Ni kwanini Rais Magufuli awaogope wapinzani aliowashinda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa asilimia 99.9?

Viongozi wote wa CCM macho yao yako kwa watumishi wa serikali kuwasaidia kuiba kura basi. Viongozi wa ccm huku kwetu vijijini wanawaogopa sana wapiga kura. Uchaguzi ukianza kila siku kushinda ofisi za Halmashauri na za watendaji wa vijiji unaweza kudhani wapiga kura wanaishi ofisini.
 
Nimeshangazwa sana na kauli aliyoitoa Rais Magufuli wakati ajihutubia makada wenzie wa CCM kuwa wasibweteke kuwa watashinda kirahisi uchaguzi mkuu ujao, ambao unategemewa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu na akawaeleza makada hao kuwa wapinzani wana mbinu nyingi za wazi na za kificho, kwa hiyo inabidi na wao wasibweteke na wawe macho sana, ili wasije kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa, hivi ni kitu gani kinachomtia hofu Rais wetu hadi aingie woga kiasi hicho hadi kuwatahadharisha wana CCM wenzie?

Hivi inakuwaje kwa wana CCMambao katika kipindi chote cha utawala wa awamu ya tano, mmekuwa mkitamba sana na kuita upinzani kuwa umekufa kutokana na juhudi kubwa za Rais Magufuli katika ujenzi wa Taifa hili, mkitoa mifano ya ujenzi wa reli ya kisasa wa SGR, ununuzi wa ndege kubwa mpya, ujenzi wa bwawa la umeme katika Mto Rufiji, ujenzi wa flyovers mbalimbali na ujenzi wa barabara za lami unaoendelea sasa nchi nzima?

Hivi inakuwaje kwa ushindi wa kishindo mlioupata katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa asilimia 99.9 muingie "mchecheto" kwa upinzani ambao mmedai umekufa, ambao umejikongoja kwenye uchaguzi huo kwa kuambukia kura asilimia 0.1 pekee?

Kama kweli mlipata kihalali ushindi huo wa kishindo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kama ambavyo mmekuwa mkituaminisha, msingekuwa na sababu za kuogopa upinzani ambao mnadai kwa upo kwenye "stretchers" ukisubiri kuzikwa rasmi.

Hilo ndilo swali langu kwa Mwenyekiti wa CCM, Dr. John Pombe Magufuli, ili mwenye jibu lake naomba anijibie.
Hiyo ni danganya toto tu na kuwabeza CDM mufu. Ni sawa na mtu anakuambia jamaa yangu naona upo vizuri wakati shati lako limechanika mgongoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani bado kuna ahadi muhimu walizoahidi hawajazitimiza ambazo zinaweza kuwa fimbo yao ya kuadhibiwa ndio maana anayo hofu tena hofu kuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana.
Ni zaidi ya hapo. Ingekuwa ni swala la "kutimiza ahadi" pekee pasingekuwepo na hofu hiyo.

Jitahidi kufikiri kwa kina zaidi ya ulivyofanya. Mimi najua, lakini sikusaidii kwa hili.
 
Back
Top Bottom