Wakili Msomi Mwabukusi; Je, ndiye 'Daudi' wa Tanzania au tumtazamie mwingine?

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,893
3,200
Nawasalimu kwa jina la Bwana.

Leo nimekumbuka kisa kilichoandikwa kwenye Biblia, 1 Samweli 17.

Sura hii kwa ufupi inahusu kisa cha kijana mdogo Daudi na Goliathi. Daudi alikuwa ni mchunga kondoo ambaye hakuwa na uzoefu katika masuala ya vita ilhali Goliathi alikuwa ni mpiganaji mwenye uzoefu wa muda mrefu jeshini. Sifa za Goliathi na umbile lake la kutisha liliwaogopesha sana wanajeshi wa Kiisraeli ambao walikimbia kila shujaa huyo alipoinuka kuwatukana na hakuna aliyethubutu kwenda kupambana naye.

Hata Mfalme Sauli (kiongozi wa Israeli wakati huo) mwenyewe, alimwogopa sana. Kwa bahati mbaya alikuwa ameshavunja mahusiano yake na Mungu wa Mbinguni ambaye alikuwa akilipigania Taifa hilo dhidi ya maadui zao.

Ndipo katika hali ya kukata tamaa huko, akaibuka kijana Daudi na kujitolea kwenda kupambana na hilo jitu la kutisha Goliathi.

Mungu mwema, kupitia kwa kijana ambaye hakuwa na uzoefu wa kivita, wala hakuwa maarufu kwa watu, wala hata hakuwa na zana bora za kivita, aliweza kumwua Goliathi kwa kutumia kombeo (manati) na jiwe!

Vivyo hivyo, kwa hali inayoendelea hapa kwetu, ni kana kwamba tunakabiliana na Goliathi, ambaye kila mmoja anamwogopa.

Lakini kaibuka Wakili Msomi Mwabukusi kuhakikisha raslimali za nchi na wananchi vinalindwa dhidi ya mikataba ya hovyo.

Nimalizie kwa kumwombea shujaa wetu huyu, Mungu ambariki sana, yeye na familia yake pamoja na ukoo wake wote kwa ujumla. Mungu wetu amjalie kuwa kiongozi mkubwa kabisa wa nchi yetu kwa maana anastahili. Mungu azidi kumjalia hekima na busara za kuendelea kutututetea Wananchi pamoja na rasilimali zetu. Zaidi ya yote, Mungu amlinde na kumtunza shujaa wetu huyu dhidi ya kila baya kama alivyomtunza Mfalme Daudi. Wote watakaoinuka kinyume cha Wakili Msomi Mwabukusi, walaaniwe wao pamoja na vizazi vyao.

AMIN.
 
Advocate Mwabukusi ni Mtanganyika na Mzalendo wa Kweli
F4Td0_ya0AAJm4w

Anahitaji uungwaji mkono wa hali ya juu. Juu zaidi ya uungwaji huu unaoonekana.
Mwenyezi mungu amuongezee hekima busara na ujasiri tele.
 
Nasikitika sana kuhusu Bunge letu.
Yani Bunge limebaki kuitikia tu kila kinacholetwa na Serikali.

Leo hii tunawategemea watu binafsi kuliokoa Taifa letu dhidi ya uvamizi wa maharamia wanaokuja na vazi la kondoo.

Leo hii tunawategeme viongozi wachache wa Dini kufanya kazi ya Bunge.

Hivi Wabunge wote kweli hawakuliona hili?
Yaani Bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa kamiliki kakampuni kamoja ka huko Dubai kweli ?

Kampuni ambayo tunaweza kuiajiri na tukailipa.
Hili Bunge tutaliamini vipi tena kesho ?

Binafsi nawashukuru sana SHURA YA MAIMAMU TANZANIA na BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA kwa kusimamia kidete bila kupepesa macho na kulitetea Taifa letu kwa jasho na Damu.

Kama Mlinzi wetu Mkuu anakavulia madaraka yake kakampuni ka mji wa Dubai hakika ametukosea sana.

Tulimwamini sana na kumtegemea bila wasi wasi.
Sasa hivi tuna wasiwasi mkubwa sana na vyombo vyetu vya ulinzi wa raslimali zetu.
 
Cha msingi

Kaka Ake kikazi ambaye ni LISU ,msomi mwezake akazane kupiga Sipana Kanda zahuko aliko ,Ili aingie Zanzibar akafunge majadala

Zito ,kabwe atafute pakutokea

Dp world ya Tanzania ijitafakari upya mana Dubai yawezekana kisingizio , kitendo Cha bunge kugomea jambo ,ni mtikisiko
 
IMG-20230829-WA0091.jpg
 
Dp world ya Tanzania ijitafakari upya mana Dubai yawezekana kisingizio , kitendo Cha bunge kugomea jambo ,ni mtikisikoView attachment 2732985
Nimeona Uturuki Kuna Bandari wamiingia Ubia na DP W Kwa mgao wa asilimia 52 Kwa 48 sio sawa na huu wa Mama
Nahuhakika mkataba wetu ilikuwa na jambo la Siri Sana ndiyo maana tukaanza kuona akina Abduli wanaenda Kwa Mu7 kuuza Ummeme Sola
Haya mambo yatakuja kujulikana tu
Kitenge na New modell Prado
Masikini akipata matako hulia mbwata walio andika methali sio wajinga tutajua tu nawatu wataabika mchana kweupeee
 
Nawasalimu kwa jina la Bwana.

Leo nimekumbuka kisa kilichoandikwa kwenye Biblia, 1 Samweli 17.

