Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Kwa nini unasema huko nyuma.
Unajua maendeleo ya nchi sio vitu vichache vya serikali wakati watu wana maisha duni! Kwa hiyo binadamu anahitaji hivyo vitu vichache tu ulivyotaja na vikikamilika basi kila kitu kitakua safi kabisa.

Unajua hivyo ulivyotaja vinafanyika wakati kuna watu wanadai pesa zao halali kabisa na hawajalipwa.
Kuna wafanyakazi mishahara yao ni midogo na sheria imewekwa wawe wanaongezwa kidogo kidogo na kupandishwa madaraja ili waweze kujikimu na kuendana na dunia yenye maendeleo ambayo kama huna hela unapata tabu sana na sio serikali.

Unajua MTU akipata msiba ndugu na marafiki ndio wanaomsaidia kuchangia pesa za kununua mpaka sanda na sio serikali?
Mtu akizaa mtoto anawajibika kumnunulia pumpas yeye mwenyewe kwa pesa zake .
Wazazi wetu kule kijijini wanategemea mahitaji kutoka kwa watoto wao wanaojishughulisha kwenye ajira au shughuli za kuwaingizia kipato na kama hawana kipato basi maisha yanakua magumu.
Ndio maana viongozi wote wa chama na serikali wana mishahara na marupurupu mazuri ulilinganisha na wafanyakazi wa chini. Kwa nini kwa sababu wanajua wakistaafu sio treni wala ndege itakao watinza Bali ni mafao yao na miradi waliojiwekea wao binafsi.
Unajua kila anachofanya mtu au binadamu kwa asilimia zaidi ya 90 kinategemea kipato alichonacho na sio kipato wala gari wala ndege wala treni ya serikali.

Somalia hakuna serikali lakini watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida wanachokosa ni amani inayotokana na ulinzi wa uhakika. Kinachowafanya waishi ni vipato vyao.
Nadhani wasomalia ni kati ya watu wanaosafiri sana kila mahali japo hawana hivyo ulivyotaja. Kinachowafanya wasafiri na kufanya biashara popote ni vipato vyao.

Wasomali ndani ya nchi yao Wanachokosa ni huduma muhimu za jamii na za uhakika kama elimu ,afya na maji na mfumo rasmi wa kifedha ndani ya nchi yao.
Siwasifii Wasomalia bali nataka uone umuhimu wa kuwapa wananchi uwezo wa kumiliki Mali kwanza ili waweze kuwekeza baadae .

Hakuna mtu anayepinga ndege lakini pia isiwe sababu ya kuona kuwa wanaoikosoa hawana haki. Yani ndege isionekane kuwa ni bora kuliko kila kitu.Isije ikawa kama Sanamu ya kuabudu enzi za mfalme Nebukadreza kwamba kila mtu ainame na kusujudu mbele ya sanam na anayepinga anatupwe kwenye tanuru la moto.
Binadamu tumeamriwa na Mungu kuwapenda wengine kama tunavyojipenda wenyewe.
Sio kupenda vitu na kuwachukia wengine.

Nakuuliza ,Hivi umewahi kukaa ukafanya tafiti za miradi iliyoanzishwa na awamu ya Tatu na ya NNE ambayo iliongeza mzunguko wa fedha na fursa kwa wananchi wote kuanzia wa chini mpaka wa juu ?
Unajua awamu zilizo tangulia kuna miradi mingi ilikua inazinduliwa tu na mawaziri na wakimbiza mwenge tu hivyo watu wengi walikua hawafuatilii.

Kazi nzuri na mafanikio ya awamu zilizopita zimesababisha Leo hii karibu kila familia kuna angalau mtu mmoja anamiliki gari.
Ukitoka Dar es salaam mpaka Kagera au Mwanza maeneo yote hayo yana lami na watu mpaka vijijini wana nyumba bora za bati na matofali na nje kuna gari imepakiwa. Walimu walijenga ,madaktari ,manesi,mapolisi ,wanajeshi,wafanyabiashara mpaka wamachinga walikua wananunua viwanja wanajenga nyumba zao za kuishi.
Hayo ndiyo maendeleo ya kwanza kabisa yanayomuhusu binadamu moja kwa moja ili aishi aishi maisha bora. Binadamu ni kiumbe hai kinachoishi kwa kula chakula na kunywa maji na kuvaa nguo kwa gharama. Ni lazima apate uwezo wa namna ya kupata mahitaji yake kabla ya yale yanayopatikana kwa wale wa madaraja ya juu kama ndege na treni ya umeme.

