Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Ni hela ipi ndo imekuwa ngumu?

Nyani Ngabu we ni double agent??? Nakumbuka kuna uzi ulileta hapa ukiwa unamponda Magufuli kwa kuwakataza wapinzani kufanya mikutano...and here you are again!!!

Mimi sio zumbukuku wa kupongeza tu hata mambo yaliyo ya kipu.mbavu, yasiyo na tija, na yanayoturudisha nyuma.

Kwenye kukemea na kulaani nitafanya hivyo na penye kupongeza na kuunga mkono nitafanya hivyo.

Siangalii sura, itikadi, wala kadi ya chama. Naangalia tija tu.

Niko huru.
 
We baba mkaa ndani toka nje usikie kuna habari inavuma vuma vuma kama uko USA ya huku tuachie
 
Mkuu,kuna binamu yangu yupo tfda,kuna siku wakati nasubiri matokeo yangu ya chuo mwaka jana,huku nikiwa arosto for days,aliniambia kwa week mbili nisiende popote!nikamuuliza,why?akanijibu kuna semina ya NGO Mmoja ya Uholanzi iliyokuwa inadili na Utafiti na Uboreshaji wa Ulaji wa Chakula cha Asili(organic foodstuffs)!sasa,nikamuuliza tena mie nimesomea beekeeping,mambo ya drugs and food nayawezea wapi!akaniambia wewe utajifanya ni waiter kwenye hotel tunamofanyia semina,na kila siku for the next two weeks utalipwa na serikali 200k!
Na hapo sijajua kama alinichakachua!
.....
......Njoo London utumikie fani wafuga Nyuki ni sponsa wa Manchesta Unitedi
 
Hilo la safari zisizo na mbele wala nyuma watu tumelipigia kelele sana humu.

JK alikuwa akisafiri anaambatana na rundo la watu.

Sasa piga picha jamaa alivyokuwa mtu wa trips za nje hususan Marekani.

Nahisi kuna watu walikuwa hata hawaigusi mishahara yao kabisa.
indeed hapa tulikuwa tunahesabu safari zake sasa imagine mtu ndani ya miaka 10 katumia miaka 2 nje ya nchi, kama kuna aliyepata kuhudumu katika timu yake na akasafiri naye kwa siku zote hizo per diem zinamtosha kujenga nyumba.

Kilichokuwa kinanichosha ni pale unapokuta wabunge, au madiwani wanafanya ziara nje ya nchi kujifunza shughuli za kimaendeleo na mipango miji as if wao ndio kazi yao, Yani tuna wataalamu hawatumiki ambao walistahili hata hiyo nafasi waipate ili kwenye shughuli zao iwasaidie. Kila binadamu ana mazuri yake na mabaya yake, kwenye mizani Rais wa sasa anafanya kazi ya kupoza majeraha yaliyokuwa yapelekee kifo kwa taifa letu
 
Kilichokuwa kinanichosha ni pale unapokuta wabunge, au madiwani wanafanya ziara nje ya nchi kujifunza shughuli za kimaendeleo na mipango miji as if wao ndio kazi yao,

Speaking of wabunge...hao nao vile viinua mgongo vya mamia ya mamilioni ya shilingi havijakaa sawa kabisa.

Watu wanalipwa viinua mgongo vya juu namna hiyo kwa kazi gani?

Huko kwenye majimbo yao mbona hata sionagi ya maana wayafanyayo!

Mimi nasema hawastahili kulipwa hizo hela zote.

Ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi ambao wengi wao ni maskini.
 
Ni kweli kabisa. Pesa zilikuwa zimezagaa hovyo mpaka kwa watu wasio wazalishaji. Kuna sehemu kwenye food centre huku ulikuwa ukipita utafikiri mtaa mzima ulikuwa unanunua chips kwa hiyo foleni yake lakini pita sasa hivi uone unaweza usikute mtu hata mmoja ndani ya dakika 20.
 
Nashukuru Mungu baada ya huyu mzee kushika nchi mambo yangu nliyokuwa nafanya kwa shida kwa kuwa ni ya kihalali sasa yanaenda vizuri waliozoea misheni town ndo wamefulia balaaaa japo kamshahara alikashusha mwanawani ila nimezoea nikiuza natoa risiti mambo safi sana
 
njinsi anavyopanda mambo utafikiri yuko Tanzania hajui hata bei ya vitunguu na nyanya kwa sasa dude.


swissme
Regardless na alipo Nyani Ngabu, alichosema kwani ni uongo? Point kubwa ambayo ungechukua ni kwamba mambo yamerudishwa pale yanapotakiwa baada ya miaka kumi ya kutegemea ufisadi. Wale watakao acknowledge hili mapema ndio watakaofanikiwa. Kama unang'ang'ania uchumi urudishwe kwa mafisadi ili na wewe wakurushie kidogo basi utangojea sana.
 
Regardless na alipo Nyani Ngabu, alichosema kwani ni uongo? Point kubwa ambayo ungechukua ni kwamba mambo yamerudishwa pale yanapotakiwa baada ya miaka kumi ya kutegemea ufisadi. Wale watakao acknowledge hili mapema ndio watakaofanikiwa. Kama unang'ang'ania uchumi urudishwe kwa mafisadi ili na wewe wakurushie kidogo basi utangojea sana.
....
......Mkuu mbaazi imeshuka bei na mvua imeanza Babati ...jee .kuna doti komu
 
....
......paundi na doralee jaeni kwenye chungu nirudi nyumbani CHOMA CHA NKOLA
 
Back
Top Bottom