Mataifa yenye nguvu ya silaha za nyuklia duniani

BANDOKITITA

JF-Expert Member
Oct 4, 2022
1,176
2,279
Yafuatayo ni mataifa 9 yenye uwezo mkubwa wa silaha hatari za nyuklia duniani.

1. Urusi
Pamoja na kupunguza hifadhi zake za nyuklia tangu kumalizika kwa vita baridi (Machi 12, 1947 – Desemba 3, 1989), Urusi na Marekani zinamiliki asilimia 90% ya silaha zote za nyuklia duniani. Lakini Urusi ni kinara ikiwa na umiliki wa asilimia 47.7% kwa takwimu za mwaka 2021, kwa mujibu wa chama cha udhibiti wa silaha cha Marekani.
Kwa mujibu wa mtandao wa Worldpopulationreview Urusi ina vichwa 6,255 vya silaha za nyuklia, ikiwemo RS-28 Sarmat au Satan 2 yenye uwezo mkubwa wa kusafiri umbali mrefu na kuleta madhara makubwa.

2. Marekani
Miaka takribani 80, imepita tangu Marekani iangushe bomu la nyuklia katika mji wa Hiroshima nchini Japan na kuua makumi ya maelfu ya watu papo hapo, wengine makumi ya maelfu walifariki dunia baadaye na wengine wengi miaka iliyofuatia.
Kwa sasa Marekani ina silaha hizo 5,550.

3. China
China inatajwa kutumia fedha nyingi kuwekeza kwenye jeshi lake huku silaha za nyukilia zikiwekewa mkazo. Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm, ambayo inachapisha tathmini ya kila mwaka ya jumla ya hifadhi za dunia za silaha za nyuklia, inasema China imeongeza idadi yake ya silaha hizo za kivita katika miaka ya hivi karibuni.
Mwezi Novemba, Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitabiri kuwa China ingetumia silaha zake za nyuklia ifikapo mwishoni mwa muongo mmoja. Alisema China “huenda inakusudia kuwa silaha za aina hiyo 1,000 ifikapo mwaka 2030.”
Hata hivyo Vyombo vya habari vya serikali ya China viliuita utabiri huo kuwa “uvumi wa uwongo na wa upendeleo,” ukibainisha kuwa silaha za nyuklia ziko katika “kiwango cha chini.” Ripoti inasema China ina silaha za nyukilia 350, lakini ujenzi wake wa nyuklia unachukuliwa kuwa moja ya vitisho vikubwa kwa nguvu za kijeshi za Magharibi.

4. Uingereza
Taifa hili haliko nyuma pia kwa idadi ya silaha za nyuklia ikiwa na silaha 225 za nyuklia. Katika mzozo wa Ukraine Uingereza pia imeonyesha kutofurahishwa na uvamizi wa Urusi.

5. Ufaransa
Taifa la Ufaransa haliko mbali na China, likiwa na silaha za nyuklia zipatazo 290 sawa na asilimia 2.21% ya silaha zote za nyuklia duniani.

6. Pakistan
Kwa upande wa Pakistan mwaka 2020 iliongeza kuongeneza vinu vitano vya nyuklia na kufikisha vinu 165 vya silaha za nyuklia.

India, Israel na Korea Kaskazini
Mbali na nchi hizi ziko nchi zingine zinazomiliki silaha hizo ni India, Israel na Korea Kaskazini. India ina silaha za nyuklia 160 sawa na asilimia 1.22% ya silaha zote za nyuklia duniani, Israel 90 (0.69%) na Korea Kaskazini inazo 45 sawa na asilimia 0.34%

 
Back
Top Bottom