Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Nchi hii ......... kazi kweli kweli!!

Sasa imekuwa ni ya nani ni afadhari kuliko mwingine .............!!
 
Hujamwelewa kitu gani hapo. Ujio wa ndege utapelekea ajira kwa marubani wa ndege, wahandisi wa ndege, wahudumu mbali mbali wa ndege etc etc. Ujio wa ndege utaleta watalii wengi zaidi hivyo ajira zaidi kwenye hoteli za kitalii, kampuni za kuhudumia watalii etc. Pato la taifa litaongezeka na hivyo nchi kuwa na uwezo zaidi wa kutoa ajira, kuongeza mishahara na kutoa huduma zaidi za kijamii hususani afya, elimu na maji.
Tatizo letu watanzania ni ukosefu wa uvumilivu. Tunazo akili za mchicha, ukipandwa leo unavunwa ndani ya miezi michache ijayo.
 
Nchi hii ......... kazi kweli kweli!!

Sasa imekuwa ni ya nani ni afadhari kuliko mwingine .............!!
Kweli Mkuu. Hizi pesa zinazonunua ndege hapo awali zilikuwaga zinaenda wapi?
 
airntanzania 1.jpg

Hivi kwani ATCL ndio mara ya kwanza kumiliki ndege? mbona hatuambiwi hapo awali ndege zake zilipatwa na nini?
 
Awali ipi kamanda?
Ile ya wapiga dili?
Hujui tuu ndugu yangu! wapiga dili sasa ndio wapo wa nguvu sema idadi yao ni ndogo lakini mapigo yao ndio makubwa. Shirika lilikuwa na ndege sio haba. Na wakati huo baada ya EAA kuvunjika 1977 kulikuwa na Boeing, Fokker mpaka Twin Otters. Safari za ATC zilikuwepo mpaka viwanja kama Mtwara, Lindi, Nachingwea hadi Masasi ndege za abiria zilikuwa zinaenda.
Ajabu badala ya kujiuliza tulipatwa na nini hadi kufikia hali iliyo kuwepo sasa, tunataka kudanganyana kama vile Watanzania wote wamezaliwa Miaka ya 1990 au 2000! maana aliyezaliwa 2000 leo ana miaka 18 na anaweza kuwepo hapa JF na akabisha hakuna mfano ukizingatia hata historia ya nchi haisomi na kuielewa bali muda wake mwingi ni kubet na kufatilia wasanii wa Bongo na swagga zao.
Waulize wazee wa zamani Pascal Mayalla , Elli ,JokaKuu Mzee Mwanakijiji to mention the few, watakuambia ATC ya baada ya East African Airways baada ya kuvunjika ilikuwaje. Ilikuwa na uwezo wa kukodi ndege kutoka Air Madagascar au Msumbiji (kama sikosei walikuwa wanaita DELTA) na mambo yalikuwa mazuri tuu. Hata Mwalimu aliwahi kujisifia wakati Fulani akiwa amesha staafu baada ya kuona ndege ya ATC imepaki Johannesburg ikisubiri kupakia.
 
hata 1.5 trillion ,tunaziona pia...
Kafie mbele kule uliwe na mamba ukivuka mto na wenzako.
Uliza mbowe hizo dosari za mamilioni ya shilingi zilokuwa audited na cag amepeleka wapi
 
Hujui tuu ndugu yangu! wapiga dili sasa ndio wapo wa nguvu sema idadi yao ni ndogo lakini mapigo yao ndio makubwa. Shirika lilikuwa na ndege sio haba. Na wakati huo baada ya EAA kuvunjika 1977 kulikuwa na Boeing, Fokker mpaka Twin Otters. Safari za ATC zilikuwepo mpaka viwanja kama Mtwara, Lindi, Nachingwea hadi Masasi ndege za abiria zilikuwa zinaenda.
Ajabu badala ya kujiuliza tulipatwa na nini hadi kufikia hali iliyo kuwepo sasa, tunataka kudanganyana kama vile Watanzania wote wamezaliwa Miaka ya 1990 au 2000! maana aliyezaliwa 2000 leo ana miaka 18 na anaweza kuwepo hapa JF na akabisha hakuna mfano ukizingatia hata historia ya nchi haisomi na kuielewa bali muda wake mwingi ni kubet na kufatilia wasanii wa Bongo na swagga zao.
Waulize wazee wa zamani Pascal Mayalla , Elli ,JokaKuu Mzee Mwanakijiji to mention the few, watakuambia ATC ya baada ya East African Airways baada ya kuvunjika ilikuwaje. Ilikuwa na uwezo wa kukodi ndege kutoka Air Madagascar au Msumbiji (kama sikosei walikuwa wanaita DELTA) na mambo yalikuwa mazuri tuu. Hata Mwalimu aliwahi kujisifia wakati Fulani akiwa amesha staafu baada ya kuona ndege ya ATC imepaki Johannesburg ikisubiri kupakia.
Narration hii inaonesha sasa umeelewa kwa nini JPM ameingia na HASIRA kwenye hii issue.
Wapiga dili wametuumiza sana hapo kati.
 
Hakuna nchiimewahi kufungwa kwa madeni.
Wacha tudaiwe huku tukiwa na UMEME wa uhakika, USAFIRI wa uhakika na huku madini yetu yakitulipa kwa UHAKIKA

Kila Awamu Kauli ni hizi hizi ,hata Awamu hii ikimaliza Muda wake atakae kuja tena nae atakuwa anaimba Wimbo huu huu kama Kasuku.Utafikiri ndio tume pata Uhuru hivi ...!.
 
Nachukia sana watu wenye akili fupi.. we unadhani katavi ungefika kwa Rami bila ya Kikwete?? Vp kuhusu Hapo JKIA unadhani hiyo ndege ingepata pa kupaki kama sio mkwere... mpumbavu mkubwa ww... kuna mengi sana kafanya Jakaya huyu Magu hata ajaribu hatofikia.. mf ajaribu kujenga chuo kama UDOM.. yaan hostel kelele kibaooo.. narudia tena Watangulizi walikuwa bora sana..
 
unaangalia tu ndege
huangalii hali mbaya ya biashara
hali mbaya ya kipato cha watanzania
unyang'anyi unaofanywa na serikali ya ccm
dhuluma kwa watumishi..
utekaji mauwaji
wanaume kugeuka kuwa wanamipasho..
dada hela ilienda sana kwenye huduma za kijamii na miradi inayogusa moja kwa moja wananchi kama vile kilimo..
ndege ni kipaumbele cha pombe..
 
Acha kujadili Watu ,jadili Hoja.
Sijadili watu, najadili na kuhoji wapi pesa ya chadema ilipo? Cag kafanya auditing, kagundua millions of money missing.
Sasa mtu anashindwa kumanage hela ya chama, ataweza vipi kumanage doo ya serikali
 
Afadhali tunaziona ndege! Ndio level ya ujinga tuliyofikia, watu wanazoa fedha hazina wanakwenda kununua ndege bila kufuata taratibu za kisheria wala bunge kuridhia matumizi hayo halafu kama haitoshi wanazuia ukaguzi wa manunuzi hayo. Tunaona ni sawa! Sijui huu upoyoyo unatokana na nini
 
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!

Hizo ndege ndo laana watanxania tutayojutia in the next 50 yrs
 
Back
Top Bottom