Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,142
- 143,750
Karibu kila kona siku hizi utasikia watu wanasema eti oh hela imekuwa ngumu kupatikana.
Sasa mimi nauliza, ni hela ipi hiyo ambayo imekuwa ngumu kupatikana tokea mheshimiwa MTUKUFU rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ashike madaraka?
Kama mtu ulikuwa unaishi kwa kutegemea kipato chako halali na bado unaendelea kukipata, huo ugumu unatokea wapi?
Au mshahara wako umepunguzwa tokea Magufuli ashike madaraka?
Mimi nadhani Watanzania tulilemazwa sana na uchumi wa kifisadi. Tuliuzoea na tukaukubali na kuufanya uwe sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.
Sasa huyu kamanda mpya alipoingia na kujaribu kuziba ziba mianya ya hizo pesa za kijanja kijanja ndo maana inaonekana kama vile pesa hakuna.
Lakini kwa vile ufisadi ulishakuwa sehemu [isiyo rasmi] ya uchumi wetu kwa kiasi kikubwa, kuzibwa kwa mianya ya upatikanaji wa hizo pesa haramu lazima kutaleta athari flani katika sekta mbalimbali ambazo naamini ni za mpito tu.
Uchumi wetu ulikuwa feki mno. Pesa walizokuwa nazo baadhi ya watu wachache zilikuwa haziendani kabisa na hali halisi ya uchumi wetu wa dunia ya tatu.
Kwa hiyo mimi sidhani kama hela iliyo halali imekuwa ngumu kupatikana. Labda uniambie hela ya kifisadi ndo imekuwa ngumu. Lakini si vinginevyo.
Je, wewe mdau wasemaje? Nimepotoka katika muono wangu?
=== Majibu===

Katika jukwaa letu pendwa la Siasa kumeibuka mjadala kwamba NI HELA IPI IMEKUWA NGUMU?. Mjadala huu umeanzishwa na Nyani Ngabu akidai kwamba eti hakuna sababu za msingi kulalamika kupungua kwa vipato. Nakubaliana kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakitegemea ufisadi na rushwa katika kuendesha maisha yao. Lakini hata kwa wale waliokuwa wakitegemea kipato halali na kipato hicho hicho halali kimepungua. Tunaomba tuheshimiwe na mfumo urekebishwe.
Kuna baadhi ya hoja zinazodhibitisha kuwa vipato vyetu halali kimepungua.
Posho Stahiki kwa mujibu wa Sheria, Kanuni za Kudumu na Nyaraka
Kwa mujibu wa Sheria, Kanuni za Kudumu na Nyaraka watumishi wanazostahiki zao ambazo kwa sasa baadhi zimekuwa hazitolewi ama kwa wakati au kutokutolewa kabisa. Mfano:-
- Ongezeko la Mshahara la Mwaka. Kwa mujibu wa mkataba wa ajira mshahara wa mtumishi wa umma unatakiwa kuongezeka kiasi Fulani kwa kila mwaka. Mantiki ya kufanya hivyo ilitokana na kuongezeka kwa gharama za maisha pindi mwaka mpya wa fedha unapoanza. Ngani Ngabu nijibu ni lini mshahara umeongezwa kwa 2016/17? Je, gharama za maisha zimepanda kiasi gani?Tukilalala kipato halali kimepunguzwa msituone wajinga.
- Kanuni za kudumu zinatoa stahiki za kulipwa posho ya masaa ya ziada ambapo mda wakazi huisha saa 9.30 na kwa mfanyakazi atakeyafanya kazi zaidi ya hapo anatakiwa kulipwa posho ya masaa ya ziada kama fidia kwa mda ambao angekuwa anafanya shughuli binafsi. Leo hii wahasibu tunafunga hesabu za CAG mpaka saa4 usiku bila posho ya masaa ya ziada
Ujasiliamali
Watanzania wengi waliokuwa wakijishughulisha na ujasiriamali kipato chao kimepungua sana. Hii imesababishwa na biashara kuwa mbovu kutokana na kupungua kwa purchasing power. Wateja wengi wa wajasiriamali walikuwa ni watumishi wa umma ambao kipato chao cha halali walikuwa wakigawana na ndugu zao wasio na kazi. Mfano mimi nikipata kijiposho nawatumia wazazi, madogo,bibi yangu na hata machizi wangu katika kugawana umasikini. Ni vibanda vingapi vya ujasiriamali vimefungwa? Nao walikuwa wanavipata vya kifisadi?
Kilimo
Msimu wa mavuno ulikuwa mbaya sana kwa wakulima. Mfano sote tulishuhudia kwenye media kwamba wakulima wa nyanya na mbaazi walikula hasara. Serikali ilichofanya ni kukataza kuuza mazao nchi za majirani. Kipato cha wakulima hao kilikuwaje? Kilibaki kama kilivyo kipindi cha JK? Watu tumejitoa kulima matikiti tukilia taimingi Tanzania ya wiwanda vya Magufuli?Matikiti yanajiozea tu kwenye meza za masoko na mashambani.
Huduma za Afya
Tatizo hili limekuwepo toka enzi za JK. Huduma za afya ni mbovu sana, kuna upungufu mkubwa sana wa madawa muhimu katika hospitali za umma, vituo vya afya na zahanati. Kwa hiyo pamoja na kuwa na NHIF na CHF nalazimika kwenda kwenye duka binafsi kununua madawa kwa ajili yangu, mke ,watoto na wategemezi wangu wote. Ndugu zangu kule kijijini hawana kipato zaidi ya kuuza mazao najikuta nategemewa sana kusaidia pale ndugu anapopata shida ya kiafya.
Kupuuzwa kwa watumishi wa umma
Appreciation kwa mtumishi wa umma au mtumishi yeyote ni sawa na kumuongezea kipato. Nani hapendi heshima hata kama ni mfagizi.
Hakuna kipindi kigumu kama hiki kwa watumishi wa umma kama awamu hii. Watumishi tunadharauliwa sana na viongozi. Mheshimiwa raisi amekuwa na lugha mgumu sana kwetu.Tumekuwa tunaitwa majina ya ajabu ajabu yasiyo na heshima. Nataka kuamini hata kuchomwa kwa wenzetu kule Dodoma wakifanya kazi ya serikali ni zao la kupuunzwa. Watumishi wa afya wamekuwa wakitukanwa matusi ya nguoni na wateja. Nani anawapa kiburi hiki wananchi?
SWALI LA KIZUSHI
Nyani Ngabu kanunuliwa? Mbona alikuwa ana hoja makini kinzani dhidi ya mwenendo wa Serikali. Amekutana na Mzee Mwanakijiji huko Marikani ‘‘kalishwa sumu’’?
Itaendelea (to be continued)
Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?