Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Bibi yangu huko Namtumbo zitamsaidia nn hizo ndege?
 
Magufuli huhitaji kupiga kampeni ili, au kunibembeleza ili uweze kupata kura yangu, yale uliyofanya Kwa kipindi kifupi ulichokaa madarakani yananilazimisha kukupa kura yangu, na kutokufanya hivyo nitakuwa nimefanya dhambi isiyosameheka.
 
unavyonionyesha fursa za Kigoma unasahau za chattle unataka nikufanye nini?
fursa Zaidi za kwenye ndege ni nyie watu wa chattle kuweka mifugo yenu kwenye Dreamliner na kuyapeleka malishoni,sijaona la ziada ambalo watanzania watafaidika nalo...umeshindwa kuweka hapa,ni kwamba hakuna..end of!
Nimerudi dada.
samahani huku kigoma kazi ni nyingi zinatuelemea sana nikakuacha kwa muda.
Enhe! Bado unatafuta kazi? au we unataka za Chattle tu?
 
Tunajadili vipaumbele kwa sababu ni wajibu wetu ingawaje tunafahamu impact ya mijadala yetu ni dogo to nothing!!!

Binafsi sipingi Flyover kwa sababu, as far as I know, zinajengwa kwa pesa za Wajapan na ni project ambayo JPM kaikuta ingawake pia alikuwa na uwezo wa kuifuta ikiwa inatumia pesa zetu!

Sipingi SGR kwa sababu whether we like it or not lazima tuwe na reli ya kisasa... concern yangu kwenye reli ni ikiwa tulifanya utafiti wa kutosha na ku-conclude, kwa mfano "...why to central corridor and not to southern highland, north au kwingineko!"

Concern yangu ni endapo tunafahamu ni kwanini wafanyabiashara wana-opt kutumia malori wakati reli ya TAZARA bado ipo vizuri!!

Ikiwa watu wanaiacha TAZARA na kutumia malori, nini kitawafanya wasiiache SGR na kutumia malori?

Mimi ugomvi wangu mkubwa na Magu ni ndege pamoja na ukuta wa Merelani!!!

Sipingi ndege eti kwa sababu ni za pangaboi or anything like that lakini napinga investment kwenye ndege kwa sababu hatuna muscles za ku-compete kwenye airline business ambayo kwa Afrika inaonekana ni loss making business na kuna factors kibao zinazofanya iwe hivyo!!!

Sisemi tusiwe na ndege but issue ni timing! Kwa sasa, ilikuwa bado kwa sababu zile trilioni kuna sehemu kibao ambako tungewekeza na kupata return maradufu kulikio kwenye airline, ambayo si tu possible return inaegemea kwenye loss lakini hata multiplier effect yake ni ndogo!

Viwanja vya ndege, fine lakini sio vyote fine! Chato International Airport ni uwekezaji wa hovyo!!!

Umehoji kwenye elimu, afya na kilimo!!!

Tuchukue mfano wa elimu!! Aliyemtangulia alikuta upungufu mkubwa sana, tena sana wa walimu!!! Serikali ikawekeza kwenye kudahiri wanafunzi wa Ualimu hadi ikafikia watu wakawa wana-opt ualimu kutokana, pamoja na mambo mengine, uhakika wa ajira!!

Matokeo yake, tukapata walimu wengi sana wa masomo ya sanaa kiasi kwamba hivi sasa serikali inalazimika kuhamishia wengine primary schools ingawaje wana shahada!!!

Nakumbuka mtihani mgumu ulikuwa kwenye kupata walimu wa sayansi lakini jitihada za kupata walimu wa sayansi zilionekana! Jitihada ya wazi kabisa ni ile ya kuanzisha Special Diploma ya masomo ya sayansi!

Magu alipoingia tu, akaifuta ile special diploma kwa hoja kwamba hawakuwa na sifa!!!

Kama hawakuwa na sifa, FINE but tell me...

Baada ya kufuta ile special diploma serikali imefanya nini kukabiliana na uhaba mkubwa wa walimu wa sayansi?!

Kama hoja ni kwamba wale wanafunzi hawakuwa na sifa, kimefanyika nini kudahiri wanafunzi wenye sifa?!

Unauliza kuhusu afya?! Au nikukumbushe pale serikali ilipokuwa imekubaliana na serikali ya Kenya kuajiri madaktari kutoka Tanzania?!

