Nikipata wasaa, nitarudi kujadili hayo mengine manake nimekuja kuchungulia tu! Kwa sasa nitaongea jambo moja tu: Walimu na Special Diploma Education (primary & secondary school)!!
Hili suala nilifuatilia kuanzia sifa hadi course outline!
Sifa ilikuwa ni wale waliofaulu Form IV kwa kiwango cha Div I - III huku masomo ya sayansi walitakiwa kupata at least C kwenye Physics, Chemistry, Maths and Biology!
Hawa wangesoma Special Diploma for 3 Years tayari kwa kuwa walimu wa sayansi O-Level & Primary Schools! Ukiangalia course outline; walikuwa wanatakiwa kusoma in deep masomo yale yale (PCMB) waliyosoma from Form I to Form IV!!
Now tell me, hivi mtu aliyefaulu kwa akili yake Form IV, say PCM amepata CBB kisha akapelekwa Special Diploma miaka 3 huku akisoma zaidi masomo yale yale... Physics, Chemistry and Maths! Mtu kama huyu anashindwa vipi kumfundisha mwanafunzi wa O-Level?
Nikiwa A-Level nilisoma tuition ya Physics & Maths toka kwa fresh Form VI Leaver! Na hata hapa JF, watu wa aina yangu tumejaa kibao kwa sababu hata ukienda pale Mchikichini, Tutors wengi ni Fresh Form Six Leaver na wanafundisha wanafunzi wa A Level na wanafanya vizuri!
Sasa ikiwa Fresh Form Six Leavers wasio na any additional training wanaweza kufundisha vijana wa A-Level na wanafaulu vizuri; sasa how come mtu aliyemaliza Form IV na kufaulu vizuri kisha akapata extra 3 years training huku akisoma tena masomo yale yale bado ashindwe kumfundisha mwanafunzi wa O-Level?!
Binafsi naamini kabisa katika hili JPM alikurupuka! Alikurupuka kwa sababu bado alikuwa na moto wa urais huku akitaka kuonesha yeye ni bora zaidi na kukusudia kukosoa kila la waliomtangulia!
Endapo asingekurupuka, angekaa chini na timu yake na kuangalia vigezo na kuviboresha!! Kama aliona mtu aliyepata C asingekuwa na uwezo na kumfundisha mtu wa O-Level hata baada ya kupata 3 years special diploma training; basi angesema sifa ni lazima mwanafunzi apate A or B!
Kama kungekuwa na incentives kama zilivyokuwa hapo awali, wapo ambao na A & B zao wangeacha kwenda Form V na kwenda kusoma Special Diploma!
Labda kiburi changu ktk hili kinatokana na ukweli kwamba, nilipomaliza kidato cha IV bado nilikuwa na uwezo wa kumfundisha mwanafunzi wa O-Level na akafaulu ingawaje sikuwa miongoni mwa watu wa kupata misonge!
Sasa ikiwa hata mimi ambae sikuwa among the best class bado nilikuwa nina uwezo wa kumfundisha kijana wa O-Level, kwanini huyu aliyefaulu vizuri na kusoma miaka 3 ya ziada yeye ndie ashindwe?!
Ninachomsifu JK katika hili ni kwamba alionesha jitihada hata kama hakufanikiwa!!
Nakumbuka, katika kutatua hili tatizo, awamu iliyopita walianza na kutaka kuajiri wa sayansi waliostaafu!
HAWAKUPATIKANA! Pale Wizarani walienda less than 100 teachers!!
Baada ya kugonga mwamba kwa walimu wastaafu, wakaita wale waliomaliza Form VI na kufaulu comb za PCMB miaka ya nyuma lakini hawakuwa na issue mtaani! Hawa waliandaliwa kusoma Special Advanced Diploma!!
HAWA NAO HAWAKUPATIKANA!!
Baada ya kugonga mwamba hapo, ndipo wakageukia O-Level na kuwaandalia special diploma na kuwapa incentive ya mkopo pamoja na uhakika wa ajira!
Sasa huyu JPM anafanya jitihada ipi kutatua hili tatizo?!
Fine... tukubaliane nae kwamba hawa wa O-Level hata kama wangekuwa na ufaulu wa AAA bado hawana ubavu wa kufundisha O-Level! Sasa ni kipi kinafanyika hivi sasa kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wa O-Level wanasoma Sayansi ili hatimae waende combination za sayansi kisha tupate hao walimu anaoamini ndio wanastahili?! Nini kinafanyika ku-motivate Form VI waliofaulu vizuri sayansi kwenda kusoma ualimu?
Umesema "hatuwezi kujaza walimu fake!" Mtu aliyefaulu vizuri kidato cha iv (kwa mujibu wa sifa zilizotakiwa) kisha akaenda kusoma special diploma miaka 3 ni kumkosea kusema eti ni mwalimu fake!!!
Aidha, kutochukua hatua za makusudi kutatua tatizo ni kuwakosea watoto wa maskini!!!
Tulimuona Mwigulu Nchema akipeleka watoto wake pale Feza! Na wengine wengi aina ya Mwigulu Nchemba watapelaka watoto wao Feza, St. Francis, Marian n.k ambako hakuna shida ya walimu wa sayansi!!!
What about watoto wa wapiga kura wake waliorundikana kwenye shule za kata kule vijijini?!