Nguvu za Mungu kwa Daudi kumshinda Goliati kwa jiwe la kombeo

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Kwenye vita za zamani kulikuwa kuna utaratibu kabla vita haijaanza inabidi kila upande ukae umbali wa takribani mita 400 (viwanja vinne vya mpira), hivyo kulikuwa na eneo kubwa la wazi kati yao, kila upande ulipeleka mpignaji wao mahiri katikati ya hilo eneo la wazi kupigana ANA KWA ANA mpaka kifo kwa kutumia ngumi, mateke, sambamba na kutumia silaha kama mapanga, rungu, visu, ngaao, mkuki, n.k , baada ya hapo ndio vita ilianza.

Daudi alichaguliwa awe mwakilishi wa pambano hilo huku upande wa pili walimchagua Goliati kwa umahiri wake wa kupigana ana kwa ana, ila cha ajabu Daudi alienda na silaha ya masafa marefu kwenye mapigano ya ana kwa ana, kwa mbali alipoona Goliati anakuja akaweka jiwe kwenye kombeo akalenga kichwa cha Goliati, Kwa wale waliowahi kuuona uwezo wa jiwe la kombeo wanajua kombeo linabeba jiwe kubwa kuzidi manati na jiwe linafika mbali zaidi kwa nguvu zaidi, jiwe moja kombeo linaweza kuua nyati !

Ukiwaona watu wanavyomsifia Daudi kuwa ni shujaa kunaibua sana maswali, utasikia "alimpiga kwa kombeo jiwe moja tu kichwani"

Kuna watu wanatetea kwamba Daudi alijitolea hakuwa mwanajeshi, Hata wanajeshi wetu wa wa JWTZ huwa wanaanza kwa kujitolea JKT, hata vita ya Kagera wanajeshi kibao walijitolea, hata nae Daudi aliingia jeshini kwa kujitolea. hata kama hakuwa na mafunzo kitendo cha jeshi kumruhusu ashiriki vita tena kwenye combat roles huyo tayari ni mwanajeshi.

Pia kutetea Daudi alikuwa kijana mdogo ni hoja dhaifu, kwa wastan tunaweza kukadiria alikuwa na miaka 16, nchi zilizo vitani ni kawaida kukuta watoto wenye miaka 10 wanafundishwa kutumia silaha za mbali kama bunduki kuzitumia kushambulia watu wazima.
 
Wewe na huo utu uzima wako unaweza kupigana na mtoto mdogo mwenye shahaha aliepewa pisto yenye risasi moja tu ?

Mtoto akikulenga kichwani ni kwamba ana nguvu kukuzidi ?
Mkuu hii ndio maana ya mtoa mada kwamba pale hakukua na miujiza isipokuwa ni hesabu tu Daud alipiga, ni kama mtu yeyote akienda kuwinda nyati usitegemee ataenda kumkamata kwa mikono ila atamvizia kwa siraha kulingana na hesabu zake.
 
Daudi alichaguliwa awe mwakilishi wa pambano hilo huku upande wa pili walimchagua Goliati kwa umahiri wake wa kupigana ana kwa ana
We sio msomaji wa Biblia acha kuandika uongo, Daudi hakuchaguliwa kupigana na Goliath, bali alijitolea kwa hiari yake mwenyewe kumnyamazisha huyo jamaa mwenye tambo.

Daudi hakuwa katika kikosi cha vita bali alienda tu huko kama raia mchunga kondoo na akakuta Goliath akiwa anatamba hadharani huku Sauli na watu askari wake wakiwa na hofu kupigana na huyo Goliath.

Ni vyema kusoma vyema kisa ndipo uje ulete ukosoaji wako.
 
Hiki kitu nlitoka kumwmbia mtu Jana.....
Pia kuna movie inaitwa David...inaelezea historia ya daudi.
Haikuwa miujiza Bali n hesabu za daudi Tu zilikubali....Kwa maana hawakupigana ila daudi ndiye alimpiga Goliath Kwa jiwe tena kwenye kombeo......hatuwez kukataa fact Kua daudi alikua shujaa lakin tuache kujidanganya Kua ule n muujiza
 
Ile ni drone ilimlenga Goliath, watu wanafikiri hizi technology zimeanza kizazi hiki.

Hata ile hadithi ya Yoshua na kuta za Yeriko, kwamba zilipigwa tarumbeta kuta zikaanguka.
Pale inasemekana F35 ilipita ikashambulia kwa makombora.
 
Mkuu ebu fafanua nini maana ya MUUJIZA ?
 
