Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

Ni afadhali Rais Magufuli tunaziona hata ndege

wazifanyie nini??kiendacho kwa mganga hakirudi….
Ndo basi tena, wataziona watakapoanza kusafirisha migebuka ndani ya masaa machache tu na kwa bei nafuu kutoka ziwa Tanganyika hadi Dar.
 
Ndo basi tena, wataziona watakapoanza kusafirisha migebuka ndani ya masaa machache tu na kwa bei nafuu kutoka ziwa Tanganyika hadi Dar.

mnh sio kupeleka Chato,ziende kubeba wafuga mg'ombe? au watalii wa mashamba?
 
Kwani ndege za precision na emirates hazipo ?
Mimi binafsi bora pesa iwe mtaani ,mishahara na madeni yalipwe basi
Mishahara mkuu siku hizi inawahi balaa. Madeni (Halali sio yale ya kimadili) yamelipwa na yanaendelea kulipwa
Pesa mtaani ipo kwa anayefanya kazi. Kwa wazee wa madili imepotea
 
Mnatuongezea deni la Taifa linalotafuna kodi zetu kwa miradi ambayo baadhi haina ulazima na mingine itakuwa ni majanga tu huko mbeleni.
 
Inaonekana kama Rais alipaswa kuzipeleka pesa hizo kwenye elimu, afya, kilimo, ajira nk.

Madai haya ni kama vile hizo pesa hapo awali zilikuwepo na zilikuwa zikienda huko wanakotaka ziende lakini sasa Magufuli amezichukua na kufanyia haya anayoyafanya.

Wenye akili tunayopaswa kujiuliza, tena kwa HASIRA na UCHUNGU -hivi hizo pesa huko nyuma zilikuwa zikienda wapi au zilikuwa zikifanyia nini?
Si Afadhali Magufuli ndani ya miaka miwili na nusu tu! tumeshaanza kugombania Vipaumbele na huku Ndege, Reli, ukuta, viwanja vya ndege tukiviona?
Huko nyuma kabla JPM hajaingia "tulipokuwa" na hivyo vipaumbele pesa ilikuwa ikienda huko kwenye elimu, afya na kilimo?
Afadhali JPM katufanya tuanze kujadiliana VIPAUMBELE
Hii ni dalili nzuri kuwa tupo kwenye RIGHT TRACK!
Sasa kwavile hata huko nyuma hizo pesa hazikupelekwa kule watu wanakoona ingefaa ziende ndo basi tena na Magufuli nae sio lazima apeleke huko na kwa maana hiyo anaweza kuwekeza kokote hata kwenye investments za hovyo?!

Hivi unaweza kueleza tofauti kati ya serikali iliyofanya ufisadi, kwa mfano, wa Sh. 100 Billion na serikali ambayo imewekeza Sh. 100 Billion kwenye white elephant project ambayo ina kila dalili ya kuendelea kunyonya akiba iliyobaki kwa kuhudumia hizo white elephant projects?!

Hapa hakuna cha afadhali kwa sababu bado kuna investment opportunities nyingi tu tena zenye direct and immediate impact kwa Watanzania!!!

Moja ya sifa ya kiongozi bora ni kufanya maamuzi yaliyo sahihi!! Maamuzi yako yatapimwa kwako na si kwa kuangalia wenzako walifanya nini!!!!

I hate to say this lakini ukweli ni kwamba, ingawaje serikali ya JK ilijaa ufisadi lakini ilikuwa inafahamu ianze na nini kisha igeukie nini!!!

Heri ya mtu anayeiba sh. 30 lakini sh.70 anawekeza kwenye right investments kuliko mtu ambae haibi hata senti 5 lakini ni sh.25 tu ndio zinaenda kwenye right investments huku 75 zote zikienda kwenye investments za hovyo hovyo ambazo zina kila dalili za kuendelea kuligharimu taifa siku za usoni!!!
 
Mnatuongezea deni la Taifa linalotafuna kodi zetu kwa miradi ambayo baadhi haina ulazima na mingine itakuwa ni majanga tu huko mbeleni.
Hakuna nchiimewahi kufungwa kwa madeni.
Wacha tudaiwe huku tukiwa na UMEME wa uhakika, USAFIRI wa uhakika na huku madini yetu yakitulipa kwa UHAKIKA
 
Dada ulitaka wote tukafanye kazi kwenye ndege?
Haohao watakaopata ndo riziki yao na watatupunguzia msongamano kwenye kazi zingine

wewe huelewi,nilikua namaanisha hilo lindege litapunguzaje unemployement?? yaani unafurahi watu kumi kati ya miambili kupewa kazi wakati kulikua na possibility ya Zaidi ya hao kupata kazi?
 
"Binadamu kazi"
Kuongoza nchi ni kazi watu wanashindwa kuendesha familia ila wanaona haki kuponda nchi inavyoendeshwa.
Watu wajiulize kwenye familia zao wamefanya nini na nini wanacho kinachoonekana ni hatua kwao kimaendeleo.
Haaaahaaaaa
Kuongoza nchi ni kazi tena ni kazi kweli kweli. Hongera Rais kwa machache ufanyayo. Mungu akubariki.

Mbona mnakuwa na maoni ya kujipendekeza? Ni mkosoaji gani alipeleka familia yake magogoni akasaidiwe kisa ameshindwa kuihudumia?
 
Back
Top Bottom