Hivi makubaliano yale yalitokana na hospitali zetu kuwa na madaktari wa kutosha au nchi yetu kuwa na madaktari wengi wasio na kazi ilihali hospitali zina uhaba mkubwa wa madaktari?!

Inawezekana tuna mashule kila mtaa... kuna maana gani basi ikiwa hazina walimu wa kutosha huku pesa zikiwekezwa kwenye vitega uchumi vinavyotia shaka?!

Inawezekana tuna mahospitali kila baada ya kilometa 1... umuhimu wake ni nini basi ikiwa zina uhaba mkubwa wa madaktari ilihali madaktari wamejaa mtaani huku vipaumbele vyetu vikiwa ni ndege?!

Kilimo?! Sema unatania...

Kuna mahali niliandika... endapo Magu angekuwa ni mtu wa ku-evaluate vipaumbele, basi haya yote anayotaka yangewezekana tena kwa kiwango cha juu kabisa endapo nguvu kubwa anazotumia kwenye madini angewekeza kwenye gas!

Umetoa hoja murua sana mkuu.
Nyingi nakubaliana nawe, lakini zingine zinahitaji mjadala mrefu na kuelimishana.
Nikipata muda tunaweza kuendeleza mjadala huu hapo baadaye.
Kwenye issue ya elimu na waalimu kuna issues nyingi sana zinazohitaji mjadala maana tulikokuwa tunaelekea tulijali zaidi quantity kuliko quality. Binafsi nilifurahi sana JPM alipoingilia kati suala hili. Hakuna haja ya kujaza waalimu feki mashuleni eti kwa sababu tu shule hazina waalimu wa sayansi. Ni bora gap iendelee kuwepo ili tujue tuna shida kuliko kujiliwaza tuna waalimu lakini ni namba tu.
Kwenye afya JPM kaimprove sana huduma kuliko mtangulizi wake. Ni kweli bado kuna changamoto lakini improvement ipo.
Kuhusu ajira ni kweli zilisimama lakini ni kwa sababu ilibidi kuhakiki zile zilizokuwepo, na yaliyotokea yanajustify the means. Na hivi sasa wengi tu wameanza kuajiriwa.
Kwenye Kilimo nakubaliana nawe kinahitaji kuangaliwa.
Maswali ya kwa nini TAZARA haitumiki na watu wanaopt malori ni maswali muhimu sana! Tuyaweke mezani kwa mkuu. I am sure kama JPM atagundua hila yeyote TUNAMFAHAMU, atayafanyia maamuzi, ingawa hii ni kazi ya waziri wa uchukuzi.
JPM pamoja na kasoro za kibinaadamu anazoweza kuwa nazo, lakini ni RAIS mwenye dhamira ya kweli ya kupambana na hila zozote zinazohujumu nchi yetu. Tumtumie tusije tukajajuta hapo baadaye tutakapokuja wekewa RAIS na MAFISADI na wauza madawa ya kulevya.
 
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Elimu bora ni utashi wa mtu sio bure na igharamie,no free lunch,Tanzania sio social welfare state.Hakuna cha bure.Msuya alisema kila mtu abebe msalaba wake.
 
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Bandiko zuri sana hili,congrats.Ni kweli JPM tunaona output,wengine ilikuwa zero.
 
Hivi nani kakuambia shghuli zza gas zimeachwa ? unajua kuana kiwanda cha mbolea kinataka kuanza kujengwa? unajua Gas inasambazwa viwandani na kwenye majumba hapa Dar , please msipende kudanganya watu kujitia kujua kila kitu,.Pia utafiti wa Gas unaendelea sehemu nyingi hapa nchini nenda ziwa Rukwa , Mkoa wa Pwani na bila kusahau utafiti wa Mafuta Wembere unajua hicho.
Kiwanda cha mbolea kipi?!

Hizo project za gas viwandani na majumbani ni za tangu awamu iliyopita!

Hata hiyo project ya viwanda vya mbolea ni tangu awamu iliyopita !

I doubt ikiwa una details za kutosha kuhusu oil and gas industry!

Hayo yote hapo juu kwa sasa yanasuasua kwa sababu ufanisi wake ulitegemea uchimbaji wa "gas ya Muhongo" na sio gas ya Msimbati!!

Kama unadhani unajua (am certain hujui lolote), tell us unafahamu nini kuhusu Gas Processing Plant pale Lindi!!
 
