Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Duh! Aisee hii kali. Unataka kusema hata hizo sheria na kanuni na taratibu ni feki.
Hiyo ya likizo nimetoa mfano ambao ni rahisi kueleweka. Likizo haijakataliwa; kilichokosekana ni hela. Na kuna malipo mengi mengine ya kisheria hayajafanyika.

Sababu ya msingi? Pesa hakuna. Mbona wanafunzi na walimu wao waliotakiwa kwenda field wamepata matatizo hayo hayo. Pesa zilipelekwa baadaye; na hazikutosha.
Kuna kichekesho cha wanafunzi wa vyuo na mikopo ya elimu ya juu. Sitakisema kwa sasa.

Kukosekana kwa fedha mtaani si suala la kuwabana mafisadi. Hela halali imepotea.
Likizo hewa zilikuwepo. Mfano mtu anafanya kazi Mafinga. Kwao ni Iringa mjini. Anajaza likizo kwenda Kigoma Ujiji.
Hana mke wala mtoto lakini analipwa nauli ya mke na watoto wanne. Badala ya kupita njia fupi (easiest route) atazungukia dsm.
Na likizo wala haendi. Je unasemaje hapo?
 
Nyani Ngabu

Kwa mizinga ilivyozidi na watu wanavyotaka safari kama tumerudi tena 1999 naweza kusema kuna tofauti kiuchumi Tanzania hata mimi niliye nje naiona.

Ona huyu njaa inamfanya atake kwenda nje kucheza picha za uchi

Mtihani: Sina kazi ila nimepata fursa ya kutengeneza filamu za ngono nje ya nchi

Haipiti wiki sijaambiwa kuna kiwanja kinauzwa, tena vimeporomoka bei kutoka milioni 30 mpaka milioni 1 siku hizi.

Kweli ufisadi mbaya, na kuupiga vita ni wajibu, lakini lori la tani 40 ukipiga breki ili kubadili njia upige breki kwa mahesabu ili usije sababisha ajali na kuua watu.

Unaweza kupiga breki ghafla ukaua watu hata kama njia unayotaka kwenda ni sahihi.

Andija koyomba noo libehi geke litoeta chiza mamihayo genago ga nya chilochilo gete.

Obese tole mamnho ga masala nyalali pye mang'ingwana gatumanile, aleyo ng'wene oyo weta mamihayo nya chilo chilo gete.

Ahene ale igulu henaho, galeho mamnho minge gete gatotogwile noo mamihayo aleta.
Mamho genago gakobiza kufumbula miso loshiko lomo ese yene eye bakopela gete ba Magufuli.

Noni ya ng'wigulu mashikolo hagati, aleyo ng'wene oyo aleta geke amanile ese pye. Ateho masala pene apo.

Hagaaayaaa!

Lolagi e mbina ja kaya basumba batale baleeta mbina CHOMBO KADETE


Nimemind Magufuli mpaka nimeshusha internal service hapa kwa msisitizo.

CC Azarel
 
Nakerwa na tabia ya maskini wanaotamani matajiri nao wawe maskini!
Badala ya kutamani na wao wawe matajiri.
Malipo halali yanaitwa 'dili'
Wanabana matumizi wanasema wanapambana na wapiga 'dili'
Hakuna increment bado wanakazania hakuna fedha za 'dili'
Ajira mpya hakuna kisa hakuna fedha za 'dili'
Posho wanaziita 'dili'
Malipo ya huduma yanaitwa 'dili'
Sukari bei juu kisa? hakuna sukari za 'dili'
 
Hiki kinachosemwa kwenye hii article ya Prof. Ochonu ndicho kinachosemwa na mleta mada. Tofauti ni lugha tu.

Mleta mada ameleta kwa lugha ya kiswahili wakati Prof. Ochonu ameandika kwa lugha ya kiingereza.

Possibly but I believe the two do not share the same worldview. Mleta mada anasema "inaonekana kama vile pesa hakuna" wakati ni kweli pesa imekuwa ngumu (malalamiko ya "pesa imekuwa ngumu" ni real). Wakati mleta mada na Prof. Ochonu wanakubaliana kwamba "pesa imekuwa ngumu" ni kilio kinachosema "bring back corruption" (kutamani kurudi wakati ambapo rushwa ilitamalaki), mleta mada anaunga mkono mapambano dhidi ya rushwa yanayopelekea "pesa kuwa ngumu" ilihali Prof. Ochonu anakosoa kile anachokiita "neoliberal anti-corruption rhetoric". Mahali ambapo rushwa imekuwa sehemu ya maisha na sehemu kubwa ya uchumi, unapopambana nayo kienyeji utasababisha ugumu wa maisha (probably a no brainer). Ni kweli Magufuli hazuii madalali kufanya kazi na kujiingizia kipato, lakini kwa kupambana na rushwa conventionally anawanyima ulaji madalali waliotegemea uwepo wa pesa za rushwa kwenye mzunguko. Wanaoathirika na mapambano dhidi ya rushwa yasiyozingatia uhalisia wa maisha si wala rushwa pekee bali pia wale ambao wanafanya kazi halali lakini zinazotegemea uwepo wa pesa za rushwa kwenye mzunguko e.g. vibarua kwenye miradi ujenzi, gardeners, clearing and forwarding agents, mpaka wachuuzi wa samaki.
 
