Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,437
3,457
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
 
"Binadamu kazi"
Kuongoza nchi ni kazi watu wanashindwa kuendesha familia ila wanaona haki kuponda nchi inavyoendeshwa.
Watu wajiulize kwenye familia zao wamefanya nini na nini wanacho kinachoonekana ni hatua kwao kimaendeleo.
Haaaahaaaaa
Kuongoza nchi ni kazi tena ni kazi kweli kweli. Hongera Rais kwa machache ufanyayo. Mungu akubariki.
 
Back
Top Bottom