Siipingi ndege wala Treni lakini hivi vitu tusivifanye kuwa ni vitu vya kutweza na kuumiza watu wengine kwa sababu tu ya siasa.
Anayeisifia aisifie mana ni kodi yake lakini pia anayeikosoa akosoe mana ni Kodi yake pia.

Watu wanakosoa kwa sababu ya gharama kubwa zilizoingiwa kwa wakati mmoja na kwa muda mfupi.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake
Mpeni ; Awamu ya Tatu iliwawezesha wananchi wengi kuishi maisha bora . Hospitali zilijengwa kwa kiwango kizuri, maabara mashuleni, majengo hasa shule za kata,Vituo vya afya kila kata. Madaraja Makubwa kama la Kigamboni, hata ukipita mijini palikua na muonekano wa miji kukua kwa kasi na shughuli za kiuchumi zilishamiri. Kariakoo ilikaribia kuwa Soko LA Afrika mashariki na kati.

Ukipita barabarani palikua na vituo vya mafuta barabara zote na vijana waliajiriwa na kuendesha maisha yao.
Awamu ya NNE ilikuta kima cha chini cha mshahara kikiwa kidogo sana.
Marupu rupu mbalimbali yakiwemo ya wabunge na hao hao ambao Leo wanawatukana watangulizi wa awamu hii yalikuwa chini sana.

Wakubwa unaowaona leo walipewa maisha bora na awamu zilizopita kuanzia mishahara yao na marupu yao.

Kila awamu ilianza mambo yake kwa speed yake.

Hivi utasemaje waliotangulia hawakufanya kitu wakati tuna amani iliyolindwa kwa uwezo mkubwa wa vyombo vya ulinzi na usalama vyenye vifaa na zana za kiwango kizuri kabisa.?

Ukipita kwenye makambi ya jeshi hauoni nyumba za kisasa au ndio kujaribu kuwashushia heshima viongozi wa awamu zilizopita ?

Unajua ni zana kiasi gani za vyombo vyetu vya ulinzi na usalama zimenunulia na awamu ya tatu na ya NNE?
Kwa nini tunawazarau watangulizi wa awamu hii ambayo ni mapema kabisa . Kwa nini tunawadharau wakati wote wametoka na Chama Cha Mapinduzi?
Viongozi wote unaowaona ni matokeo ya mipango ya kujenga uwezo wa watu tangu awamu zilizopita! Wangepatikana vipi hao wa Leo kama nchi haikua na mwelekeo wowote.

Musiwavunjie heshima viongozi wetu wa awamu zilizotangulia .

Hebu angalia pia diplomasia ya taifa letu iko vizuri kwa sababu nchi ilikua ina viongozi mahiri walioitangaza dunia nzima.
Hivi unafikiri urafiki wa China na Tanzania ulianza leo?

Kwa Taarifa yako miradi yote unayoiona isipokua uwanja wa ndege wa Chato yote ilikua kwenye Ilani ya CCM kuelekea 2025 ili kuingia kwenye uchumi wa kati.
Na kila awamu ilikua na na ilani yake na kila mmoja alifanya mambo take .
Acheni kupotosha ; Watu wanapingana namna ya kutekeleza mipango ya uchumi na miradi ya maendeleo lakini hawapingi kwamba isiwepo.

Ni dhambi kubwa kusema kuwa kiongozi wa awamu Fulani hajafanya kitu.

Kila mmoja amefanya yake na akamaliza ngwe yake akawaachia wengine. Hakuna aliyaacha kwa sababu ya kushindwa kufanya kitu Bali walitimiza muda wao na kustaafu kwa heshma.
Sasa hii ya kusema Fulani tu ndio kafanya haifai. Tutamtathimini vizuri akimaliza muda wake 2025.
Kwa sasa tumpe muda afanye kazi.
Kazi ambayo itakutana na vikwazo ikiwemo kukosea na kukosolewa .
 
