Ni haki kumwabudu marehemu?

Ni haki kumwabudu marehemu?

Wana JF.Hili swala la kumwabudu marehemu au kumwombea wakati yeye kashakufa na hana ufahamu wowote kweli ni jambo jema? Maiti haijui wala haisikii nijuavyo mimi sijui wenzangu mnajuaje? Maiti haina thamani yoyote hata fungu la mchicha la mia mbili inaizidi thamani nijuavyo mimi.Naombeni na nyie mawazo yenu kuhusu hili watu wa jf.

Nadhani uanhitaji kuelewa kuwa kuabudu na kuombea ni tofauti kabisaa.
 
kuabudu sio haki. ni maamuzi binafsi, ndio maana unaweza kutoabudu chochote au yeyote.
pia kuombea na kuabudu ni mambo mawili tofauti.
kwa mtazamo wangu haina maana sana kwa kua maiti ni sehemu ya tuchokipata kutokea kwene dunia hii na kuzika ni part ya kukirudisha so kuombea maiti...ni kupoteza mda......kitokacho kwa Mungu ndio kinarudi kuhukumiwa na hukumu inatokana na namna mtu alivotumia mda wake duniani kufanya mema au mabaya...cdhani kama maombi yanaweza kubadilisha chochote

Mawazo bhana! Kweli unaamini MUNGU wetu mtukufu atuumbe atupe thamani ya juu and then aje atutese duh!
 
Albosignathus
Soma Mhubiri 9:5 inasema Mtu akifa hajui neno lolote.Pia Mungu anasema usiabudu kitu chochote isipokuwa Mungu wa Mbinguni peke yake. Kwa hiyo ibada za wafu ni ibada za mizimu na Mungu amezikataza.
 
Last edited by a moderator:
Soma Mhubiri 9:5 inasema Mtu akifa hajui neno lolote.Pia Mungu anasema usiabudu kitu chochote isipokuwa Mungu wa Mbinguni peke yake. Kwa hiyo ibada za wafu ni ibada za mizimu na Mungu amezikataza.

Asante kwa mchango wako mkuu.
 
Kama mngalijua,imani ni kitu kigumu sana!

Mungu kakupa akili itumie mkuu.watu wangesema ngumu hata simu zisingekuwepo ila binadamu inatakiwa ujitahidi ujue hata kama umeshindwa kuunda japo baiskeli ila si vyema kulaghaiwa na uwongo na uzushi na watu waongo nawe ukakubali hata bila kufikiri?
 
Wana JF.Hili swala la kumwabudu marehemu au kumwombea wakati yeye kashakufa na hana ufahamu wowote kweli ni jambo jema? Maiti haijui wala haisikii nijuavyo mimi sijui wenzangu mnajuaje? Maiti haina thamani yoyote hata fungu la mchicha la mia mbili inaizidi thamani nijuavyo mimi.Naombeni na nyie mawazo yenu kuhusu hili watu wa jf.

Sasa swali lako unataka lijibiwe kwa misingi ipi?maana chukulia mfano hapa afrika tunaupinga ushoga ila wazungu kwao ni jambo la kawaida,kwahiyo na swali lako sijajua tulijibu kwa misingi ipi.
 
Sasa swali lako unataka lijibiwe kwa misingi ipi?maana chukulia mfano hapa afrika tunaupinga ushoga ila wazungu kwao ni jambo la kawaida,kwahiyo na swali lako sijajua tulijibu kwa misingi ipi.

Misingi ya akili timamu kwa mimi kwangu kama vile ni utahira kuabudu mzoga au kuombea mzoga.jibu vyovyote uwezavyo mkuu.
 
We umejuaje kuwa marehemu hajijui?

Nikimgusa hashtuki,nikimsemesha hasikii kwa maana hata hanijibu na nambeba namweka kwenye kaburi na kumfukia hapigi kelele wala kulalamika lakini mkuu wewe hapo ulipo nikija kukuchukua nikuweke kaburini utapiga mayowe hadi hadi mashuzi kwa maana unajielewa kwamba hai.
 
Soma Mhubiri 9:5 inasema Mtu akifa hajui neno lolote.Pia Mungu anasema usiabudu kitu chochote isipokuwa Mungu wa Mbinguni peke yake. Kwa hiyo ibada za wafu ni ibada za mizimu na Mungu amezikataza.

marehemu anaweza kuombewa akarudi duniani , je kuna uwezekano wa kumuombea kwenda mbinguni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom