Ni "HAIRISHA" au "AHIRISHA"

Ni "HAIRISHA" au "AHIRISHA"

Tumia neno Ghairi kwa kuelezea kama ni mtu mmoja Ame kama ni wengi Wame..
Nime ghairi kwenda shule

Nime ahirisha kwenda shule

Ghairi inaonekana kama ni kitendo cha ghafla

Na ku ahirisha unapanga kwa kutumia mda na sio ghafla

Au nakosea?
 
Neno sahihi ni "ahirisha". Mzizi mkuu ni -ghairi-.

Wengine wakiwa na haraka wanaandika "harisha"

Watanzania japo Kiswahili ndiyo lugha yetu, lakini tuna makosa mengi sana kwenye uandishi. Japo Kiswahili ni lugha yetu kuu kuliko watu wote duniani, lakini bado inatushinda. Ukiangalia post za wasomi na wataalam, zina makosa mengi sana ya kiuandishi.
 
vijana wa siku hizi hujuaji mwingi kama suruali na mkanda. Hivi ni hawezi au awezi?. Hivi ni hawezi kuja au awezi kuja. Gen Z bwan.a. Tunakoelekea tutaanza kuulizana ni neno sahihi ni lipi kati ya xaxa au sasa.
Hivi ni hujuaji au ujuaji?
 
Bora katika matamshi itaeleweka, nikimsikia Heche anawema "kweri mmeerewa" simshangai kabisa ila akiandika "kweri mmeerewa" nitashangaa 😁

Au lafudhi inaenda hadi kuandika?? Sijawahi kuona Robert Heriel Mtibeli kaandika "thithi" badala ya sisi.

😂😂
Siku ukisikia naongea ndio utaelewa.

Naongea kithembe kile cha wapare wa gonja kabisa
 
Onya na hali kitu kuwa bayana yani kuonekana ina husiana vipi bwashee?
Ngoja nikuache rafiki yangu Ingekuwa ni miaka ya tisini ningesema jana usiku ulikesha beach party . Beach party ilifungwa na serikali kati ya mwaka 1996 au 1997.
 
Back
Top Bottom