Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Tufanye mimi sio muungwana lakini na wewe unaonekana sio mstahimilivu wa mawazo huru ya wenzako... kwa sababu ikiwa naamini mawazo uliyotoa ni ya hovyo basi nina uhuru wa kuweka wazi hapa na unapohoji uungwana wangu hapo, bado unatia shaka ikiwa kweli unaamini katika mawazo huru!

...........uwe na wakati mwema ndugu yangu....
 
Wote mnaoshabikia uzi huu ni walebl mlioajiliwa tu.wafanyabiashara tuanelewa maana ya hela kuwa ngumu.mfano mimi nina hardware yangu ambayo kabla ya magufuri nilikuwa nauza kwa siku hadi million 3 ,ila kwa sasa unakuta nafunga laki 6 na kwa tabu hadi nimepunguza mfanyakazi mmoja,ukija pale kwenye bar,jikoni nilikodi niuze supu na mbuzi,mwanzo nilikuwa nauza hadi mbuzi wanne ila kwa sasa mbuzi mmoja akiisha basi nashukuru,sasa tunaposema mambo ni magumu mnatakiwa kuelewa jamani,
 
Mjadala ulikuwa mzuri sana, ila naona jazba inatawala. Mkuu chige rudisha moyo, tuongee jamvini
Tafadhali muungwana, maana lengo ni kufunguana mawazo

Nina swali moja, iliunafuu na hali iwe na ahueni, unashauri vipi?

Nikisoma hoja zako inaonekana una hoja na sababu zako, sasa tusaidie kidogo unadhani nini kingefanyika, nini kimefanyika tofauti na siku zilizopita?
 
Well, umeeleza vema. Tunajua pia hakujatokea maafa yakaua watu kwa kiasi cha kutisha. Wateja wako wapo pale pale. Ni kwanini hawatumii kama walivyokuwa wanatumia siku za nyuma?
 
Unaifahamu multiplier effect. Pinda alivyosema kwamba ukideal na hawa watu lazima wakuyumbishe na inawezekana sio kundi kubwa la watu wanaweza wakawa ishirini tu Tanzania lakini kukatiwa kwao channels kunaweza kukawa kuna impact kwa watu hata maelfu kwa malaki..Kwa hiyo unaweza ukawa ulikuwa unajitafutia kibpato kihalali lakini hizo hela ambazo ulikuwa unazipata kihalali zinaweza zikawa results ya multiplier effect ya watu wachache waliopo juu ambao wanafanya michongo haramu. Tufanye kuna wati ishirini wanato rushwa ya bilioni 20 ili mizigo yao iingie bila kodi labda ya bilioni 100. Zile bilioni 20 za mpokea rushwa zinaingia kwenye black market maana ni fedha haramu lazima uhakikishe haziwi traced. Anafika mtu mtaani anaamua kujenga nyumba zaidi ya mia moja ina maana hapo kuna mafundi kibao watapata ajira. Hao mafundi wanatafuta kipato cha halali lakini hela watayolipwa imepatikana kwa njia ya haramu. Mafundi watachukua zile hela na kwenda kutumia huko mtaani kwao . Kwa hile hela inaenda ikizida kujigawanya kushuka chini lakini origin yake ni moja. Kwa ikitokea siku ukawabana hao watu wanaingiza b 20 haramu kwenye mzunguko mzunguko basi effect yake itaenda mpaka chini kwa kufuata hiyo chain niliyotolea mfano..Wanasema ukitaka kumuua nyoka mkate kichwaa. Umeelewa? Kwa hiyo ni kweli hela imeadimika sababu black market haina supply ya hela kwa karibu mwaka sasa...teh teh teh
Black market - Wikipedia, the free encyclopedia
Mkuu umeeleza vizuri na umethibitisha kwamba msemo kuwa hela imepotea ni sahihi. na kwamba si kwa vile wanaopokea mshahara wanaendelea kupokea!
Kilichopo ni kufikiri upya nn cha kufanya. labda diversification ya shughuli za uchumi mfano fundi ujenzi anaweza kuwa na kabustani mahali au akafuga japo vikuku vya kienyeji n.k. nk. basically tufanye kazi zaidi na iwe hapa kazi na kazi halali tu!
 