Umetoa hoja murua sana mkuu.
Nyingi nakubaliana nawe, lakini zingine zinahitaji mjadala mrefu na kuelimishana.
Nikipata muda tunaweza kuendeleza mjadala huu hapo baadaye.
Kwenye issue ya elimu na waalimu kuna issues nyingi sana zinazohitaji mjadala maana tulikokuwa tunaelekea tulijali zaidi quantity kuliko quality. Binafsi nilifurahi sana JPM alipoingilia kati suala hili. Hakuna haja ya kujaza waalimu feki mashuleni eti kwa sababu tu shule hazina waalimu wa sayansi. Ni bora gap iendelee kuwepo ili tujue tuna shida kuliko kujiliwaza tuna waalimu lakini ni namba tu.
Kwenye afya JPM kaimprove sana huduma kuliko mtangulizi wake. Ni kweli bado kuna changamoto lakini improvement ipo.
Kuhusu ajira ni kweli zilisimama lakini ni kwa sababu ilibidi kuhakiki zile zilizokuwepo, na yaliyotokea yanajustify the means. Na hivi sasa wengi tu wameanza kuajiriwa.
Kwenye Kilimo nakubaliana nawe kinahitaji kuangaliwa.
Maswali ya kwa nini TAZARA haitumiki na watu wanaopt malori ni maswali muhimu sana! Tuyaweke mezani kwa mkuu. I am sure kama JPM atagundua hila yeyote TUNAMFAHAMU, atayafanyia maamuzi, ingawa hii ni kazi ya waziri wa uchukuzi.
JPM pamoja na kasoro za kibinaadamu anazoweza kuwa nazo, lakini ni RAIS mwenye dhamira ya kweli ya kupambana na hila zozote zinazohujumu nchi yetu. Tumtumie tusije tukajajuta hapo baadaye tutakapokuja wekewa RAIS na MAFISADI na wauza madawa ya kulevya.
Nikipata wasaa, nitarudi kujadili hayo mengine manake nimekuja kuchungulia tu! Kwa sasa nitaongea jambo moja tu: Walimu na Special Diploma Education (primary & secondary school)!!

Hili suala nilifuatilia kuanzia sifa hadi course outline!

Sifa ilikuwa ni wale waliofaulu Form IV kwa kiwango cha Div I - III huku masomo ya sayansi walitakiwa kupata at least C kwenye Physics, Chemistry, Maths and Biology!

Hawa wangesoma Special Diploma for 3 Years tayari kwa kuwa walimu wa sayansi O-Level & Primary Schools! Ukiangalia course outline; walikuwa wanatakiwa kusoma in deep masomo yale yale (PCMB) waliyosoma from Form I to Form IV!!

Now tell me, hivi mtu aliyefaulu kwa akili yake Form IV, say PCM amepata CBB kisha akapelekwa Special Diploma miaka 3 huku akisoma zaidi masomo yale yale... Physics, Chemistry and Maths! Mtu kama huyu anashindwa vipi kumfundisha mwanafunzi wa O-Level?

Nikiwa A-Level nilisoma tuition ya Physics & Maths toka kwa fresh Form VI Leaver! Na hata hapa JF, watu wa aina yangu tumejaa kibao kwa sababu hata ukienda pale Mchikichini, Tutors wengi ni Fresh Form Six Leaver na wanafundisha wanafunzi wa A Level na wanafanya vizuri!

Sasa ikiwa Fresh Form Six Leavers wasio na any additional training wanaweza kufundisha vijana wa A-Level na wanafaulu vizuri; sasa how come mtu aliyemaliza Form IV na kufaulu vizuri kisha akapata extra 3 years training huku akisoma tena masomo yale yale bado ashindwe kumfundisha mwanafunzi wa O-Level?!

Binafsi naamini kabisa katika hili JPM alikurupuka! Alikurupuka kwa sababu bado alikuwa na moto wa urais huku akitaka kuonesha yeye ni bora zaidi na kukusudia kukosoa kila la waliomtangulia!

Endapo asingekurupuka, angekaa chini na timu yake na kuangalia vigezo na kuviboresha!! Kama aliona mtu aliyepata C asingekuwa na uwezo na kumfundisha mtu wa O-Level hata baada ya kupata 3 years special diploma training; basi angesema sifa ni lazima mwanafunzi apate A or B!

