Ni kisa au mkasa gani uliwahi kufanyiwa na ndugu au mtu wako wa karibu?

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,141
32,850
Habari za muda huu wapendwa

Bila shaka kwenye safari ya maisha kila mmoja wetu amewahi kukumbana na visa na mikasa mbali mbali kwenye purukushani za maisha

Mikasa ambayo imekuwa ikitupa mafunzo na mafundisho maishani mwetu na wakati huo huo kubadilisha kabisa mitazamo ya maisha yetu juu ya watu.

Watu wetu wa karibu ni watu tunaowategemea kwenye maisha yetu Kwa mambo mbali mbali lakini pia watu hao hugeuka na kutuletea vilio vya kudumu vyenye machungu maishani mwetu.

Je umewahi kufanyiwa mkasa, kisa au tukio Gani baya na ndugu au mtu wako wa karibu?

Mimi niliwahi kuchomewa utambi kazini na mtu wangu wa karibu...ambaye nilikuwa na share mambo yangu kibao na hata niliwahi kumpa mtaji wa biashara, lakini kumbe alikuwa anachukia mafanikio yangu tangia hapo nikabadilisha kabisa mtazamo wangu juu ya marafiki na watu wangu wa karibu. Kwa kifupi nikawa na chujio mdomoni mwangu na kichwani mwangu.
 
Nilishushwa kazi na mtu niliyemsaidia apate kazi kwenye kampuni nilipo.

Akawa hanisalimii Wala kuongea na mimi, pia akawa ananicheka baada ya kurudi chini yaani kutoka kuangaliana na Computer hadi kushika Spana kama fundi, sikujali kushuka kwa mshahara na marupurupu.

Nililazimisha furaha machoni pa watu huku Kila mtu akinishangaa wengine waliniita chizi au nimerogwa sikujali, nilizungukia Equipments zote za kampuni huku yule jamaa akinifanya kunisifia kuwa Mimi ni fundi Bora kwa vifaa vyote vinafanya kazi kwa usahihi.suti na tai vilimpendeza akajiona kamaliza maisha

Lakini acha MUNGU aitwe MUNGU, nilipeleka CV zangu mahali, nikapokelewa freshi , huku nikiwaonesha Nini maana ya
Mechanical engineering, nikapewa na dereva juu maanina.
 
Pole sana mkuu, hongera pia kwa kuonyesha kua haukua-disappointed
 
Ndugu yangu wa mbali kaja mjini kakaa kwangu miezi 2. Cha ajabu alivyoondoka kaenda kunianika kijijini kuwa tunakula wali maharage Kila siku jioni....na Dagaa kabichi mchana na kwamba wife atakua mchoyo!
 
Nilishushwa kazi na mtu niliyemsaidia apate kazi kwenye kampuni nilipo.

Akawa hanisalimii Wala kuongea na mimi, pia akawa ananicheka baada ya kurudi chini yaani kutoka kuangaliana na Computer hadi kushika Spana kama fundi, sikujali kushuka kwa mshahara na marupurupu.

Nililazimisha furaha machoni pa watu huku Kila mtu akinishangaa wengine waliniita chizi au nimerogwa sikujali, nilizungukia Equipments zote za kampuni huku yule jamaa akinifanya kunisifia kuwa Mimi ni fundi Bora kwa vifaa vyote vinafanya kazi kwa usahihi.suti na tai vilimpendeza akajiona kamaliza maisha

Lakini acha MUNGU aitwe MUNGU, nilipeleka CV zangu mahali, nikapokelewa freshi , huku nikiwaonesha Nini maana ya
Mechanical engineering, nikapewa na dereva juu maanina.
Chai
 
Kisa kizuri sana ila usingemalizia na tusi ningekupa like kabisa asee

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana ikawa nje ya mada kidogo maana haikuwa ndugu ila nitatoa kisa changu.

Nilishawahi kuajiriwa na muhindi mmoja kama project manager. Ali apply tender iliyohusisha kuweka signage (mabango) nchi nzima kutoka kampuni moja maarufu ya Makaburu (South Africans). Kipindi hicho ilikuwa project yenye thamani ya kama $100,000.

Kabla ya kupata tender kulikuwa na bidding ambapo moja ya sharti ilikuwa ni kuwakilisha installation plan (proposal) iliyohusisha uchambuzi wa matumizi ya budget, utekelazaji wa kazi mpaka kukamilika kwake.

Nilifanya kazi ya kuandaa plan wiki 2 nzima usiku na mchana maana ilikuwa inahitajika haraka. Ilipotimia na kuwakilishwa muhindi akashinda tender.

Ilipoidhinishwa tu kuwa kashinda jamaa akaniambia kuna muhindi mwenzie toka India (expatriate) atasimamia hiyo project (kutumia plan yangu), moja ya makubaliano yetu ya awali ilikuwa nitaisimamia mimi hiyo project yote endapo proposal yangu itapita.

Aliposema mambo ya expatriate tu nikatoa notice yangu ya mwezi mmoja ya kuacha kazi.

Kipindi nataarisha plan ya hiyo project nilifanya research ya kutosha nikijua nitasimamia mimi mwenyewe hivyo niliweza kuhalalisha baadhi ya matumizi ya budget nikijua nitafanikisha vipi baada ya research yangu.

Phase ya kwanza ya project ilianzia mikoa ya Tanga, Arusha na Moshi. Muhindi alipopewa mzigo installation ianze akachemka baada ya kumaliza Tanga tu. Pesa ilikata na kazi hata robo haijaisha.
Kila sehemu ilikuwa na time limit kama ilivyoanishwa kwenye proposal plan, muhindi alichemka phase ya kwanza tu huku ikiwa keshachukuwa advance ya Mkaburu.

Nilifanya presentation mimi mwenyewe kwenye bidding kwa niaba ya muhindi, hivyo sharti aliliopewa na makaburu ni kuwa aliendaa na kufanya presentation ya proposal ndio asimamie project la sivyo atanyang'anywa kazi.

Ilibidi muhindi anitafute tukae chini tena akiahidi offer kubwa kulinganisha na ya awali. Nilimkatalia na wakati huo huo nili apply kivyangu kwa makaburu wanipe project mimi kama mimi.

SIkuwa na kampuni yangu hivyo ile project ikahamishiwa kuwa in house project kumaanisha walianzisha kitengo maalum cha signage ndani ya kampuni yao kuanzia production mpaka installation na mimi nikapewa hicho kitengo kukisimamia. Hivyo badala ya Project Manager nikawa Division Manager.

Kwa ile phase ya kwanza ilimlazimu muhindi kumaliza na ilibidi areport kwangu moja kwa moja kwa niaba ya kaburu, karma is real.

Sehemu ya kazi iliyobaki iliisha kwa wakati na mpaka sasa kupitia hiyo project kitengo cha signage kwenye kampuni ya kaburu kimekuwa one of the leading signage companies kwa Tanzania.

Katika maisha chochote kinachopaswa kuwa chako kitakuwa chako tu haijalishi kitachelewa kwa kiasi gani.
 
Nilishawahi kuajiriwa na muhindi mmoja kama project manager. Ali apply tender iliyohusisha kuweka signage (mabango) nchi nzima kutoka kampuni moja maarufu ya Makaburu (South Afrcans). Kipindi hicho ilikuwa project yenye thamani ya kama $100,

Katika maisha chochote kinachopaswa kuwa chako kitakuwa chako tu haijalishi kitachelewa kwa kiasi gani.
Yeah ni kweli. Kilicho chako kitakuwa chako hata kama kitachelewa.
 
Back
Top Bottom