Ni "HAIRISHA" au "AHIRISHA"

Ni "HAIRISHA" au "AHIRISHA"

Kwa sisi vijana wa zamani, tuliofundishwa na walimu makini hatuchanganyi kabisa A na H. 😁

Ila kwa sasa sio ajabu kabisa kuona mwalimu wa somo la kiswahili anaandika "hasubuhi" huwa nashangaa kwakweli. Au mwalimu anaandika "kweri" inashangaza.
Inasikitisha sana, walimu wa upe walikua fresh sana
 
udambwi udambwi ni msemo wa mtaani ukimaanisha vionjo.
Sasa mimi nimesema nini!?..sababu udambwi upo kwenye mpira,usimuliaji,hata upishi,na aliyelileta mtaani ni mbwiga mbwiguke
 
Mtu anataka chakula anasema weka na udambwi udambwi. Urembo kwenye chakula???

Au ni neno ambalo maana inategemea na mazingira
Elewa muktadha, kwenye mpira udambwi ni chenga zile,kwenye supu ndimu na pilipili, kwenye kutiana viuno na milio
 
Tumbukiza au Dumbukiza...?
Nimemkuta hayupo...?
Nitarudi au narudi ilihali anaenda...?

Wabongo Kiswahili fasaha kinatushinda sana.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
Sahihi ni tumbukiza

Hapo kuna kutohoa kulingana na mlio wa kitu kikitumbukizwa kwenye maji yani

Dumbwii

Tumbwii 😅
 
Neno sahihi ni "GHAIRISHA(watu wa bara wanatamka hairisha)" kutoka katika neno "GHAIRI"
Maneno mengine ni kama
-Gharama(watu wa bara wanatamka garama)
-Shaghalabaghala(watu wa bara wanatamka shagalabala)

Cc Mahondaw
Hapa umeangalia usahihi kulingana na eneo ulilopo, ila sio usahihi katika lugha ya kiswahili.
 
Kukuongezea uvaaji wa kata K hapa Tanzania ulianza mwaka 1994 nikiwa form 2 na sikuwahi kuvaa hivyo.
Alianza nani kuvaa kata k?..kwa taarifa yako kata k tz ilivaliwa 1970-80s huko tunduru waliita debweza(mlegezo) wakiiga wababe wa cinema
 
Hatucheki na wowote au yeyote....
Maneno yote yapo sawa inategemea hicho usichocheka nacho ni kitu gani

Kama haucheki na mtu ni
(hatucheki na yeyote)

Kama hatucheki na kitu ni
(hatucheki na chochote)

Kama hatucheki na muda ni (hatucheki na wowote)

Kuloga na kuroga naona yanatumika yote, inategema na sehemu na sehemu.

Neno ambalo limenihangaisha mie ni kachumbali/kachumbari 😁
Yeyote na Yoyote wabongo hawajui namna ya kuyatumia ipasavyo.

Yeyote = Nafsi ya 3 umoja.
Yoyote = kiwakilishi cha kitu chochote kinachowasilishwa na kiambishi cha irabu kama "ile kamba" huendana na kamba yoyote, ila "kile kiatu" huwezi kusema kiatu yoyote bali "kiatu chochote".

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Back
Top Bottom