Kujadili vipaumbele kama unavyofanya Chige ni dalili nzuri kuwa kuna kazi inafanyika.
Lakini pia hebu fanya utafiti - Je nikweli kinachofanyika kwenye Elimu, Afya na kilimo?
Ningekuelewa kama ungesema aongeze zaidi.
Tunajadili vipaumbele kwa sababu ni wajibu wetu ingawaje tunafahamu impact ya mijadala yetu ni dogo to nothing!!!
Binafsi sipingi Flyover kwa sababu, as far as I know, zinajengwa kwa pesa za Wajapan na ni project ambayo JPM kaikuta ingawake pia alikuwa na uwezo wa kuifuta ikiwa inatumia pesa zetu!
Sipingi SGR kwa sababu whether we like it or not lazima tuwe na reli ya kisasa... concern yangu kwenye reli ni ikiwa tulifanya utafiti wa kutosha na ku-conclude, kwa mfano "...why to central corridor and not to southern highland, north au kwingineko!"
Concern yangu ni endapo tunafahamu ni kwanini wafanyabiashara wana-opt kutumia malori wakati reli ya TAZARA bado ipo vizuri!!
Ikiwa watu wanaiacha TAZARA na kutumia malori, nini kitawafanya wasiiache SGR na kutumia malori?
Mimi ugomvi wangu mkubwa na Magu ni ndege pamoja na ukuta wa Merelani!!!
Sipingi ndege eti kwa sababu ni za pangaboi or anything like that lakini napinga investment kwenye ndege kwa sababu hatuna muscles za ku-compete kwenye airline business ambayo kwa Afrika inaonekana ni loss making business na kuna factors kibao zinazofanya iwe hivyo!!!
Sisemi tusiwe na ndege but issue ni timing! Kwa sasa, ilikuwa bado kwa sababu zile trilioni kuna sehemu kibao ambako tungewekeza na kupata return maradufu kulikio kwenye airline, ambayo si tu possible return inaegemea kwenye loss lakini hata multiplier effect yake ni ndogo!
Viwanja vya ndege, fine lakini sio vyote fine! Chato International Airport ni uwekezaji wa hovyo!!!
Umehoji kwenye elimu, afya na kilimo!!!
Tuchukue mfano wa elimu!! Aliyemtangulia alikuta upungufu mkubwa sana, tena sana wa walimu!!! Serikali ikawekeza kwenye kudahiri wanafunzi wa Ualimu hadi ikafikia watu wakawa wana-opt ualimu kutokana, pamoja na mambo mengine, uhakika wa ajira!!
Matokeo yake, tukapata walimu wengi sana wa masomo ya sanaa kiasi kwamba hivi sasa serikali inalazimika kuhamishia wengine primary schools ingawaje wana shahada!!!
Nakumbuka mtihani mgumu ulikuwa kwenye kupata walimu wa sayansi lakini jitihada za kupata walimu wa sayansi zilionekana! Jitihada ya wazi kabisa ni ile ya kuanzisha Special Diploma ya masomo ya sayansi!
Magu alipoingia tu, akaifuta ile special diploma kwa hoja kwamba hawakuwa na sifa!!!
Kama hawakuwa na sifa, FINE but tell me...
Baada ya kufuta ile special diploma serikali imefanya nini kukabiliana na uhaba mkubwa wa walimu wa sayansi?!
Kama hoja ni kwamba wale wanafunzi hawakuwa na sifa, kimefanyika nini kudahiri wanafunzi wenye sifa?!
Unauliza kuhusu afya?! Au nikukumbushe pale serikali ilipokuwa imekubaliana na serikali ya Kenya kuajiri madaktari kutoka Tanzania?!
Hivi makubaliano yale yalitokana na hospitali zetu kuwa na madaktari wa kutosha au nchi yetu kuwa na madaktari wengi wasio na kazi ilihali hospitali zina uhaba mkubwa wa madaktari?!
Inawezekana tuna mashule kila mtaa... kuna maana gani basi ikiwa hazina walimu wa kutosha huku pesa zikiwekezwa kwenye vitega uchumi vinavyotia shaka?!
Inawezekana tuna mahospitali kila baada ya kilometa 1... umuhimu wake ni nini basi ikiwa zina uhaba mkubwa wa madaktari ilihali madaktari wamejaa mtaani huku vipaumbele vyetu vikiwa ni ndege?!
Kilimo?! Sema unatania...
Kuna mahali niliandika... endapo Magu angekuwa ni mtu wa ku-evaluate vipaumbele, basi haya yote anayotaka yangewezekana tena kwa kiwango cha juu kabisa endapo nguvu kubwa anazotumia kwenye madini angewekeza kwenye gas!