Wengi tu tena wenye 1st class
Ni aibu mtu una 1st class halafu unaitumia kulalamika mitandaoni na mitaani badala ya kuitumia kujiajiri.
Nchi ina Mafursa kibao 1st class yako inashindwaje kukusaidia kuziona fursa na kuzitumia wakati darasa la saba kibao wanazitumia fursa na kuishi vizuri kabisa.
Ndo maana Magu kaamua kufanya reforms vyuo vikuu,
Tumekuwa na mijitu inajivunia 1st class wakati ukiiangalia ni mizuzu tu.
Nchi hii ina kila aina ya fursa, halafu unakutana na jitu linajisifu lina 1st class lakini linalalamika halioni fursa.
 
Nakuchagulia na kibao cha "fagilia bongo" kutoka kwa mr Nice ili kusindikiza ujumbe wako
 
Ninachofahamu ni kuwa wajanja waliandika ule mradi wakapiga hela na kuwatelekeza watoto wa maskini kwenye yale majengo meupe...kabla hata Magu lile bomu lingekuja lipuka tu kwa namna yoyote ile.
Acha kupotosha!! Fuatilia hustles za kupata walimu wa sayansi... serikali ilianzia kutaka kuajiri wastaafu, ikashindikana kwa sababu walipatikana wachache!!

Baada ya kugonga mwamba kwa wastaafu, serikali ikaita waliomaliza PCMB miaka ya nyuma lakini hawakuwa na issue mtaani! Hawa walipangiwa kusomeshwa Special Advanced Diploma!!

Baada ya waliomaliza na kufaulu PCMB miaka ya nyuma kukosekana, ndipo pakawa hamna namna; likaja suala la Special Diploma kwa waliomaliza Form IV na kufaulu!! Kwahiyo hakuna cha suala la wajanja kupiga hela wala nini!!

Diploma.png

Hapo juu ni Loan Board. Taarifa hiyo inathibitisha kwamba walikuwa wanalipiwa na serikali. Sasa hilo suala la watoto kutelekezwa kwenye majengo meupe sijui umelitoa wapi!!!

Lakini hata kama kuna wajanja walipiga pesa na kusepa; then what?! Baada ya Magufuli kufuta ile program, hizo pesa ndo zimerudi?! Hivi hudhani busara ilikuwa ni kuendelea tu na ile program kutokana na manufaa yake kwa sababu kuifuta isingesaidia kurudisha hiyo pesa iliyopigwa? Na kama palikuwa na mapungufu, busara ilikuwa ni kuifuta au kuiboresha?!

Mkuu magia, maelezo yako ni sahihi kabisa labda tu niongeze machache.

Ile program ilikuwa ni kwa ajili ya walimu wa sayansi wa primary and secondary schools. Nadhani hapa ndipo Magu alipopotishwa na watu wake.

Lengo ilikuwa ni kwamba, wale ambao walionekana kama hawakuwa na maksi za juu ilikuwa ni kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na wenye maksi za juu ni kwa ajili ya walimu wa sekondari! Inawezekana utaratibu ulivurundwa lakini lengo lilikuwa hilo... na ndio jambo ambalo Magu alitakiwa kuhakikisha linafanyika!

Aidha, kama kumbukumbu zangu ipo sawa, ile program ilikuwa under World Bank sponsorship na sio Marekani! Hata hivyo, sio kwamba wao walikuwa ndio wanawalipia ada wanafunzi bali walihusika sana kwenye hatua za mwanzo za kuangalia solution ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi...

Kwa maana nyingine, walihusika sana kwenye kujenga program foundation... labda tuseme kwenye framework.

Mkuu Chintu,

Kuna siku nilikuambia kuhusu requirements za ile program lakini sikuwahi kukupa evidence. Anyway, bado nimekosa direct source ya entry requiremets lakini doc hii ya Loan Board, nadhani itakupa mwanga:
Entry 01.png

Entry 02.png

Hizo ndizo requirements ambazo serikali ilikuwa ina-finance! Na kama nilivyosema, inawezekana ni kweli kulikuwa na Vilaza kama ambavyo Magu alidai lakini hiyo haikutokana na mahitaji ya program husika bali ujanja ujanja wa Watanzania ambao ndio hasa Magu alitakiwa kuufanyia kazi!!!