Afadhari mtumishi umetupa ufafanuzi
 
Hiki kitu nlitoka kumwmbia mtu Jana.....
Pia kuna movie inaitwa David...inaelezea historia ya daudi.
Haikuwa miujiza Bali n hesabu za daudi Tu zilikubali....Kwa maana hawakupigana ila daudi ndiye alimpiga Goliath Kwa jiwe tena kwenye kombeo......hatuwez kukataa fact Kua daudi alikua shujaa lakin tuache kujidanganya Kua ule n muujiza
Sisi watumishi tunachojua daudi alimsogelea goliath kwa imani aliyo kua nayo kwa Mungu wake, yakua Mungu wake atamshindia.

Hivi ndivo bibilia inavo tuambia.

Maswala ya mahesabu/Miujiza au ndoto ni ya kwetu sisi wasomaji. Ila daudi mwenyewe aliona bila kwenda na Mungu wake hatoboi hizo hesabu zenu
 
Daudi hakutengwa na jeshi la Israel kwamba yeye ndiye mpiganaji wao, alikuwa ni mdogo kiumbo na kiumri, Jeshi la Israel walikuwa wamejificha wakati Goliathi akitamba na kutukana, kwahiyo kuibuka kwa Daudi na kumshushia kipigo ilikuwa muujiza kwa jeshi la Israel hata kwa wafilisti wenyewe walishangaa imekuaje kamanda wao tegemezi ameshushwa bisha na kijana mdogo hiyo ilikuwa muujiza out of expectations
 
Ile ni drone ilimlenga Goliath, watu wanafikiri hizi technology zimeanza kizazi hiki.

Hata ile hadithi ya Yoshua na kuta za Yeriko, kwamba zilipigwa tarumbeta kuta zikaanguka.
Pale inasemekana F35 ilipita ikashambulia kwa makombora.
Hahaha mkuu ukianza kuweka habari za "inasemekana" unakuwa huna tofauti na hao wanaoamini hayo ambayo wewe unaona ni uongo, yani unakuwa unapinga uongo halafu nawe hapo hapo unapachika uongo wako mwingine, inatakiwa unachokisema kiwe proven beyond doubt siyo tena kuleta habari za kufikirika
 
Eeh! We unafikiri Yona alimezwa na samaki mkubwa? Eti baadae akamtema ufukweni, Ile ni nyambizi ni ile tu watu wa kipindi kile walikua hawafahamu nyambizi zipo, wakadhani ni samaki.

Hata Artficial intelligence ilikuwapo zamani sana.
Andiko.
Yoshua 8 : 20.
20 Kisha hapo hao watu wa Ai walipotazama nyuma yao, wakaona, na tazama, moshi wa huo mji ulikuwa unapaa juu kwenda mawinguni, nao hawakuwa na nguvu za kukimbia huku wala huku; na wale watu waliokuwa wamekimbia kuenenda nyikani wakageuka na kuwarudia hao waliokuwa wakiwafuatia.

Sasa unaona hapo kwenye Ai ulikuwa ni mji wa Ai, tech zote za artificial intelligence ni hapo.
Usije shangaa punda wa Balaamu aliwezaje zungumza, huo mji wa Ai walitengeneza robot akama watu na wanyama pia.
 
We sio msomaji wa Biblia acha kuandika uongo, Daudi hakuchaguliwa kupigana na Goliath, bali alijitolea kwa hiari yake mwenyewe kumnyamazisha huyo jamaa mwenye tambo.

Daudi hakuwa katika kikosi cha vita bali alienda tu huko kama raia mchunga kondoo na akakuta Goliath akiwa anatamba hadharani huku Sauli na watu askari wake wakiwa na hofu kupigana na huyo Goliath.

Ni vyema kusoma vyema kisa ndipo uje ulete ukosoaji wako.
Kujitolea kupigana ndio huko huko tu kwamba akawa chaguo la kuliwakilisha jeshi la nchi yake,
 
Sisi watumishi tunachojua daudi alimsogelea goliath kwa imani aliyo kua nayo kwa Mungu wake, yakua Mungu wake atamshindia.

Hivi ndivo bibilia inavo tuambia.

Maswala ya mahesabu/Miujiza au ndoto ni ya kwetu sisi wasomaji. Ila daudi mwenyewe aliona bila kwenda na Mungu wake hatoboi hizo hesabu zenu
Kombeo ni silaha ya masafa ya mbali sio ana kwa Ana, kombeo inabidi uweke jiwe kisha uanze kuizungusha kuliachia jiwe, ni zoezi la sekunde kama kumi hivi, huo muda wote ni dhahiri walikuwa hawajakutana ana kwa Ana, kuna vitu sio vya kuumiza kichwa, ni suala la kuangalia vitu unatumia hata akili ya kawaida.

Kombeo ukijua kuitumia unaweza kuua hata nyati akiwa mbali, hakuna haja ya kukutana ana kwa Ana, unapiga kichwani akiwa mbali shughuli imeisha
 
Back
Top Bottom