Karibu kila kona siku hizi utasikia watu wanasema eti oh hela imekuwa ngumu kupatikana.
Sasa mimi nauliza, ni hela ipi hiyo ambayo imekuwa ngumu kupatikana tokea mheshimiwa MTUKUFU rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ashike madaraka?
Kama mtu ulikuwa unaishi kwa kutegemea kipato chako halali na bado unaendelea kukipata, huo ugumu unatokea wapi?
Au mshahara wako umepunguzwa tokea Magufuli ashike madaraka?
Mimi nadhani Watanzania tulilemazwa sana na uchumi wa kifisadi. Tuliuzoea na tukaukubali na kuufanya uwe sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.
Sasa huyu kamanda mpya alipoingia na kujaribu kuziba ziba mianya ya hizo pesa za kijanja kijanja ndo maana inaonekana kama vile pesa hakuna.
Lakini kwa vile ufisadi ulishakuwa sehemu [isiyo rasmi] ya uchumi wetu kwa kiasi kikubwa, kuzibwa kwa mianya ya upatikanaji wa hizo pesa haramu lazima kutaleta athari flani katika sekta mbalimbali ambazo naamini ni za mpito tu.
Uchumi wetu ulikuwa feki mno. Pesa walizokuwa nazo baadhi ya watu wachache zilikuwa haziendani kabisa na hali halisi ya uchumi wetu wa dunia ya tatu.
Kwa hiyo mimi sidhani kama hela iliyo halali imekuwa ngumu kupatikana. Labda uniambie hela ya kifisadi ndo imekuwa ngumu. Lakini si vinginevyo.
Je, wewe mdau wasemaje? Nimepotoka katika muono wangu?