Lakini wakati wenye hizo sifa upande wa walimu Uncle Magu aliwaona vilaza, hizi ndio sifa za kujinga na Diploma ya Clinical Medicine:
Medicine.png

Je, inawezekana hiyo "....including D Passes..." kwenye Ordinary Diploma in Clinical Medicine imekosewa?! Lakini hata kama imekosewa, basi kilicho sahihi ndo hicho kilichopo kwenye Ordinary Diploma in Nursing & Midwifery.

If that's the case, kuna tofauti gani kati ya hizo requirements for special diploma in education (science) na ordinary diploma in Clinical Medicine? How come, wenye sifa zile zile, walipoenda kwenye special diploma in education, Mjomba Magu aliwaona vilaza lakini huku kwenye clinical medicine wanaonekana wapo okay?!

And I repeat, hawa wa special diploma in education walitakiwa kuipata kwa muda wa miaka 3 na program ouline yao inaonesha wangesoma tena kwa undani zaidi yale masomo waliyo-specialize. Sasa, yaani mtu awe amepata angalau C, kisha akakae tena darasani kwa miaka 3 na field practicals juu, halafu bado ashindwe kumfundisha mwanafunzi wa O-Level?

Lakini wakati hao watashindwa kuwafundisha watoto wa O-Level, wengine wenye sifa kama hizo wataweza kucheza na miili yetu! REMEMBER: Hawa wa Ordinary Diploma in Clinical Medicine wakifika kwenye Vituo vya Afya, hususani vya vijijini, wanakuwa ni "Madaktari" wanaoheshimika!!!

Labda Mdau Malcom Lumumba aje anipe darsa zaidi... what am I missing even after my thorough research?!
 
Last edited by a moderator:
Afadhali tunaziona ndege! Ndio level ya ujinga tuliyofikia, watu wanazoa fedha hazina wanakwenda kununua ndege bila kufuata taratibu za kisheria wala bunge kuridhia matumizi hayo halafu kama haitoshi wanazuia ukaguzi wa manunuzi hayo. Tunaona ni sawa! Sijui huu upoyoyo unatokana na nini
unalako jambo
 
Acha kupotosha!! Fuatilia hustles za kupata walimu wa sayansi... serikali ilianzia kutaka kuajiri wastaafu, ikashindikana kwa sababu walipatikana wachache!!

Baada ya kugonga mwamba kwa wastaafu, serikali ikaita waliomaliza PCMB miaka ya nyuma lakini hawakuwa na issue mtaani! Hawa walipangiwa kusomeshwa Special Advanced Diploma!!

Baada ya waliomaliza na kufaulu PCMB miaka ya nyuma kukosekana, ndipo pakawa hamna namna; likaja suala la Special Diploma kwa waliomaliza Form IV na kufaulu!! Kwahiyo hakuna cha suala la wajanja kupiga hela wala nini!!

View attachment 820820

Hapo juu ni Loan Board. Taarifa hiyo inathibitisha kwamba walikuwa wanalipiwa na serikali. Sasa hilo suala la watoto kutelekezwa kwenye majengo meupe sijui umelitoa wapi!!!

Lakini hata kama kuna wajanja walipiga pesa na kusepa; then what?! Baada ya Magufuli kufuta ile program, hizo pesa ndo zimerudi?! Hivi hudhani busara ilikuwa ni kuendelea tu na ile program kutokana na manufaa yake kwa sababu kuifuta isingesaidia kurudisha hiyo pesa iliyopigwa? Na kama palikuwa na mapungufu, busara ilikuwa ni kuifuta au kuiboresha?!

Mkuu magia, maelezo yako ni sahihi kabisa labda tu niongeze machache.

Ile program ilikuwa ni kwa ajili ya walimu wa sayansi wa primary and secondary schools. Nadhani hapa ndipo Magu alipopotishwa na watu wake.