Kama kungekuwa na incentives kama zilivyokuwa hapo awali, wapo ambao na A & B zao wangeacha kwenda Form V na kwenda kusoma Special Diploma!

Labda kiburi changu ktk hili kinatokana na ukweli kwamba, nilipomaliza kidato cha IV bado nilikuwa na uwezo wa kumfundisha mwanafunzi wa O-Level na akafaulu ingawaje sikuwa miongoni mwa watu wa kupata misonge!

Sasa ikiwa hata mimi ambae sikuwa among the best class bado nilikuwa nina uwezo wa kumfundisha kijana wa O-Level, kwanini huyu aliyefaulu vizuri na kusoma miaka 3 ya ziada yeye ndie ashindwe?!

Ninachomsifu JK katika hili ni kwamba alionesha jitihada hata kama hakufanikiwa!!

Nakumbuka, katika kutatua hili tatizo, awamu iliyopita walianza na kutaka kuajiri wa sayansi waliostaafu!

HAWAKUPATIKANA! Pale Wizarani walienda less than 100 teachers!!

Baada ya kugonga mwamba kwa walimu wastaafu, wakaita wale waliomaliza Form VI na kufaulu comb za PCMB miaka ya nyuma lakini hawakuwa na issue mtaani! Hawa waliandaliwa kusoma Special Advanced Diploma!!

HAWA NAO HAWAKUPATIKANA!!

Baada ya kugonga mwamba hapo, ndipo wakageukia O-Level na kuwaandalia special diploma na kuwapa incentive ya mkopo pamoja na uhakika wa ajira!

Sasa huyu JPM anafanya jitihada ipi kutatua hili tatizo?!

Fine... tukubaliane nae kwamba hawa wa O-Level hata kama wangekuwa na ufaulu wa AAA bado hawana ubavu wa kufundisha O-Level! Sasa ni kipi kinafanyika hivi sasa kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wa O-Level wanasoma Sayansi ili hatimae waende combination za sayansi kisha tupate hao walimu anaoamini ndio wanastahili?! Nini kinafanyika ku-motivate Form VI waliofaulu vizuri sayansi kwenda kusoma ualimu?

Umesema "hatuwezi kujaza walimu fake!" Mtu aliyefaulu vizuri kidato cha iv (kwa mujibu wa sifa zilizotakiwa) kisha akaenda kusoma special diploma miaka 3 ni kumkosea kusema eti ni mwalimu fake!!!

Aidha, kutochukua hatua za makusudi kutatua tatizo ni kuwakosea watoto wa maskini!!!

Tulimuona Mwigulu Nchema akipeleka watoto wake pale Feza! Na wengine wengi aina ya Mwigulu Nchemba watapelaka watoto wao Feza, St. Francis, Marian n.k ambako hakuna shida ya walimu wa sayansi!!!

What about watoto wa wapiga kura wake waliorundikana kwenye shule za kata kule vijijini?!
 
Walimu na Special Diploma Education (primary & secondary school)!!

Hili suala nilifuatilia kuanzia sifa hadi course outline!

Sifa ilikuwa ni wale waliofaulu Form IV kwa kiwango cha Div I - III huku masomo ya sayansi walitakiwa kupata at least C kwenye Physics, Chemistry, Maths and Biology!

Hawa wangesoma Special Diploma for 3 Years tayari kwa kuwa walimu wa sayansi O-Level & Primary Schools! Ukiangalia course outline; walikuwa wanatakiwa kusoma in deep masomo yale yale (PCMB) waliyosoma from Form I to Form IV!!
Nina mashaka na ukweli wa hiyo point niliyoibold.
Kama kweli kuna waliotimuliwa kusoma diploma ya ualimu wakiwa na passmark ya C nakubaliana na wewe kuwa kulikuwa na makosa makubwa.
Ninachojua C ni pass mark tosha kumpeleka mtoto form 5 hasa kwa masomo ya Science. Kwa hiyo kwa vigezo vyovyote vile kijana mwenye pass hiyo anaweza kusoma diploma ya ualimu kiulaini kabisa na akawa Super!
 
Mkuu, hiyo ilikuwa ndio ENTRY REQUIREMENTS kisheria.

Inawezekana wapo ambao waliingia bila hiyo sifa lakini hao ni wale walioingia kiujanja ujanja kama ilivyo kawaida yetu Wabongo!! Kimsingi, hilo ndilo ambalo JPM alitakiwa kulifanyia kazi! Kwamba, kama Entry Requirements ni C and Above basi LAZIMA iwe hivyo na wale wote ambao hawana hiyo sifa warudishwe home!!

