Mbona jibu la swala lako liko ndani ya jibu langu kwamba after 1977 = ufisadi, uhujumu uchumi + uporaji wa South Africa Airline katika shirika letu la ndege ndicho kilichotokea. Na hii ikasababisha hadi sasa shirika letu la ndege kuwa na madeni makubwa ya matrillion ya pesa.
Nimekwenda nyuma ya 1977 wakati tulikuwa na ndege kubwa kubwa za enzi hizo kama Concord na kadhalika ambazo tulikuwa tunazimiliki kwa pamoja sisi, waganda na wakenya kupitia EAC. Wakati tunamshughulikia nduli Amini wa Uganda aliyekuwa amevamia nchi yetu, wakenya wakavunja hiyo EAC na kupora ndege zote, treni zote na viwanda vyote. Baada ya vita dhidi ya nduli Amini, Tanzania na Uganda zikaanza upya wakati Kenya wanapeta na kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda. Sasa mimi ninakufundisha historia ya uchumi wetu tulikotoka, wewe unaniona ninanuka maziwa. Yaani babu yako anuke maziwa badala ya wewe mjukuu!