kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,189
- 16,867
Kazi yangu mimi ni biashara ya genge, nauza mboga. Nilichogundua hapa kijijini kwetu ukiona noti mpya nyingi zinakuja gengeni kununua bidhaa ujue watumishi wamelipwa misharaha yao. Wingi wa hela hizi nyingi na mpya unapotea ndani ya siku 7 hadi kumi tu. Nikamuuliza mwenzangu anaemiliki glossary ya vinywaji nae akamiambia hivyohivyo huko kwake.
Tulipojiuliza hii inatokana na nini tukagundua kuwa pesa nyingi za muda wote huku vijijini zinaletwa na wafanyakazi kama maji kubwa na maji kujaa kila mwezi. Hela nyingine zinakuja wakati wa msimu wa mavuno watu wanapouza mazao yao ya msimu kwa mwaka mara moja. Pesa za uhakika za angalau kila mwezi ni pesa za watumishi vijijini wanapolipwa mishahara yao na wafugaji kidogo wanapouza mifugo yao mara moja moja.
Tulichogundua ni kwamba mishahara ya watumishi wengi inawatosha kufanya manunuzi angalau kwa siku 7 hadi 10 tu, siku 20 zilizobakia hawana uhakika wataishije bila pesa. Hapo ndiyo dhana ya usawa wa kamba inapojitokeza. Ili uweze kuwa na kamba ndefu lazima uwe chawa wa kiongozi wako ili akupatie safari, nafasi, kazi au overtime zenye malipo ili upate fedha ya kuliziba pengo la siku 20. Katika kipindi hichi chote cha siku 20 kazi na huduma za umma zitazorota kwasababu mtumishi hana morali anawaza afanye nini apatiwe safari, semina, kusimamia au kazi yoyote yenye malipo ya ziada.
Mbinu zinazotumia kwenye uchawa ni pamoja na kuwapiga "shoti" wafanyakazi wenzako, kumsifia sana boss, kuleta zawadi kwa boss unapopewa safari, nafasi au kuhudhuria semina ili akupatie tena safari nyingine wakati mwingine; yaani safari na semina na kusimamia upewe wewe kila wakati fursa zinapojitokeza. Utapeleka umbeya kwa bosi, utamuandika vizuri yeye na kampuni/taasisi yake hata kama yeye na taasisi yake hawako vizuri. Unavizia uteuzi all the time.
Kama tunataka huduma kwa wananchi ziboreke, tusijidanganye, tuwalipe vizuri watumishi ili wabaki kazini siku zote 30 wanahudumia wananchi, pili, mishahara mikubwa inachechemua uchumi kwakuwa inawapa watumishi uwezo mkubwa wa kufanya manunuzi. Watanunua kwa wingi na kutumia mazao ya wakulima, wafugaji na bidhaa za viwandani.
Nchi zote zenye uchumi mkubwa zinawalipa vizuri watumishi, wakulima na wafugaji. Hawa wakilipwa vizuri wataenda kulipa kununua na kutumia bidhaa za viwandani kama cement, kulipa kazi za wasanii na michezo kama mpira wa miguu, nk. Bila hivyo hata AFCON hapa tutatia aibu watu hawataweza kugharimia kuingia viwanjani; they have no money, lower purchasing power everywhere.
Mama fikiria kuongeza kibunda kwa watumishi kama unataka huduma bora kwa raia wako na uchumi upae kama mwewe. Hata Dangote anajua purchasing power ya watanzania iko chini sana, ndio maana ameshawishika kujenga refining yake Kenya. Mtumishi wa kenya analipwa vizuri kuliko mtumishi wa tz kwa kazi hiyohiyo hali iliyosababisha wakenya wazaje viwanja wakati wa CHAN kuliko tz.