Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,921
- 30,266
Gazeti la Jamhuri la Jumanne 21 - 27 November, 2023 lina makala: ''Zanzibar Ndani ya Muungano Haishikiki - (14).
Baada ya kusoma niliingia Maktaba na nikakuta hayo yafuatayo niliyoandika miaka mingi nyuma (2016):
''Katika mambo yaliyosaidia sana kuiweka vyema historia ya Zanzibar ni vitabu vilivyoandikwa na Wazanzibari wenyewe ambao walipigania u huru wa Zanzibar.
Historia iliyokuwa ikipewa nafasi ni historia ya mapinduzi peke yake ilhali Wazanzibari walipigania uhuru wao kutoka kwa Muingereza wakaupata na baada ya hapo kiasi cha mwezi mmoja tu yakatokea mapinduzi yaliyosababisha umwagaji mkubwa wa damu na madhila mengi.
Baada ya Ali Muhsin Barwani kuandika kumbukumbu zake: ''Conflicts and Harmony in Zanzibar,'' ambayo kwa hakika ni historia ya kudai uhuru wa Zanzibar na historia ya vyama vilivyopigania uhuru wa Zanzibar - Zanzibar Nationalist Party (ZNP) au Hizbu, Afro Shirazi Party (ASP) ya Abeid Aman Karume na Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) ya Mohamed Shamte picha mpya ikajitokeza. Lakini ilikuwa kalamu ya Aman Thani katika kitabu chake: ''Ukweli ni Huu,''
ndiyo iliyokuja na historia ya kutisha.
Hata hivyo kitabu cha Dr. Harith Ghassany: ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' utafiti huu ulishinda tafiti zote za kigeni na ndicho kilichokuja kuweka historia ya Zanzibar katika mawanda ya dunia.
Yale yaliyokuwa yamefichwa sasa yakawa yapo uwanjani peupe yanasomwa, na wengi wa wasomaji hao ni vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi.
Matokeo ya mwamko huu mpya ndiyo haya tunayoshuhudia hivi sasa.
Bahati mbaya badala ya kusikitishwa na yaliyotokea na kujaribu kuleta umoja pamezuka watu wanakejeli waliouawa kwa dulma katika mapinduzi yale.
Waliouawa wameacha watoto na wajukuu wapo kwa sasa, wamesimama kupinga kila aliyekuwa anaonyesha kufurahishwa na historia ile iliyowapotezea wapendwa wao.''
Sasa tupitie pamoja hayo niliyosoma kutoka kalamu ya Mihangwa:
Kitabu cha Sheikh Ali Muhsin Barwani kwa Kiingereza na Kiswahili (1997)
Kitabu cha Aman Thani
Dr. Ghassany ndiye mwandishi wa kwanza kuieleza dunia kuwa katika ardhi ya Tanganyika, kijiji cha Kipumbwi kulikuwa na kambi iliyoweka mamluki kwa ajili ya kuvushwa kwenda Zanzibar kusaidia kuiangusha serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.
Dr. Ghassany kaja Tanga na mimi ndiye mwenyeji wake nikampeleka nyumbani kwa Mohamed Omari Mkwawa akazungumzenae kuhusu hii kambi ya Kipumbwi.
Nilimfikisha nami nikaondoka nikawaacha wawe na faragha wazungumze yale yaliyotokea katika mapinduzi ya Zanzibar.
Niliporudi kumchukua Dr. Ghassany nilimkuta amekalia mgongo wake.
Kitu gani kilimnyong'onyeza?
Endela kusoma:
''Hivi ndiyo nilivyomkuta Dr. Ghassany alivyokuwa amekaa nyumbani kwa Mohamed Omari Mkwawa Kisosora Tanga akisikiliza yale yaliyotendeka Zanzibar baada ya Wamakonde kuingia kushiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Hakuwa na nguvu ya kukaa sawasawa.
Alikuwa amechoka sana.
Watengeneza filamu wa Hollywood ni mafundi wa kutengeneza kitu kinaitwa, "set."
Ingekuwa wanapiga movie ile hali ya nyumba ya Mzee Mkwawa au Tindo kama Mzee Karume alivyopenda kumwita ilijitosheleza.
Mzee Mkwawa alikuwa kapanga banda la uani vyumba viwili Kisosora na mkewe alikuwa anafanya biashara ya "Mama Ntilie," nyakati za usiku.
Juu ya hali zao za shida walikuwa nadhifu.
Mpiga picha wa Hollywood angeonyesha chumba kidogo nadhifu lakini hakina mwanga wa kutosha.
Camera ingemchuka Harith Ghassany akiwa kainama anamsikiliza Mzee Mkwawa.
Katika scene hii Harith kakaa vizuri kitini.
Sasa camera inatoka kwake inakwenda kwa Mzee Mkwawa.
Mzee Mkwawa yuko kizani ila kwa sura yake iliyopigwa na mashakili ya maisha iko katika mwanga na anaanza kuzungumza.
Maneno yake yanasindikizwa na "flashbacks," za mapigano na mauaji Zanzibar wakionyeshwa watu "ragtag," wameshika mapanga mengine yakivuja damu."
Muogozaji filamu anakata anairudisha camera kwa Dr. Harith Ghassany.
Scene hii ndiyo inamuonyesha Dr. Ghassany aliyeelemewa na yale anayosikia sasa hajiwezi tena anakalia mgongo wake.
Taratibu camera man anaingiza giza kwenye kile chumba na anawaonyesha wote wawili Mzee Mkwawa na Dr. Ghassany kama vivuli lakini sauti ya Tindo bado inasikika.
Lakini hapa Tindo yuko katika, "soliloquy," anaisemesha nafsi yake kwa sauti ya masikitiko.
Mzee Mkwawa aliniambia, ''Hivi kweli baada ya kazi yote ile niliyofanya ijaza yangu ni hii mimi leo kuishia kuishi kwenye banda la kuku?''
Mzee Mkwawa ndiye aliyekuwa akiwavusha hawa Wamkonde usiku kwa siri kuwapeleka Zanzibar.
Mohamed Omar Mkwawa
Joseph Mihangwa anaandika anasema: "EAMWS kiongozi wake alikuwa Mnajimu mashuhuri Afrika Mashariki, Sheikh Yahaya Hussein.
Ilifutwa mwaka wa 1968 kwa sababu ya kujijusisha na nambo ya siasa kwa ukinzani na serikali za Afrika Mashariki.
Ukweli ni kuwa Tewa Said Tewa ndiye alikuwa President wa EAMWS kwa upande wa Tanzania.
Sababu za serikali kuivunja EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu Cha Waislam.
Hili halikutakiwa.
Serikali ikavunja EAMWS na kuunda BAKWATA.
Tewa Said Tewa Rais wa EAMWS
JOSEPH MIHANGWA ANASEMA JULIUS NYERERE HAKUWA NA TAARIFA ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Kulikuwa na kambi Kipumbwi ambayo waliwekwa Wamakonde wakata mkonge na hawa Wamakonde walivushwa kuingia Zanzibar kupigia kura ASP Uchaguzi wa 1961 na walishiriki katika kupindua serikali mwaka wa 1964.
Hawa Wamakonde waliua Waarabu wengi waliokuwa wakiishi mashamba.
Dr. Harith Ghassany kaeleza kwa urefu historia hii katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).
Huu ndiyo ufahamu wa Joseph Mihangwa kuhusu historia ya mapinduzi ya Zanzibar na yalifuatia baadae.

JOSEPH MIHANGWA ANAVYOMWELEZA ABOUD JUMBE