Ni haki kumwabudu marehemu?

Ni haki kumwabudu marehemu?

Ni haki kumwabudu marehemu?

Kwa kuwa umeulizia haki, hebu tuangalie Katiba ya JMT inasemaje:

19.-(1) Kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa mtu
kubadilisha dini au imani yake.

(2) Bila ya kuathiri sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu ya binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.

(3) Kila palipotajwa neno "dini" katika ibara hii ifahamike kwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na maneno mengineyo yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa kwa maana hiyo.
 
Jabulani
umetoka nje mada mkuu hata hivyo asante kwa kuchangia.
 
Last edited by a moderator:
Pumzi ya mungu + udongo = MTU. Na MTU toa pumzi inabaki UDONGO.
Sasa unapoabudu udongo maanake akili yako sio timamu. Abudu aliefinyanga huo udongo na kupulizia pumzi yake akatokea adam
 
Kimsingi si sahihi na hata kibiblia pia c sahihi na nikosa kubwa Hakuna ibada ya wafu pia na MTU akifa ni hukumu nyinyi hata mkiomba Mara mia kwa cku haisaidia ushauri ACHENI KUTENDA MABAYA JIFUNZENI KUTENDA MENA

Hebu weka na aya uliyosoma kwenye Biblia yako.
 
Kwa kuwa umetumia neno 'haki' ambalo limekaa kisheria zaidi, jibu huenda likawa ni haki...

Uhuru wa kuabudu huweka bayana kuwa mtu yu na haki ya kuabudu atakavyo mradi tu asivunje sheria za nchi...

Ila kama unataka kujua ni sahihi au si sahihi basi nakushauri urejelee mafunzo ya imani yako...
 
Kwanini utupe mchicha wakati kuna watu wanahuhitaji waule na kwa desturi za wanadamu maiti huzikwa na wengine huchoma ila mchicha huliwa je maiti unakusaidiaje mheshimiwa?

usipende ubishani usio na maana.
Huwez mtu kusema ni bora utupe jalalani maiti ya mamaako mzazi iliwe na mbwa kuliko kutupa fungu la mchicha.
 
Watu wa imani huwa tunaamini kuwa kuna maisha baada ya kifo.....kwa hiyo kwetu sisi mtu aliyefariki ni mfano wa mtu aliyehama makazi kutoka hapa duniani kwenye ulimwengu wa kimwili na kuhamia mbinguni kwenye ulimwengu wa roho....

Ndio maana huwa tunaamini kuwa kimwili huwa hatupo nao lakini kiroho tupo nao wapendwa wetu......na ni jambo la hekima na kiungwana kumtakia heri huko alipofikia mpendwa na kwa kuthibitisha upendo huo ndio maana huwa kuna watu wanashindwa kujizuia na kuangua kilio kwa uchungu wa kuondokewa na mpendwa wao.....na baada ya kilio huwa tunasema REST IN PEACE......

natumaini nimeeleweka..........
 
KikulachoChako

Hayo maisha ya mtu baada ya kifo unaweza kunipa uthibitisho kwamba kweli huwa wanaishi au ni uvumi tu mkuu?
 
Last edited by a moderator:
usipende ubishani usio na maana.
Huwez mtu kusema ni bora utupe jalalani maiti ya mamaako mzazi iliwe na mbwa kuliko kutupa fungu la mchicha.

Soma vizuri kisha unielewe hapo umenisemea japo si msemaji wangu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom