Ni kwanini Commando huwa ni jasusi mzuri kuliko yule mtu wa kawaida tu aliyepitia mafunzo ya Usalama wa Taifa?

Acha uongo wewe. Vijana wengi wa UVCCM tumewapeleka usalama na hao nao ni makomando????!
Sasa UVCCM na usalama wapi na wapi? Jamani muwe mnasoma hata vile vitabu vya Akina Elvis Musiba. Hiki kizazi kwakweli Mungu kinusuru na uvivu wa kutafutwa maarifa. Tafuta historia ya Putin ndo utaelewa
 
Nimesikia mahala kuwa COMMANDO (si lazima awe wa Tanzania) ana uwezo wa kupata taarifa nyeti hata kuliko Mwana Usalama Taifa mwenyewe. Kwa mfano; COMMANDO wa Malawi anaweza akaenda nchini Zimbabwe katika maeneo yao muhimu na akapata akitakacho na wala asishtukiwe, lakini kwa Usalama wa Taifa wa Malawi anaweza kwenda ila atagundulika kwa haraka sana tu.

Wajuvi wa haya Masuala mliojazana hapa Jamvini JamiiForums, karibuni mtuelimishe na sisi akina Mzukulu ili nasi tuwe na Maarifa kama nyie pia.
usalama wa taifa wengi wanapenda sifa
 
Kazi ya usalama wa taifa ni kukusanya taarifa, kuchunguza na kufatilia kuna watu wa usalama wa taifa wao ni infomer kazi yao ni kujichanganya sehemu yeyote lakini komando mara nyingi ni mwanajeshi huyu anatumika zaidi kwenye vita huwa anatumika na kupeleleza nguvu za maadui
 
Namaanisha kwamba COMMANDO wa Jeshi, anaweza kupewa Oder Na anaweza kutumiwa na kazi za Usalama wa Taifa Katika kufanikisha Jambo lao isipo kuwa yeye sio Kwenye Kitengo chao na akafanya kazi yao Pasipo kujua. Maana hiyo ni taasisi kubwa.Mfano mzuri M 16 wa Uingereza
Sio M16 ni MI6
 
Yaani kile kitendo cha kuitwa usalama ndo kinachanganya sana na kuhisi n kitu hatari sana ila tusisahau hata usalama yetu ilimeguliwa polisi, hayo n majukumu tu yana taratibu zake za kazi ambazo ndo zinazipa uzito, km mtu wa kawaida anaweza kukusanya data mtaani (usalama) kwanini komando ashindwe, nilichokielewa kuwa ukitaja komando watu wana picha zao pichani za mapicha.
 
Usalama wa taifa wako kila mahali kuna usalama wa taifa polisi,kuna usalama wa taifa raia,kuna usalama wa Taifa jeshini,kuna usalama wa taifa kwenye vikosi vya makomandoo Maada yako hueleweki.Wako makomandoo usalama wa taifa.sasa unaposema tofauti ya usalama wa taifa na komandoo hueleweki
 
Mkuu wangu hizi taaluma zina uzito eake kulingana na majukumu husika kwa wkt huo. Komando hii ni nafasi ambayo kwanza lazima uwe ni askari jeshi kwa hapa Tz ni TPDF, wanajeshi hupitia mafunzo mbali mbali ya kikakamavu mpka kupewa kazi au kupangiwa kituo cha kazi na mpka anakua komando kunahatua anapitia kufika pale. Usalama wataifa ni chombo au taasisi ya kiusalama inayojumuisha kada zote za utumishi wa umma nia ni kupata taarifa na kujua nna gsni ya kuzikabili isitokee au kuleta janga kwa taifa, hawa hupatikana kulingana na historia zao, familia zao, makuzi yao na hata utendaji wao wa kazi hapo baadae. Pia hii taasisi haichagui kazi husika ya mtu wao mfano ina wanajeshi, polisi, walimu, wafanyabiashara, wakulima na hata watu ambao kijamii huona hawajitambui na hawa hupewa mafunzo namna gani ya kufanya majukumu yao ya kila siku. Sasa utofauti wao unakuja ktk namna ya ufanyaji wa kazi husika, Komando atafuata alichoambiwa ktk kazi ila pia atakua na ujuzi binafsi ukumbuke huyu ni askari jeshi alie komaa kimafunzo hivyo kukamatwa kwake pia kunataka umakini sana. Jasusi au mwana usalama pia ni m'bibezi ktk fani yake ya kupata taarifa ingawa hawa ni ngumu kuwafamahu kwan hawatokei tu bali ni pandikizi kwa muda fulani na wana kua na uthibitisho sahihi mahali wanapofanyia kazi, mfano hawezi kupangiwa ubalozini bila kua ma kigezo cha kua pale kama afisa ibalozi husika. Suala la nani anaweza kukamatwa kwa urahisi hiz zinakua ni makosa ya kibinaadamu ktk kazi ndo hupelekea kugundulika kwa wahusika na hata ukamataji wake sio sawa na kutuma defender ya polisi. Nani yuko makini zaidi ya?????? Hiko swali bado linabaki kwa watendaji husika.
 
Back
Top Bottom