Lengo ilikuwa ni kwamba, wale ambao walionekana kama hawakuwa na maksi za juu ilikuwa ni kwa ajili ya walimu wa shule za msingi na wenye maksi za juu ni kwa ajili ya walimu wa sekondari! Inawezekana utaratibu ulivurundwa lakini lengo lilikuwa hilo... na ndio jambo ambalo Magu alitakiwa kuhakikisha linafanyika!

Aidha, kama kumbukumbu zangu ipo sawa, ile program ilikuwa under World Bank sponsorship na sio Marekani! Hata hivyo, sio kwamba wao walikuwa ndio wanawalipia ada wanafunzi bali walihusika sana kwenye hatua za mwanzo za kuangalia solution ya kutatua tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi...

Kwa maana nyingine, walihusika sana kwenye kujenga program foundation... labda tuseme kwenye framework.

Mkuu Chintu,

Kuna siku nilikuambia kuhusu requirements za ile program lakini sikuwahi kukupa evidence. Anyway, bado nimekosa direct source ya entry requiremets lakini doc hii ya Loan Board, nadhani itakupa mwanga:
View attachment 820826
View attachment 820828

Hizo ndizo requirements ambazo serikali ilikuwa ina-finance! Na kama nilivyosema, inawezekana ni kweli kulikuwa na Vilaza kama ambavyo Magu alidai lakini hiyo haikutokana na mahitaji ya program husika bali ujanja ujanja wa Watanzania ambao ndio hasa Magu alitakiwa kuufanyia kazi!!!

Lakini wakati wenye hizo sifa upande wa walimu Uncle Magu aliwaona vilaza, hizi ndio sifa za kujinga na Diploma ya Clinical Medicine:
View attachment 820835

Je, inawezekana hiyo "....including D Passes..." kwenye Ordinary Diploma in Clinical Medicine imekosewa?! Lakini hata kama imekosewa, basi kilicho sahihi ndo hicho kilichopo kwenye Ordinary Diploma in Nursing & Midwifery.

If that's the case, kuna tofauti gani kati ya hizo requirements for special diploma in education (science) na ordinary diploma in Clinical Medicine? How come, wenye sifa zile zile, walipoenda kwenye special diploma in education, Mjomba Magu aliwaona vilaza lakini huku kwenye clinical medicine wanaonekana wapo okay?!

And I repeat, hawa wa special diploma in education walitakiwa kuipata kwa muda wa miaka 3 na program ouline yao inaonesha wangesoma tena kwa undani zaidi yale masomo waliyo-specialize. Sasa, yaani mtu awe amepata angalau C, kisha akakae tena darasani kwa miaka 3 na field practicals juu, halafu bado ashindwe kumfundisha mwanafunzi wa O-Level?

Lakini wakati hao watashindwa kuwafundisha watoto wa O-Level, wengine wenye sifa kama hizo wataweza kucheza na miili yetu! REMEMBER: Hawa wa Ordinary Diploma in Clinical Medicine wakifika kwenye Vituo vya Afya, hususani vya vijijini, wanakuwa ni "Madaktari" wanaoheshimika!!!

Labda Mdau Malcom Lumumba aje anipe darsa zaidi... what am I missing even after my thorough research?!
Mkuu.
Kwa qualification hizo hakuna ubishi kuwa iwapo kuna mwanachuo aliondolewa akiwa na sifa hizo basi kuna makosa yanayopaswa kuwa adressed.
Wabunge wetu watusemee hilo.
 
Tunamshukuru maana hata sisi maskini tutasafiri kwa ndege mpya za ATCL
 
Kumekuwa na critics nyingi juu ya anayoyafanya RAIS wetu.

Kuna wanaodai ndege sio kipaumbele na kwamba RAIS anapoteza pesa zetu kununulia ndege, kujenga Standard gauge, flyovers, viwanja vya ndege, Stiglers George, ukuta wa Merelani nk.

Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?

Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?

Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?

Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE.

Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Mkuu sina hakika kama ndege hizo ni muhimu kuliko usalama wa Watanzania wenzetu waliopotea na wengine kupigwa risasi mchana kweupe. Uhuru wa kutoa maoni na kumkosoa rais wetu una thamani kubwa kwa nchi yetu kuliko hizo ndege unazozifagilia. Mishahara ya wafanyakazi haina increment miaka mingapi sasa? Katiba yetu ina thamani kuliko hayo maendeleo unayoyaeleza hapa.
 