Exactly mkuu...You can say it again...Ni muda umefika watu kuwa creative. Kuna vitu hata uchumi uwe vipi haviwezi kosa soko...
 
Wote mnaoshabikia uzi huu ni walebl mlioajiliwa tu.wafanyabiashara tuanelewa maana ya hela kuwa ngumu.mfano mimi nina hardware yangu ambayo kabla ya magufuri nilikuwa nauza kwa siku hadi million 3 ,ila kwa sasa unakuta nafunga laki 6 na kwa tabu hadi nimepunguza mfanyakazi mmoja,ukija pale kwenye bar,jikoni nilikodi niuze supu na mbuzi,mwanzo nilikuwa nauza hadi mbuzi wanne ila kwa sasa mbuzi mmoja akiisha basi nashukuru,sasa tunaposema mambo ni magumu mnatakiwa kuelewa jamani,
Soma post yangu hapo juuu naona hamtaki kufikiri nje ya box. Hela imepungua kweli ila mnapaswa kujiuliza why?
 
Soma post yangu hapo juuu naona hamtaki kufikiri nje ya box. Hela imepungua kweli ila mnapaswa kujiuliza why?
Hili swali nimeuliza sana
Ikiwa wateja ni wale wale wakiwa wameajiriwa kule kule, nini hasa kimetokea hawatumii tena pesa?

Na wanaosema hakuna pesa, wanashauri nini kifanyike irudi mtaani?

Niliowauliza wamekimbia, mbele ya safari wataibuka tena pesa hakuna
 
Mawazo ya hovyo kabisa haya! Mawazo ya hovyo hovyo ambayo yalizoeleka kusikika toka kwenye kambi fulani lakini yameambukizwa haata kwa kwa wengine! Tuchukue mfano mdogo sana!! Serikali ime-impose VAT kwa Mawakala wa Forodha... by Rule of Thumb, nao waka-pass VAT to Foreign Importers! Gharama kwa Foreign Importers zikaongezeka na solution kwao ikawa ni kuikimbia bandari!

Kutokana na kuikimbia bandari... wenye malori wakakosa mizigo, madereva na matingo wakakosa kazi, Wabeba mizigo mgongoni wakakosa vibarua, soko la Mama Lishe linalotokana na madereva, makonda na wabeba mizigo likapungua! Huyu Mama Lishe kama alikuwa ananunua Mchele kilo 10 toka kwa Mangi au Mpemba akalazimika kununua kilo 5, badala ya kununua sukari kilo 3 analazimika kununua kilo 1, badala ya kununua unga kilo 10 ananunua kilo 6... msululu ni mrefu!

Hivi kweli kabisa unaamini hao watu walikuwa wanaishi kiujanja ujanja na ndio maana siku hizi wanalalamika? Serious? Kabisa unaamini walikuwa wanakula pesa za dezo hao?! Hivi kabisa unaamini wale mafisadi ambao kweli walikuwa wanainyonya hii nchi leo hii ni miongoni mwa wanaolalamika kupotea pesa?! Hivi kweli kabisa unaaamini wale ambao walitorosha makontena na baadae wakaambiwa walipe tu mambo yaishe ndio wanaolalamikia kupotea kwa pesa?! Hivi mtu ambae kwake 10 Million aliita ni pesa ya mboga unaamini kabisa anahisi kupotea pesa?! Hivi kabisa unaamini watoto wa Masamaki yule Kamishina wa TRA ni miongoni mwa hawa wanaolalamika kwamba hali ngumu... do you really believe that?
Huo ni upande mmoja wa shilingi, vipi kuhusu meli 60 hewa ambazo watu walikuwa anapiga kiulaini?. Vipi kuhusu wingi wa ICDs ambao tija yake haionekani?.
Ugumu wa maisha huumiza wengi lakini lengo likiwa ni wengi kufaidika na utajiri wa taifa, basi uwepo wa ugumu huo ni suala la muda tu.
 
Mjadala ulikuwa mzuri sana, ila naona jazba inatawala. Mkuu chige rudisha moyo, tuongee jamvini
Tafadhali muungwana, maana lengo ni kufunguana mawazo

Nina swali moja, iliunafuu na hali iwe na ahueni, unashauri vipi?

