Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Binafsi sidhani kama hela ilikuwa nyingi kwa sababu ya ufisadi. Ni suala la sera. Bwana Magufuli kaamua kuwa na sera ya kubana matumizi. Hii si sawa na kuondoa ufisadi.

Ninavyojua katika sekta ya umma malipo mengi ya halali (kadiri ya sheria au taratibu) yamesitishwa. Kuna watu, kwa mfano wanadai hela ya likizo wanayostahili. Hawajapata. Hii nayo ni hela ya kifisadi?
Mkuu pesa kama za likizo ni za muda mfupi Nazo si nyingi kiasi cha kuleta mtafaruku kwenye vipato halali vya watu, Kusitishwa kwa baadhi ya matumizi inaweza kuwa ni mpango wa muda mfupi ili kuweza kutambua nani anastahili kulipwa ki halali na nani halipwi kihalali(Ndio maana ya uhakiki).
 
Hizo zilikuwa ni likizo halali au?

Maana ufisadi hauishii kwenye pesa tu.

Hata likizo feki nazo ni ufisadi kama ilivyokuwa mishahara hewa.

Naamini kutakuwepo na sababu ya/za msingi ya/za kusitisha hayo malipo.
serikali haina hela,vipaumbele vingi kutokana na ahadi za kampeni alizotoa na magu na ccm yake wameona bora kuwaumiza watumishi kwa kutowapa stahiki zao(kupandishwa vyeo,malimbikizo ya mishahara,likizo,posho ya uhamisho nk).Lakini wasichojua ni kuwa mwisho wa siku morali itapungua na matokeo yatakuwa mabaya sana.
 
Likizo hewa zilikuwepo. Mfano mtu anafanya kazi Mafinga. Kwao ni Iringa mjini. Anajaza likizo kwenda Kigoma Ujiji.
Hana mke wala mtoto lakini analipwa nauli ya mke na watoto wanne. Badala ya kupita njia fupi (easiest route) atazungukia dsm.
Na likizo wala haendi. Je unasemaje hapo?
unaongea kama vile una uhakika,kuna internal auditors katika hizo taasisi,pia kuna vitengo vya pre audit ambavyo hukagua nyaraka kabla ya malipo...na lhizo case ni chache sana kiasi cha kuathiri mzunguko wa pesa
 
watu hawaspend money kwenye mzunguko, wengi wanafanya manunuzi ya msingi tu
Hakuna extra Money kwenye mzunguko

Umesema watu hawatumii pesa kwenye mzunguko balo wanafanya manunuzi ya msingi tu...

Well, iko hivi, kama huna hela za kijanja kijanja ni wazi hutazitumia bila busara zile za halali ulizonazo.

Hakuna pesa ya ziada kwa sababu mianya ya ufisadi imebanwa mbavu.
 
Nendeni vijijini kuona hali ilivyo ngumu tatizo la wengine mpo Dar mnakula tu kuku mtajuaje mtanzania anavyoteseka Mimi kawaida yangu naenda kule ndani kabisa vijijini ambapo wananchi wamesahaulika na serikali kama yule dogo wa mwanza alivyosema tangu atoke kijijini kuja mwanza mjini ndo ameanza kutambuliwa kama citizen wa hii nchi.
 
Katika jukwaa letu pendwa la Siasa kumeibuka mjadala kwamba NI HELA IPI IMEKUWA NGUMU?. Mjadala huu umeanzishwa na Nyani Ngabu akidai kwamba eti hakuna sababu za msingi kulalamika kupungua kwa vipato. Nakubaliana kuwa kulikuwa na watu waliokuwa wakitegemea ufisadi na rushwa katika kuendesha maisha yao. Lakini hata kwa wale waliokuwa wakitegemea kipato halali na kipato hicho hicho halali kimepungua. Tunaomba tuheshimiwe na mfumo urekebishwe.
Kuna baadhi ya hoja zinazodhibitisha kuwa vipato vyetu halali kimepungua.

Posho Stahiki kwa mujibu wa Sheria, Kanuni za Kudumu na Nyaraka

Kwa mujibu wa Sheria, Kanuni za Kudumu na Nyaraka watumishi wanazostahiki zao ambazo kwa sasa baadhi zimekuwa hazitolewi ama kwa wakati au kutokutolewa kabisa. Mfano:-
  • Ongezeko la Mshahara la Mwaka. Kwa mujibu wa mkataba wa ajira mshahara wa mtumishi wa umma unatakiwa kuongezeka kiasi Fulani kwa kila mwaka. Mantiki ya kufanya hivyo ilitokana na kuongezeka kwa gharama za maisha pindi mwaka mpya wa fedha unapoanza. Ngani Ngabu nijibu ni lini mshahara umeongezwa kwa 2016/17? Je, gharama za maisha zimepanda kiasi gani?Tukilalala kipato halali kimepunguzwa msituone wajinga.
  • Kanuni za kudumu zinatoa stahiki za kulipwa posho ya masaa ya ziada ambapo mda wakazi huisha saa 9.30 na kwa mfanyakazi atakeyafanya kazi zaidi ya hapo anatakiwa kulipwa posho ya masaa ya ziada kama fidia kwa mda ambao angekuwa anafanya shughuli binafsi. Leo hii wahasibu tunafunga hesabu za CAG mpaka saa4 usiku bila posho ya masaa ya ziada

