Kimsingi si sahihi na hata kibiblia pia c sahihi na nikosa kubwa Hakuna ibada ya wafu pia na MTU akifa ni hukumu nyinyi hata mkiomba Mara mia kwa cku haisaidia ushauri ACHENI KUTENDA MABAYA JIFUNZENI KUTENDA MENA
Mimi kwa upande wangu naona kuombea na kuabudu maiti haina maana kabisaaa na sio kidogo kama uonavyo wewe.
umetoka nje mada mkuu hata hivyo asante kwa kuchangia.
Mhubiri 9:5 unasema mtu akifa hajji chochote, Hana kumbukumbu tena
Pumzi ya mungu + udongo = MTU. Na MTU toa pumzi inabaki UDONGO.
Sasa unapoabudu udongo maanake akili yako sio timamu. Abudu aliefinyanga huo udongo na kupulizia pumzi yake akatokea adam
Hayo maisha ya mtu baada ya kifo unaweza kunipa uthibitisho kwamba kweli huwa wanaishi au ni uvumi tu mkuu?
Ukijua maana ya neno IMANI utakuwa umshapata jibu lako......kwani nilianza na neno......kwa watu wa IMANI..
hata kama ni imani je ni sahihi kumwabudu marehemu au kumwombea maana marehemu hajui na hajijui kabisaa.
Nimempa na andiko..
Heshima katika mwili ila sio kumwabudu au kumwomba atuombee au kumsihi atuletee mvua au eti anataka achinjiwe mbuzi.
Ninachoamini mimi ni kuwa Binadamu akiwepo duniani ndipo unapoweza kumuomba chochote na hata Kumuombea.
-Pia binadamu anapokuwa duniani ndipo anapokuwa na fursa ya kuamua na kukata shauri aishije na Atakapokufa tu ndipo atakapohukumiwa kulingana na aliyoyatenda duniani. "Duniani ndipo penye bonde la kukata maneno"
-Akishakufa ndugu yangu huwezi kumwombea akabadilishiwa hukumu na Muumba wake,au akifa na maovu yake eti awekwe peponi.tunajifariji tuu kwa kuonesha kumjali. Kata shauri ukiwa bado una pumzi ya bure.
-
Wewe binadamu mtenda dhambi mkubwa utamwitaje mtu mtakatifu wakati Yesu mwenyewe alikataa asiitwe mtakatifu? Labda mteuwe mtakafujo ila sio mtakatifu.
Kumb 18:9-12.hakuna ibada za wafu,Waebrania 9:27 Baada ya kifo,hukumu na kila mtu atabeba madhambi yake mwenyewe.
Wacha uongo wa mchana....Daaah
Kwani kumuombea mfu ni kumwabudu?
Soma Kitabu cha Pili cha Wamakabayo uone mambo....