Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Hivi we mshikaji hunaga hoja ingine juu yangu zaidi ya kuniambia nirudi kwetu?
Achana na huyu mbega,ni dhana potofu ugumu wa fedha ni kwenye noti laini za jero zimefanywa ngumu baada kubadilishwa kuwa coins huo ndo ugumu.
 
Karibu kila kona siku hizi utasikia watu wanasema eti oh hela imekuwa ngumu kupatikana.

Sasa mimi nauliza, ni hela ipi hiyo ambayo imekuwa ngumu kupatikana tokea mheshimiwa MTUKUFU rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ashike madaraka?

Kama mtu ulikuwa unaishi kwa kutegemea kipato chako halali na bado unaendelea kukipata, huo ugumu unatokea wapi?

Au mshahara wako umepunguzwa tokea Magufuli ashike madaraka?

Mimi nadhani Watanzania tulilemazwa sana na uchumi wa kifisadi. Tuliuzoea na tukaukubali na kuufanya uwe sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.

Sasa huyu kamanda mpya alipoingia na kujaribu kuziba ziba mianya ya hizo pesa za kijanja kijanja ndo maana inaonekana kama vile pesa hakuna.

Lakini kwa vile ufisadi ulishakuwa sehemu [isiyo rasmi] ya uchumi wetu kwa kiasi kikubwa, kuzibwa kwa mianya ya upatikanaji wa hizo pesa haramu lazima kutaleta athari flani katika sekta mbalimbali ambazo naamini ni za mpito tu.

Uchumi wetu ulikuwa feki mno. Pesa walizokuwa nazo baadhi ya watu wachache zilikuwa haziendani kabisa na hali halisi ya uchumi wetu wa dunia ya tatu.

Kwa hiyo mimi sidhani kama hela iliyo halali imekuwa ngumu kupatikana. Labda uniambie hela ya kifisadi ndo imekuwa ngumu. Lakini si vinginevyo.

Je, wewe mdau wasemaje? Nimepotoka katika muono wangu?
Upo sahihi kabisa
 
Nyerere aliwahi kusema, "Nchi hii ni ya wakulima na wafanyakazi ambao ni masikini, nchi hii haijawa ya matajiri" Uchumi wa kuishi kimjini mjini ulifanya watu wabweteke sana na kuona ndiyo maendeleo.
Maendeleo ya kweli huletwa na uzalishaji sasa wabongo tulizoea uchumi usiozalisha (fiat money economy).
 
Ngoja kwanza watanzania wajefunze maisha halisi kipindi hiki wanayo takakiwa kuishi sio kuishi kwa ujanja ujanja .

Wewe uliwahi kuwona wapi Dunia ya leo watu wanalipa KODI YA NYUMBA kwa mwaka mzima zaid ya Tanzania ...,uliwahi kuona wapi Manunuzi iwe nyumba ,
Au gari za bei kubwa watu wananunu kwa CASH ni Tanzania ...uliwahi kuona wapi manunuz ya nyumba au kodi walio wengi wanataka DOLA baadala ya shiling zaid ya TANZANIA .

Hapo lazima kuna matatizo sio bure.
 
Unapozungumzia hela ya kifisadi unamaanisha mabilioni ya matajiri tu? au unamaanisha mpk hela kwa wauza maduka na hela za wakulima baada ya kuuza mazao yao

Ufisadi ulishakuwa sehemu kubwa ya uchumi kiasi kwamba watu wengi walikuwa wananufaika nao kwa namna ya moja kwa moja ama nyinginr.
 
ivi hela haipatikani kivipi??yaan kuna mtu kaipeleka mbinguni au??..unakuta mwalimu naye anasema hela imekuwa ngumu wakati mshahara wake ndo ule ule...................

Ekzaktli!
 
Pesa za kijanja ziliwafanya watu wasiwe na nidhani ya kuzitunza.

Watu walikuwa wana spend with reckless abandon.

Sasa mambo yamebadilika.

Kuna watu imebidi hadi wauze magari yao ya kifahari, wengine imewabidi wawahamishe shule watoto wao, na kadhalika.
umeruka hoja yako sasa unasema pesa za kijanja hiyo nafasi uliyopo ungempa mtu mwingine qkaitumia ladba angesaidia watanzania 2-5.

swissme
 
Ngoja kwanza watanzania wajefunze maisha halisi kipindi hiki wanayo takakiwa kuishi sio kuishi kwa ujanja ujanja .