Lakini kwa upande mwingine; pale kulikuwa na special diploma za aina mbili: moja ni kwa Walimu wa Sekondari na nyingine walimu wa primary school! Kwahiyo kabla ya kuwarudisha home, ilitakiwa kufahamika ikiwa Mhusika ni special diploma secondary or primary!!

But all in all, wapo wengi tu ambao walienda kusoma ile special diploma wakati walikuwa na sifa ya kwenda Form V! And am telling you, endapo ile program ingeendelea; hata Form VI waliokosa pass za kujiunga university, wangeenda kusoma ile special diploma kwa kutumia cheti cha Form IV kama ilivyo kwa fani zingine!

Boom na uhakika wa ajira ungewavuta wengi!
 
Ahaa Rebby hujanielewa point yangu kumbe samahani kwa hilo.
Hujamwelewa kitu gani hapo. Ujio wa ndege utapelekea ajira kwa marubani wa ndege, wahandisi wa ndege, wahudumu mbali mbali wa ndege etc etc. Ujio wa ndege utaleta watalii wengi zaidi hivyo ajira zaidi kwenye hoteli za kitalii, kampuni za kuhudumia watalii etc. Pato la taifa litaongezeka na hivyo nchi kuwa na uwezo zaidi wa kutoa ajira, kuongeza mishahara na kutoa huduma zaidi za kijamii hususani afya, elimu na maji.
 
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Hongera sana.
 
umepita Kariakoo maduka yanavyofungwa??? hakuna biashara..watu wenye ajira rasmi hawazidi 2m.punguzeni kuandika crap
 
Umetoa hoja murua sana mkuu.
Nyingi nakubaliana nawe, lakini zingine zinahitaji mjadala mrefu na kuelimishana.
Nikipata muda tunaweza kuendeleza mjadala huu hapo baadaye.
Kwenye issue ya elimu na waalimu kuna issues nyingi sana zinazohitaji mjadala maana tulikokuwa tunaelekea tulijali zaidi quantity kuliko quality. Binafsi nilifurahi sana JPM alipoingilia kati suala hili. Hakuna haja ya kujaza waalimu feki mashuleni eti kwa sababu tu shule hazina waalimu wa sayansi. Ni bora gap iendelee kuwepo ili tujue tuna shida kuliko kujiliwaza tuna waalimu lakini ni namba tu.
Kwenye afya JPM kaimprove sana huduma kuliko mtangulizi wake. Ni kweli bado kuna changamoto lakini improvement ipo.
Kuhusu ajira ni kweli zilisimama lakini ni kwa sababu ilibidi kuhakiki zile zilizokuwepo, na yaliyotokea yanajustify the means. Na hivi sasa wengi tu wameanza kuajiriwa.
Kwenye Kilimo nakubaliana nawe kinahitaji kuangaliwa.
Maswali ya kwa nini TAZARA haitumiki na watu wanaopt malori ni maswali muhimu sana! Tuyaweke mezani kwa mkuu. I am sure kama JPM atagundua hila yeyote TUNAMFAHAMU, atayafanyia maamuzi, ingawa hii ni kazi ya waziri wa uchukuzi.
JPM pamoja na kasoro za kibinaadamu anazoweza kuwa nazo, lakini ni RAIS mwenye dhamira ya kweli ya kupambana na hila zozote zinazohujumu nchi yetu. Tumtumie tusije tukajajuta hapo baadaye tutakapokuja wekewa RAIS na MAFISADI na wauza madawa ya kulevya.
Sio kwenye afya tu, ule ukiritimba wa wizara ya ardhi na wenyewe umepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Ujenzi wa nchi ya viwanda unahitaji uvumilivu, kama mtu kazoea pesa za bure bure za upigaji hawezi kuwa na uvumilivu huo, ni lazima atakuwa siku zote akiongea na kuandika upuuzi.
 
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
kuna ka ukweli hapo,nisiwe mtu wa kuping pinga tu ila ni lazima tuelewe huwezi pendwa na kila mtu,hata watoto wako uliozaliwa na mkeo kuna wengine watakupenda ila kuna wengine hawatakupenda japo ni baba yao na hawawezi kukuonyesha hawakupendi hii ndio dunia yetu
 
Back
Top Bottom