Nikisoma hoja zako inaonekana una hoja na sababu zako, sasa tusaidie kidogo unadhani nini kingefanyika, nini kimefanyika tofauti na siku zilizopita?
Kwanza siwezi kukejeli yanayofanywa na JPM hata kidogo... in short, mengi nayaunga mkono!

Nikirudi kwenye swali lako... tusisahau ili uchumi tuite uchumi basi inabidi kuwe na development of both, macroeconomic and microeconomics! Hii microeconomics part of economy ndio more challenging part kwa sababu ndio inashikilia uchumi wa watu wengi! Abuse kwenye microeconomics development ndiyo inasababisha kukuta nchi ina very big GDP, very big GDP per capita lakini maisha ya watu yapo duni kwa sababu kuna abuse ya microeconomic development! It's fine... una-impose VAT kwa Mawakala wa Forodha na sio kwa Goods in Transit kama ilivyokuwa inasemwa! Lakini mtu haihitaji kuwa mchumi au mtaalamu wa masuala ya kodi kufahamu kwamba hiyo tax burden ya VAT itakuwa transferred to Importers ambao nao wana choice! Kiuchumi, huwezi kupandishwa kodi hovyo hovyo kwa bidhaa yenye close substitutes! Bidhaa ya importers hapa ni bandari... na close substitutes hapa ni chain of ports available in various countries! Sasa penye umakini, badala ya ku-discourage importers/exporters kwa ku-impose kodi, unatakiwa ku-encourage hata ikibidi kwa kuondoa kodi zisizo na impact kubwa kiuchumi! Ukifanya hivi, utavutia watumiaji wengi zaidi wa bandari, watakaosababisha mahitaji makubwa ya magari ya usafirishaji, ambayo nayo yatahitaji mafuta mengi na wafanyakazi wengi zaidi, yatakayo-encourage kuongezeka kwa vituo vya mafuta vingi zaidi, vitakavyozalisha ajira nyingi zaidi ambayo yote hayo net outcome ni development of microeconomic enterprises itakayoongeza money circulation in the economy ambayo leo tunataka kuaminishwa kwamba, ukiona money circulation in the economy ni kubwa basi huo ni ufisadi!!!

Tumia mfano kama huo kwenye sekta zingine kama vile utalii! Hapa tukaambiwa hatuna haja ya waralii maskini! Yaani watawala wanasahau au hawajui kwamba ni hawa watalii maskini ndio wateja wakubwa wa local products! Kutokana na umaskini wake atalazimika afikie 4 Star Hotel ambayo possibly itakuwa inamilikiwa na Mtanzania! Huyu mwenye 4 Star Hotel akipaata watalii maskini wengi zaidi ndipo atakavyoweza kuongeza hotel ya pili na ya tatu na ya nne! Hapo si tu kwamba atachangia macroeconomic sector kwa kulipa kodi na kutoa ajira, lakini pia atachangia ukuaji wa microeconomic sector kv ataongeza hoteli ya pili, ya tatu n.k... ataongeza ununuzi wa vyakula, mboga n.k kwavile ana watalii maskini wengi zaidi! Lakini VAT inasababisha watalii masikini wasije, matokeo yake yule mwenye 4 Star Hotel anakosa wateja halafu akilalamika kwamba wateja wamepungua anaambiwa alikuwa anategemea biashara za kiujanja ujanja... wapi na wapi?! Matokeo yake tunapata hao waatalii matajiri wanaotakiwa... ambao majority wataingia na kuondoka bila kuonja japo mahindi ya pale posta ambayo Watalii maskini wanayanunua kila leo... muuza mahindi hapa akisema biashara imepungua kwa sababu wamekuja watalii classic ni sahihi kusema alizoea biashara za ujanja ujanja?! Watafika na kufikia hoteli za akina Agha Khan pale Serena ambae, ambae si ajabu nyanya na vitunguu anatoa South Africa na kuku anatoa Brazil!! Sasa mfugaji wa kuku akisema biashara imedorora sana kwa sababu wenye mahoteli yanayobeba watalii masikini biashara kwao imepungua... ni sahihi kusema huyu muuza kuku analalamika kwavile alikuwa anafanya biashara za kiujanja ujanja?!