Ujasiliamali

Watanzania wengi waliokuwa wakijishughulisha na ujasiriamali kipato chao kimepungua sana. Hii imesababishwa na biashara kuwa mbovu kutokana na kupungua kwa purchasing power. Wateja wengi wa wajasiriamali walikuwa ni watumishi wa umma ambao kipato chao cha halali walikuwa wakigawana na ndugu zao wasio na kazi. Mfano mimi nikipata kijiposho nawatumia wazazi, madogo,bibi yangu na hata machizi wangu katika kugawana umasikini. Ni vibanda vingapi vya ujasiriamali vimefungwa? Nao walikuwa wanavipata vya kifisadi?

Kilimo

Msimu wa mavuno ulikuwa mbaya sana kwa wakulima. Mfano sote tulishuhudia kwenye media kwamba wakulima wa nyanya na mbaazi walikula hasara. Serikali ilichofanya ni kukataza kuuza mazao nchi za majirani. Kipato cha wakulima hao kilikuwaje? Kilibaki kama kilivyo kipindi cha JK? Watu tumejitoa kulima matikiti tukilia taimingi Tanzania ya wiwanda vya Magufuli?Matikiti yanajiozea tu kwenye meza za masoko na mashambani.

Huduma za Afya

Tatizo hili limekuwepo toka enzi za JK. Huduma za afya ni mbovu sana, kuna upungufu mkubwa sana wa madawa muhimu katika hospitali za umma, vituo vya afya na zahanati. Kwa hiyo pamoja na kuwa na NHIF na CHF nalazimika kwenda kwenye duka binafsi kununua madawa kwa ajili yangu, mke ,watoto na wategemezi wangu wote. Ndugu zangu kule kijijini hawana kipato zaidi ya kuuza mazao najikuta nategemewa sana kusaidia pale ndugu anapopata shida ya kiafya.

Kupuuzwa kwa watumishi wa umma

Appreciation kwa mtumishi wa umma au mtumishi yeyote ni sawa na kumuongezea kipato. Nani hapendi heshima hata kama ni mfagizi.

Hakuna kipindi kigumu kama hiki kwa watumishi wa umma kama awamu hii. Watumishi tunadharauliwa sana na viongozi. Mheshimiwa raisi amekuwa na lugha mgumu sana kwetu.Tumekuwa tunaitwa majina ya ajabu ajabu yasiyo na heshima. Nataka kuamini hata kuchomwa kwa wenzetu kule Dodoma wakifanya kazi ya serikali ni zao la kupuunzwa. Watumishi wa afya wamekuwa wakitukanwa matusi ya nguoni na wateja. Nani anawapa kiburi hiki wananchi?

SWALI LA KIZUSHI

Nyani Ngabu kanunuliwa? Mbona alikuwa ana hoja makini kinzani dhidi ya mwenendo wa Serikali. Amekutana na Mzee Mwanakijiji huko Marikani ‘‘kalishwa sumu’’?

Itaendelea (to be continued)

Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?
 
serikali haina hela,vipaumbele vingi kutokana na ahadi za kampeni alizotoa na magu na ccm yake wameona bora kuwaumiza watumishi kwa kutowapa stahiki zao(kupandishwa vyeo,malimbikizo ya mishahara,likizo,posho ya uhamisho nk).Lakini wasichojua ni kuwa mwisho wa siku morali itapungua na matokeo yatakuwa mabaya sana.
..exactly..utawala huu wanacheza na bomu.....na bomu lenyewe ni mismanagement of human resource.....watu wanaminywa stahiki zao kwa kigezo cha uhakiki...lakini tayari dalili zinaonyesha kuwa issue ni kutokuwepo hela....Labda tuwakumbushe tu utawala huu kuwa....utawala uliopita walikopa kokote ili kulipa stahiki za watumishi.....naona utawala huu hili hawalioni....vitakavyoanza vilio vya watumishi halali nchi hii itakuwa ni issue endelevu...na hakutakua na hayo maendeleo wanayotambia majukwaani....
 
Ni kweli uchumi usio rasmi ulikuwa ni tegemeo kwa wengi hasa wapiga dili.