Kuna watu hawawezi kukaa bila kuanzisha thread matokeo yake ndio thread za kitoto kama hizi!

1. Bandari washasema mizigo imepungua, madereva wanakosa kazi!

2. Hivi mlundikano wa kodi huuoni?
Watu hawapewi ajira, nalo hujui?

3. Nyongeza za mishahara zimesitishwa, hivi hata hilo hujaskia?

4. Posho za vikao hakuna, au Posho ni ufisadi?

Hebu kuweni na uchungu na vilio vya watu!
 
Ufisadi ulishakuwa sehemu kubwa ya uchumi kiasi kwamba watu wengi walikuwa wananufaika nao kwa namna ya moja kwa moja ama nyinginr.

..hapo sasa.

..haitoshi kuziba mianya ya kuishi kiujanja-ujanja.

..wanatakiwa wafungue mianya ya kuishi kwa njia za halali.

..vijana wanamaliza vyuoni halafu wanaambiwa wajiajiri. Hawana uzoefu wala mitaji. Sasa wakianza kuishi kuijanja-ujanja wanalaumiwa.

..un-employment figures nchi hii zinatisha.
 
Nilimskia Rais naye akilalama kuwa wapo watu wameficha pesa ndio mana pesa hazipo kwenye mzunguko wa kiuchumi na kutisha kubadilisha noti ghafla kwa sababu yao ili washindwe kuzitumia vipi Nyani Ngabu unaonaje kauli hii ya rais hata rais mwenyewe amekiri pesa imekuwa haba kwenye mzunguko na alisema ni imefichwa na watu sio kukosekana kwa pesa ilokuwa inapatikana kwa ufisadi.
 
Mtu katoa maadA kuhusu mambo ya uchumi na Hali ya maisha wewe unaanza kum attack yeye na mambo binafsi... ACHA UTOTO NA SIFA ZA KIJINGA.. KUWA MKUBWA USIWE MSHAMBA WA MITANDAO
hajui kitu kinachoendela nyumbani ni sawa mtu anaanza kuongelea mambo ya nyumbani kwako huku hajui matatizo uliyonayo.


swissme
 
Kuanzia mwezi machi wastaafu hawajapata mafao yao. Statutory Increments na promotions zimesimamishwa, biashara zimefungwa kwani hamna wanunuzi, employments frozen, mazao hayauziki, bodi ya mikopo haijavilipa vyuo ada za wanafunzi, MSD waliomba 180 milioni wamepewa 20, dawa vituo vya afya hamna, endelee kutaja majanga mengine ndipo utajua fedha zipo au hazipo. Lakini hata tushangilie na kujiliwaza kwa kupata bombadia mbili.
 
Pesa ya Madafu.Yan pesa ya madafu.
Mkwanja uppo sana sema tu mmelaza fikra zenu kutafuta, mpo bzy sana ku complain no money utadhani mmeolewa na mabwana zenu hawa waletei matumizi.
 
Pesa imepungua mifukoni,Shughuli za kibiashara zinaendelea kudolola,nanyingine zimefungwa.Utafikiri matajiri wao wameondoa pesa kwenye mzunguko,na serikali imeshindwa au haina uwezo wa kuziba hilo pengo.Kwa vyovyote waadhirika wakubwa ni watu wenye kipato cha chini ambao ndio wengi.
 
Business imekuwa ngumu sana
Purchasing power imepungua mnoo
why purchasng power ipungue kama watu walikua wanatumia vipato halali toka mwanzo?maana kwa kumbukumbu zangu rais hajapunguza mshahara wa mtu wala kumnyima mtu mshahara
 
Pesa za kijanja ziliwafanya watu wasiwe na nidhani ya kuzitunza.

Watu walikuwa wana spend with reckless abandon.

Sasa mambo yamebadilika.

Kuna watu imebidi hadi wauze magari yao ya kifahari, wengine imewabidi wawahamishe shule watoto wao, na kadhalika.
Waliouza magari nawafahamu wengi, wengine walikuwa na magari zaidi ya sita na sasa wamebaki na mawili Au moja

Bora kikwete
 
why purchasng power ipungue kama watu walikua wanatumia vipato halali toka mwanzo?maana kwa kumbukumbu zangu rais hajapunguza mshahara wa mtu wala kumnyima mtu mshahara
Kupungua kwa purchasing power hakutokani na mabadiliko ya mshahara pekee,
Sio kila mtu ana mshahara tanzania hii, hii nchi asilimia 85 ni wakulima, mshahara wao ni mavuno yao, uchumi umeyumba,watu hawaspend money kwenye mzunguko, wengi wanafanya manunuzi ya msingi tu
Hakuna extra Money kwenye mzunguko
 
P1030144.jpeg
Kero+ya+Maji+Kisarawe.jpeg

wewe unakula ma kuku broiler huku watu wanashinda siku nzima bila kula.
sijui hao watu unaowatete ni washua wa masaki au watanzania kumbuka watu hawa hata pembejeo.


swissme
 
Back
Top Bottom