Ni kwanini Rais Magufuli awaogope wapinzani aliowashinda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa asilimia 99.9?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,137
Nimeshangazwa sana na kauli aliyoitoa Rais Magufuli wakati ajihutubia makada wenzie wa CCM kuwa wasibweteke kuwa watashinda kirahisi uchaguzi mkuu ujao, ambao unategemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na akawaeleza makada hao kuwa wapinzani wana mbinu nyingi za wazi na za kificho, kwa hiyo inabidi na wao wasibweteke na wawe macho sana, ili wasije kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi ni kitu gani kinachomtia hofu Rais wetu hadi aingie woga kiasi hicho hadi kuwatahadharisha wana CCM wenzie?

Hivi inakuwaje kwa wana CCMambao katika kipindi chote cha utawala wa awamu ya tano, mmekuwa mkitamba sana na kuita upinzani kuwa umekufa kutokana na juhudi kubwa za Rais Magufuli katika ujenzi wa Taifa hili, mkitoa mifano ya ujenzi wa reli ya kisasa wa SGR, ununuzi wa ndege kubwa mpya, ujenzi wa bwawa la umeme katika Mto Rufiji, ujenzi wa flyovers mbalimbali na ujenzi wa barabara za lami unaoendelea sasa nchi nzima?

Hivi inakuwaje kwa ushindi wa kishindo mlioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa asilimia 99.9 muingie "mchecheto" kwa upinzani ambao mmedai umekufa, ambao umejikongoja kwenye uchaguzi huo kwa kuambukia kura asilimia 0.1 pekee?

Kama kweli mlipata kihalali ushindi huo wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kama ambavyo mmekuwa mkituaminisha, msingekuwa na sababu za kuogopa upinzani ambao mnadai kwa upo kwenye "stretchers" ukisubiri kuzikwa rasmi.

Hilo ndilo swali langu kwa Mwenyekiti wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, ili mwenye jibu lake naomba anijibie.
 
Hofu ya Rais ni kule Zanzibar sio huku bara

Huu ni mwaka wa Uchaguzi lakin kimya cha Mawakala wa Sultan kimerindima sana na si kawaida yao

Kuna dalili dalili za usaliti Visiwan kwny Uchaguzi wa mwaka huu ikiwa Mgombea Urais wa Visiwan atatokea Chimwaga badala ya Kiswandui
 
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi ni kitu gani kinachomtia hofu Rais wetu hadi aingie woga kiasi hicho hadi kuwatahadharisha wanaccm wenzie?
Kwenye uchaguzi hutakiwi kulala
Uliza yaliompata kaunda kwa chiluba
 
Hofu ya Rais ni kule Zanzibar sio huku bara

Huu ni mwaka wa Uchaguzi lakin kimya cha Mawakala wa Sultan kimerindima sana na si kawaida yao

Kuna dalili dalili za usaliti Visiwan kwny Uchaguzi wa mwaka huu ikiwa Mgombea Urais wa Visiwan atatokea Chimwaga badala ya Kiswandui

Hili nililiwaza baada ya kuona wakubwa wanapishana tu kisiwani.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huu ndio ujinga kutafsiri kauli ya rais kwamba ameingiwa 'na hofu. Subiri itakapotokea upinzani ukaambulia kiti kimoja cha ubunge, hatutaki kuanza kulialia hapa. Such a conclusion is a great msitake.
 
Lakini nyinyi si ndiyo mnaojimwamvafai kila siku kuwa upinzani nchini umekufa?

Sasa hofu yote hiyo ya nini?

Mkuu na ww umenasa kwenye hiyo mind game ya kuwa Magufuli anahofu na wapinzani? Kwanza ujue Magufuli hajali lolote hata kama ni kwa kuumiza wananchi, na hata madhara yatakayojitokeza kwa hatua za kikatili hana hofu nayo. Hofu pekee ataipata iwapo kutatokea machafuko ya muda mrefu ambayo yatampeleka yeye jela. Na kwa mwenendo wa vyombo vyetu vya dola, sioni wakiwa upande wa wananchi, na kumuacha kiongozi anayewapa upendeleo wa wazi. Katika mazingira hayo haogopi upinzani wa aina yoyote. Hiyo lugha ni kwa ajili ya yeye kuhadaa jicho la dunia kwamba kuna uchaguzi, jambo ambalo si kweli.
 
Siyo kwanba anaguswa na "consciousness" kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa waliiba kupita kiasi?

Hajali lolote maana hata alipokuwa mbunge ni mara chache sana alishinda kwa box la kura. Nadhani wapinzani tudai tume huru ya uchaguzi kwa nguvu, jambo ambalo silioni likifanyika hadi sasa, badala ya kunasa kwenye lugha za Hadaa za Magufuli.
 
Mkuu na ww umenasa kwenye hiyo mind games ya kuwa Magufuli anahofu na wapinzani? Kwanza ujue Magufuli hajali lolote hata kama ni kwa kuumiza wananchi, na hata madhara yatakayojitokeza kwa hatua za kikatili hana hofu nayo. Hofu pekee ataipata iwapo kutatokea machafuko ya muda mrefu ambayo yatampeleka yeye jela. Na kwa mwenendo wa vyombo vyetu vya dola, sioni wakiwa upande wa wananchi, na kumuacha kiongozi anayewapa upendeleo wa wazi. Katika mazingira hayo haogopi upinzani wa aina yoyote. Hiyo lugha ni kwa ajili ya yeye kuhadaa jicho la dunia kwamba kuna uchaguzi, jambo ambalo si kweli.
naona umeongea maneno mazima kabisa 100% uko sawa. CCM hawajali chochote na kwa taarifa yenu Uchaguzi umeshamaliza linalo subiriwa na kutangaza tu October tume ya uchaguzi washamaliza kazi
 
Wafanyakazi serikalini hali ngumu,biashara imeshuka,kilimo cha shida,ajira hamna,watu wameteswa,kauli mbaya,katiba mpya hakuna,maelewano dhaifu,marekani hatuendi,misaada finyu,madini nitabu,kodi inaumiza nk. nk. Kiufupi nitalishangaa jitu litakalopanga mstari massa kisa kumchagua aliyetuletea haya magugufuli
 
Back
Top Bottom