Sura hii kwa ufupi inahusu kisa cha kijana mdogo Daudi na Goliathi. Daudi alikuwa ni mchunga kondoo ambaye hakuwa na uzoefu katika masuala ya vita ilhali Goliathi alikuwa ni mpiganaji mwenye uzoefu wa muda mrefu jeshini. Sifa za Goliathi na umbile lake la kutisha liliwaogopesha sana wanajeshi wa Kiisraeli ambao walikimbia kila shujaa huyo alipoinuka kuwatukana na hakuna aliyethubutu kwenda kupambana naye.

Hata Mfalme Sauli (kiongozi wa Israeli wakati huo) mwenyewe, alimwogopa sana. Kwa bahati mbaya alikuwa ameshavunja mahusiano yake na Mungu wa Mbinguni ambaye alikuwa akilipigania Taifa hilo dhidi ya maadui zao.

Ndipo katika hali ya kukata tamaa huko, akaibuka kijana Daudi na kujitolea kwenda kupambana na hilo jitu la kutisha Goliathi.

Mungu mwema, kupitia kwa kijana ambaye hakuwa na uzoefu wa kivita, wala hakuwa maarufu kwa watu, wala hata hakuwa na zana bora za kivita, aliweza kumwua Goliathi kwa kutumia kombeo (manati) na jiwe!

Vivyo hivyo, kwa hali inayoendelea hapa kwetu, ni kana kwamba tunakabiliana na Goliathi, ambaye kila mmoja anamwogopa.

Lakini kaibuka Wakili Msomi Mwabukusi kuhakikisha raslimali za nchi na wananchi vinalindwa dhidi ya mikataba ya hovyo.

Nimalizie kwa kumwombea shujaa wetu huyu, Mungu ambariki sana, yeye na familia yake pamoja na ukoo wake wote kwa ujumla. Mungu wetu amjalie kuwa kiongozi mkubwa kabisa wa nchi yetu kwa maana anastahili. Mungu azidi kumjalia hekima na busara za kuendelea kutututetea Wananchi pamoja na rasilimali zetu. Zaidi ya yote, Mungu amlinde na kumtunza shujaa wetu huyu dhidi ya kila baya kama alivyomtunza Mfalme Daudi. Wote watakaoinuka kinyume cha Wakili Msomi Mwabukusi, walaaniwe wao pamoja na vizazi vyao.

AMIN.
Kwa hiyo huyo mlevi amekushawishi nini wewe? Hivi unadhani kigezo cha uongozi ni uropokaji? Zaidi ya kuropoka nini kingine anajuwa?

Achana na takataka hiyo
 
Advocate Mwabukusi amewaingizia CCM mbu kwenye neti...
Yule jamaa ana maneno ya kukarahisha, kuchekesha na kuudhi mno....
Kiufupi hata kama hukubaliani naye, ila watu iana yake ni muhimu sana kwenye nchi....
Yaani wee aacha tu, hapa nilipo nacheka tuu, alifurahisha pale alipowambia serikali kuhusu huo mswada wa marekebisho ya maliasili, eti kwa vile wachungaji wamewakataza umalaya waumini wao wametaa sasa dawa iliyopo kuweka kipengele cha kukubaliana na huo umalaya kwenye biblia.
 
Hivi Serikali na Bunge letu hawaangalii kabisa mikataba mingine ambayo kampuni flani inaaingia na nchi fulani ili kujifunza?

Mfano wangemwambia DPW
Tunaomba Mkataba wako na Uturuki tuone mlivyo kubaliana hadi ukawekeza huko.

Tunaomba mkataba wako na Wingereza ambako ukawekeza katika Bandari moja tu.

Hili Msomi wa PHD Musukuma halioni kweli

Au ndio cha awumbile Mulungu cha Kumemena.
 
Nasikitika sana kuhusu Bunge letu.
Yani Bunge limebaki kuitikia tu kila kinacholetwa na Serikali.

Leo hii tunawategemea watu binafsi kuliokoa Taifa letu dhidi ya uvamizi wa maharamia wanaokuja na vazi la kondoo.

Leo hii tunawategeme viongozi wachache wa Dini kufanya kazi ya Bunge.

Hivi Wabunge wote kweli hawakuliona hili?
Yaani Bandari zote za Bahari, Mito na Maziwa kamiliki kakampuni kamoja ka huko Dubai kweli ?

Kampuni ambayo tunaweza kuiajiri na tukailipa.
Hili Bunge tutaliamini vipi tena kesho ?

Binafsi nawashukuru sana SHURA YA MAIMAMU TANZANIA na BARAZA LA MAASKOFU TANZANIA kwa kusimamia kidete bila kupepesa macho na kulitetea Taifa letu kwa jasho na Damu.

Kama Mlinzi wetu Mkuu anakavulia madaraka yake kakampuni ka mji wa Dubai hakika ametukosea sana.

Tulimwamini sana na kumtegemea bila wasi wasi.
Sasa hivi tuna wasiwasi mkubwa sana na vyombo vyetu vya ulinzi wa raslimali zetu.
Unasikitika nini sasa...
Yaani unahisi bunge la ccm litamfanya nini Rais SSH mwenyekiti wa ccm?
Vitu vingine mjifunze kwenye historia!
Wakati umefika bunge liwe na uwakilishi yakinifu wa vyama vingi
 
Kwani maana ya kuishauri Serikali nini ?

Au unamaanisha kila anachoamua Raisi Bunge letu linakubali.

Basi hakuna haja ya kuwa na Bunge.

Raisi anatosha.
Bunge Livunjwe.
 
Kwenye listi umesahau wafuatao Dr,slaa,wapo wachungaji na maaskofu baadhi wa kipentekoste nikiipata orodha yao nitakutumia hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom