Mawazo ya hovyo kabisa haya! Mawazo ya hovyo hovyo ambayo yalizoeleka kusikika toka kwenye kambi fulani lakini yameambukizwa haata kwa kwa wengine! Tuchukue mfano mdogo sana!! Serikali ime-impose VAT kwa Mawakala wa Forodha... by Rule of Thumb, nao waka-pass VAT to Foreign Importers! Gharama kwa Foreign Importers zikaongezeka na solution kwao ikawa ni kuikimbia bandari!Kiukweli wanaolialia ni wale waliozoea hela za dezo na za ofa......yaani wale ambao walizoea kuishi kiujanja ujanja.....
Hii lazima iwe ni kama kiama kwao......wala hujapotoka ndugu upo sahihi.....!!!
Kutokana na kuikimbia bandari... wenye malori wakakosa mizigo, madereva na matingo wakakosa kazi, Wabeba mizigo mgongoni wakakosa vibarua, soko la Mama Lishe linalotokana na madereva, makonda na wabeba mizigo likapungua! Huyu Mama Lishe kama alikuwa ananunua Mchele kilo 10 toka kwa Mangi au Mpemba akalazimika kununua kilo 5, badala ya kununua sukari kilo 3 analazimika kununua kilo 1, badala ya kununua unga kilo 10 ananunua kilo 6... msululu ni mrefu!
Hivi kweli kabisa unaamini hao watu walikuwa wanaishi kiujanja ujanja na ndio maana siku hizi wanalalamika? Serious? Kabisa unaamini walikuwa wanakula pesa za dezo hao?! Hivi kabisa unaamini wale mafisadi ambao kweli walikuwa wanainyonya hii nchi leo hii ni miongoni mwa wanaolalamika kupotea pesa?! Hivi kweli kabisa unaaamini wale ambao walitorosha makontena na baadae wakaambiwa walipe tu mambo yaishe ndio wanaolalamikia kupotea kwa pesa?! Hivi mtu ambae kwake 10 Million aliita ni pesa ya mboga unaamini kabisa anahisi kupotea pesa?! Hivi kabisa unaamini watoto wa Masamaki yule Kamishina wa TRA ni miongoni mwa hawa wanaolalamika kwamba hali ngumu... do you really believe that?