Kwani hujui kwamba tulikuwa na mafisadi na wahujumu uchumi? Hujui shirika la ndege la South Africa Airline lilichotufanya? Hujui Kenya ilichotufanya kwenye shirika letu la East Africa Airline ambalo tulikuwa tunalimiki kwa pamoja Kenya, Uganda na Tanzania? Au haya mambo yalitokea wakati hujazaliwa?
Wewe kweli unanuka maziwa, mie nazungumzia after 1977 baada ya EAA kufa. Tulikwisha kuwa na shirika linalojiweza mpaka ndege zinaenda mpaka mawilayani kama Nachingwea na Masasi, nini kilitokea? Tumejifunza?
 
Mishahara mkuu siku hizi inawahi balaa. Madeni (Halali sio yale ya kimadili) yamelipwa na yanaendelea kulipwa
Pesa mtaani ipo kwa anayefanya kazi. Kwa wazee wa madili imepotea
Mkuu.
Mishahara hajaongeza , madeni halali mengi tu hayajalipwa na mtaani ni kugumu
Akifanya hayo tutamkubali sana
 
Hivi lile dege lilinuliwa ili liae humu humu au ni majaribio tuu litaanza kusepa kimataifa...someone to clear this nielewe plz
 
mkuu kifikiria sana akili za watanzania wengi unaweza shindwa kulala.

wakati unakuja ambao kila mtu atamuelewa huyu mzee.

Tunamwelewa malaika mkuu mbona siku nyingi ana boss??
 
Umenena hakuna atakayeshindwa kuelewa.....maisha ya anasa ya viongoz wetu ndo yalikuwa yanatawala tuu.....kwa sasa yamepunguzwa japo bado wezi wapo tu......bora kuona kitu kuliko ukimya wa awali....Magufuli I will support u for ever.
 
Wewe kweli unanuka maziwa, mie nazungumzia after 1977 baada ya EAA kufa. Tulikwisha kuwa na shirika linalojiweza mpaka ndege zinaenda mpaka mawilayani kama Nachingwea na Masasi, nini kilitokea? Tumejifunza?
Mbona jibu la swala lako liko ndani ya jibu langu kwamba after 1977 = ufisadi, uhujumu uchumi + uporaji wa South Africa Airline katika shirika letu la ndege ndicho kilichotokea. Na hii ikasababisha hadi sasa shirika letu la ndege kuwa na madeni makubwa ya matrillion ya pesa.

Nimekwenda nyuma ya 1977 wakati tulikuwa na ndege kubwa kubwa za enzi hizo kama Concord na kadhalika ambazo tulikuwa tunazimiliki kwa pamoja sisi, waganda na wakenya kupitia EAC. Wakati tunamshughulikia nduli Amini wa Uganda aliyekuwa amevamia nchi yetu, wakenya wakavunja hiyo EAC na kupora ndege zote, treni zote na viwanda vyote. Baada ya vita dhidi ya nduli Amini, Tanzania na Uganda zikaanza upya wakati Kenya wanapeta na kuwa nchi ya uchumi wa kati wa viwanda. Sasa mimi ninakufundisha historia ya uchumi wetu tulikotoka, wewe unaniona ninanuka maziwa. Yaani babu yako anuke maziwa badala ya wewe mjukuu!
 
Nimekuona Wa ajabu kweli! Tulishamiliki Concord? Huelewi usemalo, unaijua Concord au unasema tuu? Uko kama uncle mnaropoka bila kujua msemacho
 
Nimekuona Wa ajabu kweli! Tulishamiliki Concord? Huelewi usemalo, unaijua Concord au unasema tuu? Uko kama uncle mnaropoka bila kujua msemacho
Tatizo ulikuwa hujazaliwa. East Afrca Airline ilikuwa ina compete na mashirika makubwa ya ndege kama British Airline. Vishirika kama Ethiopian Airline wakati huo vilikuwa havifui dafu kwa EAA! Kalagha baho. Kwaheli 😈.
 
Back
Top Bottom