Pili kama ilivyoainishwa na baadhi ya wachangia hoja hapo juu watumishi wa serikali walikuwa wanafaidika na posho mbalimbali ambazo zilikuwa zinasukuma maisha ila serikali ikafuta nyingi ya hizo posho hivyo kufanya wengi kutegemea mshahara mwisho wa mwezi!!
Pamoja na hilo serikali imekata kabisa mtiririko wa pesa kutoka kwa watoa huduma mbalimbali mfano kumbi za mikutano, mahotel n.k (nyingi zikiwa ni sekta binafsi) kwa kisingizio cha kubana matumizi. Sekta binafsi imeajiri watu wengi sana hivyo chochote kinachotokea lazima (kiwe chanya au hasira) kitawaathiri wengi pia!

Kwa uhalisia maisha yetu ya kijamaa tunazungukwa na wategemezi wa kutosha.. , sasa pata picha mtu ni mwajiriwa wa serikalini (na pengine hana source ya kipato cha ziada) je kamshahara ka kima cha chizi katatosha kugawana na ndugu wategemezi?!

Hali imekuwa ngumu kwa maana ya kile kidogo kinachopatikana inalazimika kugawana na wategemezi
 
Hela imeadimika na ajira za baadhi ya watu zimeota mbawa hasa kwenye private sector. Watu wanaolalamika sana ni wale ambao wamepunguzwa kazi kutokana na sehemu zao za kazi kupunguza wafanyazi kwa sababu biashara imekuwa ngumu.
Ila kwa wale ambao bado wapo kazini wala hawapigi hizo kelele.

Wakulima pia walipiga sana kelele soko la bidhaa zao lilipotea so nadhani hata wao hela kwao imeadimika sijui kama walikuwa wanapiga magendo kwenye kilimo au nini kilitokea.
 
Mkuu nakubaliana kwa kweli kulikuwa na hela chafu sana mitaani ambazo hata Rais kasema zilikuwa za kutoka serikalini maanake Dar viwanja vilikuwa na bei zaidi ya New York au Hong Kong.

Mimi kama mdau wa usafirishaji....kweli hela imepotea kwa vile wateja wetu wengi walikuwa Zambia na DRC na wao hapa kati wamepunguza mno kutumia bandari yetu na kama unajua biashara ya usafirishaji kuna mtiririko na huo mtiririko umeathiriwa vilevile.

Kama wewe ni msafirishaji kweli kuna kitu ambacho wasafirishaji karibu nyote hamtaki kukisemea ukweli. Nacho ni wizi wa mali za wateja hasa shaba. Malori mangapi kutoka DRC na Zambia yamepoteza shaba yakiwa Tanzania? Ungekuwa wewe ni msafirishaji shaba ungeendelea kutumia hiyo njia? Hamtaki kusema ukweli na kushirikiana kukomesha tatizo sasa mnaathirika nyote.
 
Kwa muona wangu, ufisadi huongeza gharama za maisha. Yaani kwa walio wengi maisha huwa ni magumu. Sasa hii hoja ya kupunguza ufisadi na kuongezeka kwa ugumu wa maisha ni falsafa mpya kwangu.

Kwa watetezi wa uncle magu: kama jamaa kafaulu kudhibiti ufisadi, ilitakiwa tuwe tunafurahia maisha, sio kulalamikia ugumu wa maisha.
 
Well said. Hela ngumu kupatikana ni ile ya wizi, ujambazi, ufisadi na vitu vya namna hiyo.

Kwa miaka mingi kulikuwa na uchumi bandia Tanzania. Watu wanajenga au kununua magari ya gharama kubwa bila kuchukua mikopo bank.

Bila shaka sasa taratibu tunaanza kurudi kwenye uchumi halisi. Bei za viwanja zimeanza kupungua taratibu. Watu wanashindwa kulipa kodi za nyumba maeneo ya Sinza na kuamua kuhamia Mbagala (Ni mifano tu). Bei ya kupanga chumba maeneo kama Sinza itashuka kwa nguvu ya soko.

Kwa nchi za Ulaya, Utalia ilikuwa na uchumi bandia (madawa ya kulevya na rushwa). Sasa wanakiona cha moto.
 
Nendeni vijijini kuona hali ilivyo ngumu tatizo la wengine mpo Dar mnakula tu kuku mtajuaje mtanzania anavyoteseka Mimi kawaida yangu naenda kule ndani kabisa vijijini ambapo wananchi wamesahaulika na serikali kama yule dogo wa mwanza alivyosema tangu atoke kijijini kuja mwanza mjini ndo ameanza kutambuliwa kama citizen wa hii nchi.

Kwani ni lini huko vijijini hali ya maisha haikuwa ngumu?
 
Karibu kila kona siku hizi utasikia watu wanasema eti oh hela imekuwa ngumu kupatikana.

