Ni jiji lipi linampa mtu fursa ya kuanza biashara na kukua kwa biashara yake?

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,678
Dar es Salam ni jiji ambalo biashara nyingi ni za kubangaiza tu kwa mtu mwenye mtaji chini ya million 5, maana gharama ya frame, stoo ni kubwa sana.

Mfano ukifungua duka la accecories za simu Dodoma/Arusha, kukua kibiashara ni rahisi kuliko kufungua duka kama hilo Dar es Salam. Watu wengi kwa Dar wana amini mahitaji yote watayapata Kariakoo kwa unafuu, so ukifungua duka la accecories za simu Chanika au Mbezi sidhani kama maokotoo yatakua makubwa (mtazamo wangu).

Ukisema ufungue nafaka Dar es Salam utakuta watu wanauza hizo nafaka kwa ukubwa wake, mfano Tandale, Mwananyamala,Tandika n.k.

Kwa jiji kama la Dar es Salam naona ni bora kuuza huduma (services) zaidi kuliko bidhaa (goods) kwa wingi ule wa watu hapo lazima pesa zikutembelee.

Ni mtazamo tu, wewe waonaje?
 
Dar es salam ni jiji ambalo biashara Nyingi ni za kubangaiza tu kwa mtu mwenye mtaji chini ya million 5, maana gharama ya frame, stoo ni kubwa sana...
Mimi huwa na waza kwa jiji kama Dar kutoboa ina weza kuwa rahisi kwa kiasi chake. Mfano una weza kuwa na mtaji mfano 8M, ukaamua kwenda mikoa ya nyanda za juu kusini una chukua viazi vya chips au ndizi mbichi. Una kodi fuso then una leta mabibo sokoni una uza ukimaliza una rudi tena shamba kufuata.

Mimi naamini hii ina weza kuwa njia bora zaidi ya kukukuza kiuchumi kwasababu jiji kama la Dar lina watu wengi na hao watu lazima wale chakula na wewe una uza chakula na hao watu wasipo kula wata kufa kwahiyo lazima wale.
 
Mimi huwa na waza kwa jiji kama Dar kutoboa ina weza kuwa rahisi kwa kiasi chake. Mfano una weza kuwa na mtaji mfano 8M, ukaamua kwenda mikoa ya nyanda za juu kusini una chukua viazi vya chips au ndizi mbichi. Una kodi fuso then una leta mabibo sokoni una uza ukimaliza una rudi tena shamba kufuata. Mimi naamini hii ina weza kuwa njia bora zaidi ya kukukuza kiuchumi kwasababu jiji kama la Dar lina watu wengi na hao watu lazima wale chakula na wewe una uza chakula na hao watu wasipo kula wata kufa kwahiyo lazima wale.
Hahahahaaa daaaah
 
Mimi huwa na waza kwa jiji kama Dar kutoboa ina weza kuwa rahisi kwa kiasi chake. Mfano una weza kuwa na mtaji mfano 8M, ukaamua kwenda mikoa ya nyanda za juu...
Asante mkuu Umeongea vizuri sana Lakini ni Bora kufanya hivyo kwa miji inayokua kuliko kufanya hivyo kwa Dar-es-salam, kwanini ? Dar-es-salam utu ni mdogo sana Mimi nilileta Michele Hapo kwa njia hiyo Cha ajabu mzigo unamuachia dalali auzee ndio akupe Hela, watu wengi wametapeliwa na kulizwa kwa mtindo huo.
 
Asante mkuu Umeongea vizuri sana Lakini ni Bora kufanya hivyo kwa miji inayokua kuliko kufanya hivyo kwa Dar-es-salam, kwanini ? Dar-es-salam utu ni mdogo sana Mimi nilileta Michele Hapo kwa njia hiyo Cha ajabu mzigo unamuachia dalali auzee ndio akupe Hela, watu wengi wametapeliwa na kulizwa kwa mtindo huo.
Kuwa wewe mwenyewe dalali.Kazi ya udalali ni kazi ya kawaida,hata wewe waweza kuwa dalali.
 