Mbaya zaidi tunasahau kwamba waneemeka wa ufisadi nchi hii ni wachache sana na mafisadi hawa wala sio wateja wa wale wanaolalamika! Ni fisadi wa wapi nchi hii anaenda Soko la Stereo Temeke kununua nyanya? Ni fisadi wa wapi nchi hii anaenda Kariakoo au Mchikichini au Manzese kununua nguo?! Hivi ni kweli hawa wa Mchikichini ambao wateja wao walikuwa madereva na makonda wa malori na sasa hawaonekani tena kwa sababu VAT on Mawakala wa Forodha imewaondolea chanzo chao cha kipato?!

Kwahiyo, kukujibu swali lako kwa maneno machache ni kwamba serikali iache ku-abuse the development of microeconomic enterprises! Hakuna uhusiano wowote kati ya ufisadi na ukuaji wa fursa za kiuchumi! Uchumi usiozingatia ukuaji wa fursa za kiuchumi ni uchumi usio na maana yoyote ile... tutaishia kushangilia growth rate ya 10% lakini multiplier effect haionekani!
 
Huo ni upande mmoja wa shilingi, vipi kuhusu meli 60 hewa ambazo watu walikuwa anapiga kiulaini?. Vipi kuhusu wingi wa ICDs ambao tija yake haionekani?.
Ugumu wa maisha huumiza wengi lakini lengo likiwa ni wengi kufaidika na utajiri wa taifa, basi uwepo wa ugumu huo ni suala la muda tu.
Ndo tatizo lenu... unataka kusema hizo meli hewa zilikuwepo kwavile hapakuwa na hiyo VAT?Kuna uhusiano gani kati ya VAT na meli hewa?! By the way, hebu niambie hapa hao wenye ICD zisizo na tija ambazo tumeambiwa walikuwa wanatorosha makontena... hadi leo wamefanywa nini?! Si tuliambiwa Bakhresa ni mmoja wa hao wenye ICDs zisizo na tija!! Inakauwaje tena mtu anayeitia hasara serikali leo hii rais anatoa big favor kwake?
 
Mbaya zaidi tunasahau kwamba waneemeka wa ufisadi nchi hii ni wachache sana na mafisadi hawa wala sio wateja wa wale wanaolalamika
Wanaeemeka walikua wengi sana... Maana fisadi alikua akipiga sehemu labda anaenda bar, hotel au kariakoo.. Kununua bidhaa au anajenga majumba.. Ambayo Kuna mafundi watalipwa n.k
 
Ndo tatizo lenu... unataka kusema hizo meli hewa zilikuwepo kwavile hapakuwa na hiyo VAT?Kuna uhusiano gani kati ya VAT na meli hewa?! By the way, hebu niambie hapa hao wenye ICD zisizo na tija ambazo tumeambiwa walikuwa wanatorosha makontena... hadi leo wamefanywa nini?! Si tuliambiwa Bakhresa ni mmoja wa hao wenye ICDs zisizo na tija!! Inakauwaje tena mtu anayeitia hasara serikali leo hii rais anatoa big favor kwake?
Naongelea upigaji bandarini in general. Kusema wamefanywa nini wakati unajua kesi zao zipo kwenye hatua mbalimbali ni kujitoa ufahamu bila ya sababu. Bakhresa bidhaa zake zilizuiliwa kwa sababu ya issue za kodi mbalimbali.
Kulipa kodi ni suala moja, wafanyabiashara hao hao wanaolipa kodi, kuweza kupatiwa ushirikiano na serikali ni suala jingine.
 
Pesa za kijanja ziliwafanya watu wasiwe na nidhani ya kuzitunza.

Watu walikuwa wana spend with reckless abandon.

Sasa mambo yamebadilika.

Kuna watu imebidi hadi wauze magari yao ya kifahari, wengine imewabidi wawahamishe shule watoto wao, na kadhalika.
mbona hueleweki sasa?
 
Back
Top Bottom