Sasa mimi nauliza, ni hela ipi hiyo ambayo imekuwa ngumu kupatikana tokea mheshimiwa MTUKUFU rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ashike madaraka?

Kama mtu ulikuwa unaishi kwa kutegemea kipato chako halali na bado unaendelea kukipata, huo ugumu unatokea wapi?

Au mshahara wako umepunguzwa tokea Magufuli ashike madaraka?

Mimi nadhani Watanzania tulilemazwa sana na uchumi wa kifisadi. Tuliuzoea na tukaukubali na kuufanya uwe sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.

Sasa huyu kamanda mpya alipoingia na kujaribu kuziba ziba mianya ya hizo pesa za kijanja kijanja ndo maana inaonekana kama vile pesa hakuna.

Lakini kwa vile ufisadi ulishakuwa sehemu [isiyo rasmi] ya uchumi wetu kwa kiasi kikubwa, kuzibwa kwa mianya ya upatikanaji wa hizo pesa haramu lazima kutaleta athari flani katika sekta mbalimbali ambazo naamini ni za mpito tu.

Uchumi wetu ulikuwa feki mno. Pesa walizokuwa nazo baadhi ya watu wachache zilikuwa haziendani kabisa na hali halisi ya uchumi wetu wa dunia ya tatu.

Kwa hiyo mimi sidhani kama hela iliyo halali imekuwa ngumu kupatikana. Labda uniambie hela ya kifisadi ndo imekuwa ngumu. Lakini si vinginevyo.

Je, wewe mdau wasemaje? Nimepotoka katika muono wangu?

=== Majibu===
Umenena vyema sana na huo ndio ukweli
 
Mimi sipendi kabisa hayo mambo ya utegemezi.

Ifike mahali watu tuwe wachoyo tu.
Uchoyo kibongobongo ni ngumu sana maana hatujafika level za kwa wenzetu huko ambako miaka 18 mtu tayari anajitegemea.
Kibongo bongo hata kaka mwenye familia anaona ni haki kusaidiwa pale anapokwama acha ndg watu wazima ambao ni jobless waliojazana majumbani mwetu!
 
Mkuu OKW BOBAN SUNZU , bandiko limevuta nichangie kidogo'tuhuma' dhidi ya Nyani Ngabu

Ni vema tuwe wakweli na kuyaangalia mambo kwa jicho pana hata kama hayatupendezi
NN kauliza, wanaosema pesa imepotea mitaani, imepotea vipi?

Ukweli: Pesa zilizagaa mitaani kwasababu ya madili.

Kulikuwa na trickle down effect,wapiga dili wana effect kuanzia muuza bar, fundi mwashi, mjenzi, karani n.k. Kuziba mianya kume affect wapigaji to the receiving end

Madili hayajengi uchumi thabiti. Ni mfumo usio rasmi tuliokubali bila kujua madhara yake
Inflation na ongezeko la kodi ni kwasababu ya wachache kuchota na wengi kubeba mzigo

Wao wanapochukua mchele, nasi tukafurahia magunia ya pumba kwavile tunaokota punje za mchele, it doesn't make sense. In the end tunarudi kubeba mzigo mkubwa wa kodi

Watumishi: Kuishi kwa posho za mikutano si sehemu ni ujanja ujanja tu kama wa madili.
Kwa inter. orga na nchi za wenzetu, mtumishi akiwa semina ni sehemu ya kazi ya siku

Mtumishi akisafiri anapewe malazi, usafiri n.k.posho zipo nchi zetu wenzetu hawana hilo

Ni ukweli unaoudhi lakini ndio ukweli.

Tunapoondoa watumishi hewa, tukawa na semina feki ni kujaza maji ndoo inayovuja.

Ni dili kama zile za wapigaji ingawa hii ni haramu inayovumilika.

Purchasing power:
Umegusia hilo,unapodhibiti inflation , unaongeza purchasing power in a way

Purchasing power ni nguvu ya pesa kununua na si wingi wa fedha za kununulia.
Ndiyo maana nchi nyingine hadi sasa wanatumia ''senti' kwasababu ina nguvu.

Huduma za afya: Kuzorota ni priority kwa serikali na si kwasababu ya fedha
Tunapojenga daraja badala ya hospitali, tatizo ni priority

Kwa uchache, hatua za kubana pesa haram zimelenga kutengeneza uchumi.
Ni kali kwa sasa mbele ya safari ni nzuri, tutakuwa na uchumi na si uchumi usio rasmi

Kama tunakubaliana ufisadi una madhara, hatuwezi kukataa matokeo ya kudhibiti hali hiyo

Zimbwabwe ikipata uhuru $1 USD ilikuwa sawa na ZM$2.5 .
Leo $1 ni sawa na 200,000 ZM, je kuna afadhali yoyote? Ndiko tunakotaka twende?
 
Back
Top Bottom