Wewe uliwahi kuwona wapi Dunia ya leo watu wanalipa KODI YA NYUMBA kwa mwaka mzima zaid ya Tanzania ...,uliwahi kuona wapi Manunuzi iwe nyumba ,
Au gari za bei kubwa watu wananunu kwa CASH ni Tanzania ...uliwahi kuona wapi manunuz ya nyumba au kodi walio wengi wanataka DOLA baadala ya shiling zaid ya TANZANIA .

Hapo lazima kuna matatizo sio bure.

Hebu longa na wewe!

Kuna baadhi ya nyumba niliwahi kuona zinauzwa huku Mbezi beach. Moja ilikuwa ni dola milioni moja na ushee ingine milioni 2.

Nyumba zenyewe ukiziangalia halafu ukizilinganisha na million dollar homes za huko kwa hao wenye dola, unaona kabisa kuna kitu huku kwetu hakiko sawa.

Million dollar home gani iko surrounded na takataka, madimbwi, makorongo, na mifereji ya maji machafu yaliyotuama?

Ni uendawazimu kabisa huo.
 
Kuondolewa kwa posho za semina, mambo ya salary increment, kuongezeka kwa umakini kwenye taasisi za umma kama TRA, TPA, kumefamya watu waseme pesa imekuwa ngumu.

Kukosekana kwa masoko ya mazao, ukosefu wa ajira za serekali,kubana matumizi ya serekali, kumefanya watu waseme pesa imekuwa ngumu.

Kwa mtazamo wangu nadhani mabadiliko ya kiuongozi yatasababisha mabadiliko ya sura ya uchumi.Wakati wa JK ilikuwepo dhana ya 'maisha magumu', sasa ni pesa imepotea....baadhi ya watu wanapokea kauli na kuzikuza bila kuangalia uhalisia wake.
Utamkuta mtu maisha yake yapo steady kama miaka ya nyuma ila naye anaimba pesa imepotea.
 
Ufisadi ulishakuwa sehemu kubwa ya uchumi kiasi kwamba watu wengi walikuwa wananufaika nao kwa namna ya moja kwa moja ama nyinginr.
Nimekuelewa mkuu, upo sahihi.
Uzi wako hukuufafanua vizuri vipengele vingi ndo maana kuna jenga maswali mengi. Hasa kwenye uchumi
 
Karibu kila kona siku hizi utasikia watu wanasema eti oh hela imekuwa ngumu kupatikana.

Sasa mimi nauliza, ni hela ipi hiyo ambayo imekuwa ngumu kupatikana tokea mheshimiwa MTUKUFU rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ashike madaraka?

Kama mtu ulikuwa unaishi kwa kutegemea kipato chako halali na bado unaendelea kukipata, huo ugumu unatokea wapi?

je, wewe mdau wasemaje? Nimepotoka katika muono wangu?

Mkuu nakubaliana kwa kweli kulikuwa na hela chafu sana mitaani ambazo hata Rais kasema zilikuwa za kutoka serikalini maanake Dar viwanja vilikuwa na bei zaidi ya New York au Hong Kong.

Mimi kama mdau wa usafirishaji....kweli hela imepotea kwa vile wateja wetu wengi walikuwa Zambia na DRC na wao hapa kati wamepunguza mno kutumia bandari yetu na kama unajua biashara ya usafirishaji kuna mtiririko na huo mtiririko umeathiriwa vilevile.
 
Kuondolewa kwa posho za semina, mambo ya salary increment, kuongezeka kwa umakini kwenye taasisi za umma kama TRA, TPA, kumefamya watu waseme pesa imekuwa ngumu.

Kukosekana kwa masoko ya mazao, ukosefu wa ajira za serekali,kubana matumizi ya serekali, kumefanya watu waseme pesa imekuwa ngumu.

Kwa mtazamo wangu nadhani mabadiliko ya kiuongozi yatasababisha mabadiliko ya sura ya uchumi.Wakati wa JK ilikuwepo dhana ya 'maisha magumu', sasa ni pesa imepotea....baadhi ya watu wanapokea kauli na kuzikuza bila kuangalia uhalisia wake.
Utamkuta mtu maisha yake yapo steady kama miaka ya nyuma ila naye anaimba pesa imepotea.

Watu waliokuwa wamezoea vi trip vya majuu na kupiga per diems lazima walie.

Mazoea huwa ni mabaya sana.
 
Back
Top Bottom