Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Nimeshangazwa sana na kauli aliyoitoa Rais Magufuli wakati ajihutubia makada wenzie wa CCM kuwa wasibweteke kuwa watashinda kirahisi uchaguzi mkuu ujao, ambao unategemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na akawaeleza makada hao kuwa wapinzani wana mbinu nyingi za wazi na za kificho, kwa hiyo inabidi na wao wasibweteke na wawe macho sana, ili wasije kushindwa kwenye uchaguzi huo.
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi ni kitu gani kinachomtia hofu Rais wetu hadi aingie woga kiasi hicho hadi kuwatahadharisha wana CCM wenzie?
Hivi inakuwaje kwa wana CCMambao katika kipindi chote cha utawala wa awamu ya tano, mmekuwa mkitamba sana na kuita upinzani kuwa umekufa kutokana na juhudi kubwa za Rais Magufuli katika ujenzi wa Taifa hili, mkitoa mifano ya ujenzi wa reli ya kisasa wa SGR, ununuzi wa ndege kubwa mpya, ujenzi wa bwawa la umeme katika Mto Rufiji, ujenzi wa flyovers mbalimbali na ujenzi wa barabara za lami unaoendelea sasa nchi nzima?
Hivi inakuwaje kwa ushindi wa kishindo mlioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa asilimia 99.9 muingie "mchecheto" kwa upinzani ambao mmedai umekufa, ambao umejikongoja kwenye uchaguzi huo kwa kuambukia kura asilimia 0.1 pekee?
Kama kweli mlipata kihalali ushindi huo wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kama ambavyo mmekuwa mkituaminisha, msingekuwa na sababu za kuogopa upinzani ambao mnadai kwa upo kwenye "stretchers" ukisubiri kuzikwa rasmi.
Hilo ndilo swali langu kwa Mwenyekiti wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, ili mwenye jibu lake naomba anijibie.