ShesRise_1
JF-Expert Member
- Aug 21, 2025
- 16,776
- 39,743
Maana unaweza kusema, "Ninakubalika." Sawa, lakini unakubalika na akina nani?
Ni watu wa aina gani wanaokukubali?
Kwa sababu si kila anayekukubali anaelewa hata maana ya kukukubali.
Wengine wanakufuata kwa mazoea, wengine kwa mihemko, na wengine kwa sababu hawajui hata lipi ni sahihi na lipi si sahihi
Unaweza ukawa na kundi kubwa sana la watu, lakini likiwa halina uwezo wa kuhoji wala kuchambua, kweli huo ni mtaji au ni idadi tu?
Watu ambao kazi yao ni kusema, "Ndiyo mzee. (Pr J song ) Ukisema kushoto ni kulia, watasema ni kweli. Ukibadili kesho, nao watabadilika bila hata kukuuliza kwa nini
Binafsi, bora niwe na watu wachache wanaoweza kunichana makavu kuliko kuwa na maelfu wanaoniambia kila siku kuwa niko sahihi
Bora niwe na watu wanaoweza kunisifia hadharani lakini wakinikosoa hata kwa siri
Bora niwe na watu wasioniogope bali waniheshimu(tuheshimiane sio kuogopana)
Watu ambao wakiona nimepotoka, wana ujasiri wa kuniambia
Hapana, hapo umekosea
Kwa sababu watu wanaoshindwa kukukosoa si wote wanakupenda
wengine wanaogopa, wengine wananufaika na makosa yako, na wengine hawana hoja kabisa
Sasa jiulize, unataka watu wanaojenga fikra zako au wanaojenga ego yako?
Wewe mdau, unapendelea kuwa na kundi kubwa lisiloweza kukuchallenge, au watu wachache wenye akili wanaoweza kukubadilisha kwa hoja, kwa maneno na kwa vitendo?