiti wa Baraza ndiye alimteua Abed Karume kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya watu wa Zanzibar.

Huu ukweli sijui kwa nini unapotoshwa makusudi.
 
Ni nani makomredi walioshiriki Mapinduzi ya Zanzibar 1964

Picha: Baraza la Kwanza la Mapinduzi Zanzibar

Ahmed Rajab
London
18 Septemba, 2021

View attachment 2607665
Watafutwe wapewe maua yao!.
Wana bodi, japo tuko kwenye harakati za kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge, kuna swali linanitatiza kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ambapo majibu yake sahihi, pia yanaweza kuwa ni kiashiria tosha cha mshindi wa urais wa Zanzibar, iwapo uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Swali hili lahusu ukweli haswa kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964, baada ya kuibuka kwa kitabu kingine kiitwacho "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"
View attachment 2077603
kilichoandikwa na Mwanazouni wa Zanzibar, Dr. Harith Ghassany, kama kilivyofanyiwa mapitio na mwandishi Mohamed Said kwenye gazeti la Al-Nuur la leo.

Ghasanny anasema kumbe Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalitekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde (Wakata Mkonge) ambao waliongozwa na Mzee Mohamed Omar Mkwawa (Tindo) chini ya Amiri Jeshi wa jeshi la mamluki hao Victor Mkello (RIP). (kumbe amiri jeshi hakuwa Mganda John Okello pekee, bali pia Mkello yumo?!.

Mamluki hao walitumia zana zao za kukatia mkonge, zile sime za makali kuwili, walizisunda kwenye nguo zao za ndani na kusafirishwa kwa mitumbiwi usiku usiku kupitia Kipumbwi. Jee wale mashuhuda wa Mapinduzi yale Matukufu ya Zanzibar, wanayakubali haya?.

Pia mwandishi anamalizia kwa kusema hata mauaji ya Karume, hayakutekelezwa na wapinga Mapinduzi, bali ni miongoni mwa hao hao wanamapinduzi, baada ya kupishana kauli fulani fulani za uendeshaji wa Zanzibar baada ya Mapinduzi.

Nimesoma kitabu cha John Okello kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar,
View attachment 2077618
yeye anasema yake, vitabu kadhaa vya waandishi wazungu wanasema yao, historia tukuka ya Mapinduzi Matukufuya ya Zanzibar nayo nayo inasema kivyake, hivi hakuna any straight line yoyote kuhusu Mapinduzi hayo, ya Zanzibar?.
Jee yalipangwa na nani? Yalitekelezwaje?.
Nini haswa kilichotokea usiku ule wa Januari 11?.
Nani alifanya nini wapi?
Na mwisho tuzungumzie wafaidika wa Mapinduzi hayo Matukufu ya Zanzibar na bila kuwasahau wahanga wa Mapinduzi hayo ambao kwako yatakuwa sio Matukufu, ni kina nani haswa?, na kama kuleta amani na utangamano wa Zanzibar kuhusu Mapinduzi hayo kutahitajika kuundwa kwa Tume ya Ukweli na Upatanisho, "Truth and Reconciliation Commission" ili waliohasimiana kutokana na Mapinduzi hayo, wapatanishwe kwa maslahi mapana ya Zanzibar?.

Majibu ya maswali haya yatasaidia kujua mustakabali wa matokea ya uchaguzi wa Zanzibar kudhirihisha kuwa Wazanzibari ni wamoja, hakuna kundi la walishiriki Mapinduzi ndio wenye uhalali zaidi kuitawala Zanzibar kuliko wasioshiriki, after all kumbe Mapinduzi yenyewe, yametekelezwa na askari mamluki wa Kimakonde, toka mashamba ya mkonge Tanga!.

Pasco
Rejea za Mwandishi huyu kuhusu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
  1. Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1
  2. Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
  3. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Paskali
 
Mmoja wapo wa viongozi wa Umma party alikuwa Ali Hassan Mwinyi, sijui kwa nini hili halisemwi
 
Back
Top Bottom