Dar es salam ni jiji ambalo biashara Nyingi ni za kubangaiza tu kwa mtu mwenye mtaji chini ya million 5, maana gharama ya frame, stoo ni kubwa sana. Mfano ukifungua duka ...
biashara ni kama maji hufuata mkondo mkuu. namanisha si lazima uwe ndani ya jiji na unaweza piga pesa nyingi sana unaweza kuwa nje ya jiji hata aliyoko jijini ukamshangaza, mfano kuna mama mmoja namfahamu anatoa maziwa meru uko arusha kwa wakulima lt ananunua 1000 lakini anapeleka tarakea lt anauza 2100 kwa siku anachukua zaidi ya madumu 9 ya lt 20 usafiri anatumia daladala ya kukodi saa10 alfajiri 15k. kwa siku huyo mtu anatengeneza laki 3 isiyo na makato ya kodi. huwezi amini wala hajataka kununua gari lake ila izo nyumba za kupanga alizo nazo acha kabisa.
 
biashara ni kama maji hufuata mkondo mkuu. namanisha si lazima uwe ndani ya jiji na unaweza piga pesa nyingi sana unaweza kuwa nje ya jiji hata aliyoko jijini ukamshangaza, mfano.kuna mama mmoja namfahamu anatoa maziwa meru uko arusha kwa wakulima lt ananunua 1000 lakini anapeleka tarakea lt anauza 2100 kwa siku anachukua zaidi ya madumu 9 ya lt 20 usafiri anatumia daladala ya kukodi saa10 alfajiri 15k. kwa siku huyo mtu anatengeneza laki 3 isiyo na makato ya kodi. huwezi amini wala hajataka kununua gari lake ila izo nyumba za kupanga alizo nazo acha kabisa.
Hapo umenena jambo mkuu.
 
Kuwa wewe mwenyewe dalali.Kazi ya udalali ni kazi ya kawaida,hata wewe waweza kuwa dalali.
Shida uwezi fika tu pale mabibo na fuso lako la viazi au pale ilala na fuso la vitunguu ukaanza kuuza, changamoto ni moja hata au madalali pia Wana watu wao ambao ni trusted kwa dalali (anamuachia mzigo Bure pesa anarejeshewa baadae) umeiona hiyo chain? Kwahiyo lazima urudi kwa madalalio tu ambapo 50/50 kupewa Hela au kupewa kidogo.
 
Hapo umenena jambo mkuu.
kwenye biashara ukijipata vizuri na kuwa na misimamo utakuja kupiga hela nzuri tuh we komaa kikukwa biashara ilinde mtaji utakuja kuniambia.alafu usionyeshe mabadiliko yoyote kimavazi nk ndani ya jamii inayoizunguka biashara yako bila kusahau yoyote anayekuliza juu ya biashara yako mwambie inakukukata sana
 
Nakupinga. Ww bado huujui huu mji.
Kuna maeneo ukiweka duka la vifaa vya simu bado utauza sana kuliko ukiweka Dom au Arusha, Mfano wa maeneo hayo ni gongolamboto, mbezi mwisho , kimara, Mbagala, tandika, makumbusho nk Sio lazima ufungue ofis kkoo
hii kitu pia nimemwambia si lazima uwe mjini kati popote pale kikubwa tizama jamii inataka nini nenda nao sawa
 
kwenye biashara ukijipata vizuri na kuwa na misimamo utakuja kupiga hela nzuri tuh we komaa kikukwa biashara ilinde mtaji utakuja kuniambia.alafu usionyeshe mabadiliko yoyote kimavazi nk ndani ya jamii inayoizunguka biashara yako bila kusahau yoyote anayekuliza juu ya biashara yako mwambie inakukukata sana
Shukrani sana, nilichoelewa kwenye andiko lako maisha ni popote tu sio lazima mtu akae mjini kimsingi Uwe kwenye njia ya pesa.
 
Upo sahihi mkuu.
hii ndiyo njia nayoitumia siku zote huwa nalalamika tuuh juu ya biashara nayoifanya lakini faida naijua mimi ndio mana siachi.ujue hakuana haja ya kua na duka lime jaa huo ni ushamba hili liko sana mikoani , wewe kuwa na stoo yako ya uchochoroni nyumbani ikiwezekana alafu piga badika bandua ya bidha uwone kama kunamtu atakufikia.
 
Back
Top Bottom